RAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU TRA























RAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU TRA

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano - Ikulu imesema kuwa alasiri ya leo, Rais Dk. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Rished Bade.

Rais amemteua Kamishna Phillip Mpango kukaimu nafasi hiyo; na amemtaka Rished Bade kumpa ushirikiano Mpango hasa katika kutafuta ukweli kuhusu makontena 349 yenye thamani ya shilingi bilioni 80/= yaliyotoweka bandarini pasipo TRA kuwa na kumbukumbu zozote za makontena hayo.

VIGOGO WA TRA WAKUTANA NA MOTO WA MAJALIWA.












Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.
Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.

Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Katika Ziara hiyo ya ghafla Waziri mkuu Kasim Majaliwa awasimamisha kazi kamishna wa kodi Tiagi Masamaki na Habibu Mpozya kitengo cha huduma kwa wateja kutokana ubadhilifu wa fedha kwa makontena zaidi ya 300 yaliyopotea.

Wengine ni Haruni Mpande -ICT, Hamisi Ali Omari na Eliachi Mrema incharge wa ICD na amemuru wote wakamatwe uchunguzi uendelee.

HUKUMU YA MAWAZO, MBOWE MPONGEZA JAJI.




HUKUMU YA MAWAZO, MBOWE MPONGEZA JAJI.
leo mahakama ya Tanzania imetenda haki kama ilivyo elezwa na mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Freeman Aikaeli Mbowe.
Ndugu wa mawazo, marafiki, na wanachama wwnzake wameruhusiwa kutoa heshima zao za mwisho kwa mawazo, katika uwanja ambao watakubalina kati ya CHADEMA, ndugu na polis.
Kwa kwa muda wa siku mbili sasa kumekuwa majibishano ya kisheria kati ya jeshi la polis na familia ya Mawzo iliyo wakilishwa na wakili Mallya, majibishano hayo yalitangiliwa na sinto fahamu ya namna ya kuagwa na kuzikwa kwa Mawazo baada ya jeshi la polis kuzuia mkusanyiko mkubwa wa watu kwa sababu ya tishio la kipindupindu.

MARUFUKU KUTENGENEZA KADI ZA X MAS KWA GHARAMA ZA SERIKALI.


Sijui kesho tutasikia nini maana yake hii sasa imeshakuwa hatari, ofisi za umma zimekuwa kaa la moto kwa watumishi. Huyo ndio Magufuli,,, ni kazi tu.

URUSI YAZIDI KUONGEZA NGUVU SYRIA.



URUSI YAZIDI KUONGEZA NGUVU SYRIA.

Haya ni magari ya Jeshi la Urusi ya kubeba na kurusha makombora aina ya S-400 Triumf ambayo yanapiga toka ardhini kwenda angani , hivi sasa yanaelekea huko Latakia , Syria katika kambi ya Jeshi la Urusi inayohusika na mashambulio dhidi ya makundi ya kigaidi huko Syria na Ira qi .

Urusi imefanya hivyo baada ya ndege yake aina ya Sukhoi Su-24 kutunguliwa na Uturuki juzi.
Mfumo huu wa makombora unauwezo wa kupambana na maadui 300 kwa wakati mmoja , Pia wanapeleka Makombora yanayoongozwa na meli yanayoitwa Moskva karibu na pwani ya Syria sehemu ambayo ni Karibu kabisa na Uturuki .

AJIRA SERIKALINI SASA KWA MKATABA WA MUDA MAALUMU:


AJIRA SERIKALINI SASA KWA MKATABA WA MUDA MAALUMU:
Atakayefanya vizuri ataendelea na mkataba, atakayevurunda kufutwa kazi mara moja.
Taarifa kuhusu mpango wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano kuzifanyia mabadiliko makubwa sheria za Utumishi wa Umma kwa kuondoa kipengele cha Ajira ya Kudumu (Permanent Employment Contract) kimepokewa kwa hisia chanya na jamii.

Kwa miongo mingi utendaji katika sekta ya Utumishi wa Umma umekuwa ukilegalega, kuzorota na kutokuwa wa ufanisi kiasi sio tu mara kadhaa umepelekea kuingiza Serikali katika hasara ya mabilioni ya shilingi lakini pia imekuwa sababu ya kero kubwa kwa wananchi wanaokosa huduma na maamuzi stahiki katika ofisi za umma.

Sababu kuu inayotajwa kuchangia uzembe, utoro, uvivu, kutowajibika, ufujaji wa fedha za umma, manyanyaso kwa wananchi, ulevi, wizi, rushwa, ufisadi, undugunization n.k ni kwa kuwa baadhi ya watendaji hawa wa umma mikataba yao ya ajira ilikuwa ni ya kudumu na yenye pensheni (Permanent and Pensionable).

Kigezo hiki cha permanent and pensionable kimekuwa kikitumiwa vibaya sana na baadhi ya watendaji kwenye ofisi za umma kufanya kazi vile wanavyotaka wao. Hata inapobainika mfanyakazi ni mzembe kabisa kabisa ambaye hawezi kutimiza majukumu yake kumfukuza kazi linabaki kuwa jambo gumu sana ambalo hata Waziri hawezi na wengi huishia kuhamishwa vituo vyao vya kazi na kuendelea na matendo yao yasiyo na ufanisi katika utumishi.

Bunge kama chombo cha kutunga sheria kinapaswa bila woga kutimiza majukumu yake ikiwemo kurekebisha kwa kufuta vipengele vyote vya sheria ya Utumishi wa Umma ambavyo vimekuwa kichaka kwa baadhi ya watumishi kufanya mambo ya hovyo wakiamini hawagusiki.
Bunge likifanikiwa kuziboresha sheria hizi za Utumishi wa Umma tunaamini zitasaidia kurejesha Nidhamu Kazini, kuongeza ari ya Uwajibikaji, kuondoa migongano, migogoro, kupunguza hasara kwa Serikali zisizo za lazima, kutoa mwanya kwa watendaji wenye sifa kidhi kuajiriwa katika sekta ya umma na kusukumu mbele gurudumu la Maendeleo.

Miaka ya 1980's kulikuwa na kibao mashuhuri chenye maneno;
"Nidhamu ya Kazi ni msingi wa mafanikio mema kazini, viongozi na wafanyakazi, lazima wote muwe na nidhamu.
Migogoro na migongano makazini ni ukosefu wa nidhamu".
Katika kuifumua na kuisuka upya nchi yetu, tunaunga mkono juhudi zote njema zenye kulenga kuwa na Taifa lenye kuzingatia misingi ya Uzalendo, Uwazi, Uwajibikaji, Uadilifu, Umoja, Udugu, Utu na Utawala wa Sheria.
Viva Tanzania! Viva!

MAPENZI SI MAFURUSI.
















 MAPENZI SI MAFURUSI.
1.
Katu hapandi farasi, yule mzoea punda,
Mpenda kwenda kasi, mwendo pole humshinda,
Amezoweshwa fenesi, doriani lamshinda,
Sitokalifisha nafsi, nafanya ninayopenda,
Mie nina wasiwasi, kwa mambo yanavyo kwenda.
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.
2.
Nipe gongo ya kiasi, nipate ipiga funda,
Na miraa ya Ramisi, kwa ubani naifunda,
Initoe wasiwasi, hata kipoe kidonda,
Niupate na wepesi, wa kumshukia nyonda,

Natambua si rahisi, kutamka "nakupenda"
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.
3.
Niko na pepo za kusi, ni mbali ninapo kwenda,
Nausaka mdungusi, ukame 'sikose tunda,
Wenye kupendwa wakwasi, kila kiwanja hudunda,

Niache kikaragosi, nilo nayo yanishinda,
Mkononi sina tasi, n’nani atanipenda?
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.
4.
Waja wataka fususi, hawana kitu kupenda,
Ubishi kama chunusi, natafuta pa kupanda,
Aso tabia za fisi, wallahi nitampenda,
Mwenye kujali nafsi, mafurusi kuyaponda,
Mapenzi ya wasiwasi, yatesa kama kidonda.
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.
5.
Moyo una wasiwasi, akili i'njia panda,
Huyu mja Ibilisi, ni jini msaka tenda,
Kila siku alhamisi, kwake siku huganda,
Kuna siku za mafurusi, na za mifuko kukonda,
Si kuna siku nyepesi, na za kukaza mkanda?
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.
6.
Hili jua la utosi, kila mtu humtenda,
Hata mwenye ukwasi, pia laweza mponda,
Ya jini kuhama rasi, kitie anapo konda,
Mwayaiga pasi wasi, ya majini mwayatenda,
Kwa talasimu za ngisi, mioyo mnaiwinda.
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.
7.
Sina hofu sina wasi, tena nenda mwana kwenda,
Kisu changu kimepasi, hakiyumbi kimedinda,
Hupati tena nafasi, dagaa zangu kutanda,
Nimestushwa na unyasi, nyoka alinipa donda,
Nimestuka kirahisi, we endelea kutanda.
Ukipendwa kwa pesa, taachwa kwa kuzikosa.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
Mzalendo.njano5@gmail.com
784845394/764845394
Morogoro Tanzania.

SIASA MJUE NJIA, MAAMUZI KUFIKIA.












SIASA MJUE NJIA, MAAMUZI KUFIKIA.
1
Nimezama mwituni, kumtafuta mnyama,
Mwenye nguvu duniani, leo na kesho kiama,
Atajwa msikitini, kanisani wa msema,
Haliwi jambo mwituni, bila ya huyo mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
2
Naanzia shuleni, watoto wanaposoma,
Wanao soma vyuoni, na shahada za heshima,
Ngumbaru ipo kundini, unyago akina mama,
Elimu yetu nchini, huongozwa na mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
3
Uende sipitalini, na walipo wakulima,
Kwenye sekta ya madini, na kwa wapiga ngoma,
Utalii wa mbugani, uchezaji wa sinema,
Kote huko tambueni, mratibu ni mnyama.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
4
Siasa ndio mnyama, Lutumbo katuambia,
Siasa ni kitu chema, katika yetu dunia,
Siasa njia ya umma, maamuzi kufikia,
Siasa si kama sima, bali maji nawaambia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
5
Siasa kitu lazima, katu huwezi kimbia,
Waweza ikacha sima, maji huwezi susia,
Hata ngazi ya boma, siasa waitumia,
Siasa ukiitema, jua umeangamia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
6
Kuna siasa ya chama, kimoja nawaambia,
Kila shauri la umma, chama hujiamulia,
Bunge huwa maamuma, muhuri hushikilia,
Jambo lipite kwa Chama, bunge lalishadidia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
7
Zipo za demokrasia, vyama vingi nawambia,
Mfano za Tanzania, na uingereza pia,
Vyama hushindania, magogoni kuingia,
Rais kwa Tanzania, waziri kwa malikia
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
8
Siasa ndani ya vyama, huko hazikuanzia,
Ilianza toka zama, kabla ya hino dunia,
Furkani nimeisoma, sikuiacha biblia,
Malaika na Karima, pia wanaitumia,
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
9
Siasa za huko ahera, kiongozi ni Jalia,
Huongoza msafara, waja wakafuatia,
Mwenye kufanya harara, jeuri akajitia,
Atakuwa ni asira, wa shetani nawambia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
10
Muumba ndio kinara, wa mbinguni na dunia,
Maisha huyachora, na njia hutupangia,
Hupata njema ijara, mwenye kumsujudia,
Hupata kubwa hasara, mwenye kupuuzia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
11
Nani alipiga kura? Munguwe kumchagua,
Mjibu pasi kufura, kweli mpate ijua,
Hapana si masihara, si punde mtagundua,
Tena sifanye papara, siasa kuchambua.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
12
Siasa za kifalme, mfano za Saudia,
Mwana hasa wa kiume, kiti ndio hukalia,
Koo iloshika kome, dola huishikilia,
Mfalme ndio sime, na pia huwa pazia.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
13
Zipo za kidikteta, kama zile za Mobutu,
Wengine panga hufuta, pia wapo wa mtutu,
Umma wote hufyata, mbele ya miungu watu,
Kila mwenye kutukuta, ni mbwa mbele ya chatu.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
14
Dikteta awe katili, mbona mtaumwa sana,
Siombe awe jahili, mtapoteza amana,
Tena akiwa bahili, wananchi hukondeana,
Kiongozi bahaluli, asiaminiwe tena.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
15
Samaki awape nyoka, mkate awape mawe,
Nani kashindwa ondoka, kisa halina mauwe?
Ya msingi wanataka, viongozi waelewe,
Wakichoka kuboboka, watawapopoa mawe.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
16
Dikteta awe rahimu, ndipo mtanufaika,
Rasini awe timamu, na tena mshaurika,
Mtakula keki tamu, mafurushi mtashika,
Tripoli yajilaumu, Gaddafi kudondoka.
Siasa mjue njia, maamuzi kufikia.
17
Nikitazama chupani, sioni kitu jamani,
Wino wangu wa thamani, ya manjano zafarani,
Niko mengi rasini, wino umetufitini,
Mwenye nao sinihini, naomba niuzieni
Mmeshindwa nidhamini, kwa kifupi kwaherini.

Dotto Chamchua Rangimoto (Njano5)
mzalendo.njano5@gmail.com
0715845394/0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania.

BREAKING NEWZ, MAWAZO RUKSA KUAGWA.




Polisi waangukia meno ya mbele Mahakamani...wao na waliowatuma kuzuia Mawazo asiagwe!
Alphonce Mawazo ataagwa kishujaa Jijini Mwanza kama ilivyooangwa na familia na Chadema baada ya Mahakama kuridhika kuwa wanahaki ya Kikatiba kumuaga mpendwa wao. Polisi inajukumu la kulinda amani na utulivu wakati wa shughuli hiyo.

NDESAMBURO ATOA MASHARTI MAGUMU CHADEMA.

































NDESAMBURO ATOA MASHARTI MAGUMU CHADEMA.
Mdhamini mkubwa wa CHADEMA mh. Ndesamburo atoa masharti magumu kwa chadema baada ya Binti yake Lucy Owenya kukosa Ubunge wa viti maalum.

Mpashaji wetu ameieleza Kisima kuwa Ndesamburo alimwita Mbowe Moshi na kumpa masharti makali kuwa kama Binti yake Lucy Owenya hatapata Ubunge atasitisha misaada na kuipeleka kwa kwa chama cha ACT wazalendo kumuongezea nguvu Zitto Kabwe, na kutangaza rasmi Vita na chadema.

Hata hivyo Mbowe aliomba radhi na akamwambia mchakato wa viti maalum haufanywi na mtu mmoja, bali kuna taratibu ndani ya chama na NEC pia. Hata hivyo inaonekana nia ya Mbowe ilikuwa kuwatupia zigo Tume ya Uchaguzi, jambo ambalo sio kweli.

Baada ya mazungumzo yote walihitimisha kwa kukubaliana. Mbowe aliomba radhi na kukubali kuyatekeleza masharti, kwa kuanza kumtoa Lucy Owenya nafasi ya 39 na kumshusha hadi nafasi ya 37 ya orodha ya mpangilio wao wa viti maalum . Nafasi ya 37 inamfanya Lucy kuwa mtu wa Kwanza katika viti maalum vipya watakavopata chadema baada ya kumalizika uchaguzi huu unaoendelea desemba 20. Kama tutakumbuka tume ya Uchaguzi walibakiza viti vitatu kutovigawa ndio hivyo ambavyo wanategemea kimoja wampe Lucy endapo wataongeza asilimia za kura za kupata sifa kupata viti maalum hivyo.

Pamoja na hayo inasemekana sababu iliyo sababisha Lucy Owenya akose nafasi ya kiti maalum ni ukaribu wake na mwanasiasa machachari Zitto Kabwe, hongera yake Lucy Owenya kwa kupewa matumaini na poleni madada wa CHADEMA ambao mlikuwa nafasi ya 37 na 38. Lucy Owenya kachukua nafasi yenu, midhali ni maamuzi ya chama, hamna budi ya kuyakubali na kuongeza juhudi zenu katika ujenzi wa chama.

Kisima Cha Jangwani.

LOWASSA AWAPIGA CHENGA P0LISI.










LOWASSA AWAPIGA CHENGA P0LISI.

Hivi karibuni aliyekuwa mgombea wa UKAWA, Lowassa aliwaambia Polisi Jijini Mwanza kuwa Chadema haihitaji ulinzi wao kufanya matukio yake kuwa salama. Rekodi zote za vurugu huanzishwa na Polisi wenyewe...

Jana alithibitisha hilo mjini Kahama baada ya kuwapiga chenga ya mwili na kwenda hospitali bila escot yao kwake kama Waziri Mkuu mstaafu.

Baadae Polisi wakamfuatilia nyuma nyuma akiwa anarudi.. Msafara wake ukatoka nduki na kuwaacha maboya tena polisi hao.
***
Nipashe lina stori zaidi.

BRAKING NEWZ, EXPLOTION KILS KDF GARISSA















#‎BreakingNews‬: IED explosion kills KDF soldier, wounds six others in ‪#‎Garissa‬ County.

Habari kamili na picha baadae,

WAZIRI MKUU AANZA KAZI KWA MKWARA














WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.

Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, NOVEMBA 23, 2015.

SHEREHE ZA UHURU ZAFUTWA MWAKA HUU.















TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike kwa kufanya kazi. Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu. 

Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.

Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.

Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo, sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Novemba, 2015

KATIBU MKUU KIONGOZI AAGIZA WATUMISHI WA UMMA WAVAE SARE.



























KATIBU MKUU KIONGOZI AAGIZA WATUMISHI WA UMMA WAVAE SARE.


Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue ameagiza watumishi umma kuvaa sare maalum wanapokuwa kazini, lengo kubwa wapate kujulikana kwa urais na wateja wao.

MAGUFULI ABATILISHA HATI ZA UMILIKI WA ARDHI ZISIZO ENDELEZWA
















Taarifa inatolewa kwa umma kwamba, Miliki za viwanja na mashamba zilizoorodheshwa katika jedwali, zimebatilishwa kutokana na ukiukwaji wa kumiliki ardhi.

Inasemekana wale wote ambao wanamiliki viwanja kwa muda mrefu na hawajaviendeleza, kuna mpango wa kunyang'anywa. Taarifa hii inatolewa kwa mujibu wa fungu la 49(1) la sheria ya ardhi sura
 (113)




NDONDO SI CHURURU

NDONDO SI CHURURU.                                  
 1
Ndondondo sio chululu, najua maneno yao,
Waona wamefaulu, ati silingani nao,
Tena waniita mbulu, nisitie guu kwao,
Nakubali si chururu, haba mwanzo wa kibaba.

2
Nasemwa mvaa moja, mi kauka nikuvae,
Kutoka kwangu si haja, tuli nyumbani nikae,
Ati tafanya kiroja, kiasi wanikatae,
Nakubali si chururu, haba mwanzo wa kibaba.
3
Nami nitajikusuru, nitalima na miraba,
Kikubwa sitakufuru, tamuomba mungu baba,
Hata hivyo nashukuru, ninachopata si haba,
Nakubali si chururu, haba mwanzo wa kibaba.
4
Huwezi kupata kenda, bila kuanza moya,
Sijitii mbio kwenda, nachelea vunja taya,
Lolote waweza tenda, kwa paka hupati paya,
Nakubali si chururu, haba mwanzo wa kibaba.
5
Sikitaki cha kuiba, kilijaze tumbo langu,
Silipendi la kahaba, lisonisha hamu yangu,
Maovu hayawi tiba, kutibu kichomi changu,
Nakubali si chururu, haba mwanzo wa kibaba.
6
Ingawa sijakinai, cha mtu sikitamani,
Hata niwe na nishai, sirukii cha jirani,
Nina dhiki sikatai, na mungu yupo jueni,
Nakubali si chururu, haba mwanzo wa kibaba.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5.)
Mzalendo.njano5@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania

MAAFISA 50 WAPIGWA STOP KUSAFIRI



















KAZI INAENDELEA
--------------------------------------
Raisi Magufuli amezuia maafisa 50 waliokuwa wasafiri kwa ajili
ya kwenda kushirika kwenye ziara ya Jumuiya ya Madola.
Badala yake ameruhusu maafisa wanne tu na kuokoa jumla ya
sh milioni 700 ambazo zingetumika kulipia posho za safari na
kugharamia ticket za ndege.
Chanzo:Nipashe

LOHA Patli Kamar Lambe Baa

 





Hii nyimbo inapatikana katika filamu inayoitwa LOHA, moja ya filamu maarufu na nzuri ya kihindi hata sasa. Ilichezwa mwaka 1987.



AGIZO LA RAIS LATEKELEZWA, VITANDA 500

Maagizo aliyotoa rais jana yatekelezwa leo,
Vitanda 500 na magodoro 500 vinashushwa Hospitali ya taifa muhimbili, hii ni baada ya rais kusema fedha zilizotengwa kwaajili ya sherehe jana Dodoma zitumike kwaajili ya kununua vitanda muhimbili.

REJEA HABARI HII.

Wabunge wamechangisha shilingi milioni 250 kutoka bank mbalimbali kwa ajili ya sherehe yao ya jana usiku.
Baada ya muheshimiwa Magufuli kupata habari hizo, akaagiza kwamba party ya leo usiku itumia shiling milioni kumi au kumi na tano tu. Pesa inayobakia ipelekwe Hospitali ya muhimbili ikanunue vitanda ili wagonjwa wasilale chini. Huu ni mwanzo mzuri, im begining to become proud of my president.








SIDHARAU, KAZI NI KAZI.

SIDHARAU, KAZI NI KAZI.
                                   
Uza dagaa mchele, piga na kibakubaku,
Wala hupigi kelele, puyanga huko na huku,
Mkeo apike mle, mwidu sitamani kuku.
Sidharau kazi yako, mie sikufai kitu.

Piga debe kwa matatu, mchana hata usiku,
Kwa mbwembwe uite watu, kwa taxi na tukutuku,
Wana wapate viatu, sisaahu na mabuku,
Sidharau kazi yako, mie sikufai kitu.

Lima shamba bila haya, sisononeke moyoni,
Kwa ngiri hupati paya, msufi hauna buni,
Sitegemee cha mbuya, wala sikitumaini,
Sidharau kazi yako, mie sikufai kitu.

Wizi si kazi jamani, utapeli wafaani?
Si kitamu ulimini, cha kuiba kwa jirani,
Hakistiri maungoni, cha kupora madukani,
Kazi ile ya halali, yenye kufaa jamii.


Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5.)
Mzalendo.njano5@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania

IWEJE KIMBUNGA KILE, KISHINDWE ZUA PAA.

IWEJE KIMBUNGA KILE,
KISHINDWE ZUA PAA.                                                            

1.
Msije dhani natunga, wala sisemi uwongo,
Nimekiona kimbunga, kimetikisa mjengo,
Samani zilijigonga, haukupona mlango,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
2.

Hewa ikawa mchanga, vumbi ndani ya jengo,
Watu wakatangatanga, kama wanasaka fungo,
Si pakazuka kisanga, fupa kapewa mapengo,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
3.

Uhodari wa kuchunga, na kupeta kwa ungo,
Sima imejaa chenga, umethibiti urongo,
Mtoto kapewa mwanga, shetwani ataka pungo,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
4.

Miti ilipoanguka, mwenyewe nikanong’ona
Paa lililotoboka, hivi leo litapona?
Bora lipate dondoka, kwani halifai tena,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
5.

Mwenzenu niliboboka, dua mbaya nikaomba,
Paa lipate dondoka, tuezeke upya nyumba,
Mzigo hautafika, kamba hizi za mgomba,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
6.

Pepo zimezoa nguo, hadi za maungoni,
Juba na mitandio, haikubaki mwilini,
Watu wakaanza mbio, za kujistiri jamani,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
7.

Ni sharia kuchutama, zinapokuvuka nguo,
Juha aweza inama, aende kim-binuo,
Tangu zama ni hekima, kuyastiri maeneo,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
8.

Chui wamekuwa ndama, kenge amekuwa swila,
Mla wali kala sima, aliyemacho kalala,
Shilingi haikuzama, meli ikawa chakula,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
9.

Nyoka kapata miguu, jongoo kapata macho,
Wajaenda lango kuu, moyoni hawana kicho,
Watateta na mkuu, tena pasina kificho,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?
10.

Lile sikio la kufa, si limepata mganga,
Moto umeshika sofa, hando liko na mchanga,
Hino yangu falsafa, kwa hoja nimeijenga,
Iweje kimbunga kile, kishindwe kuzua paa?

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5.)
Mzalendo.njano5@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania

MCHAFUA WATU, HUCHAFUKA.

MCHAFUA WATU, HUCHAFUKA.                                                            
Kojoa ukojoavyo, hautafika mbinguni,
Na ufanye ufanyavyo, tone la mwisho guuni,
Wende mbio utakavyo, baya hurudi nyumbani,
Kila mchafua watu, huishia kuchafuka.

Boboka ubobokavyo, mkono wangu shavuni,
Sitaonekana ovyo, mithili ya majinuni,
Sitashuka upendavyo, labda nipande thamani,
Kila mchafua watu, huishia kuchafuka.

Chafua uchafuavyo, pasi na haya usoni,
Tabaki vile nilivyo, sichafuki asilani,
Dunia ndivyo ilivyo, hayana budi jamani,
Kila mchafua watu, huishia kuchafuka.

We fusa ufusavyo, sikimbii mwangu ndani,
Sitaacha hivyohivyo, nitauchoma ubani,
Harufu ndivyo ilivyo, takuganda maungoni,
Kila mchafua watu, huishia kuchafuka.

We dhani udhaniavyo, sina baya mtimani,
Waelewa ndivyo sivyo, ungauliza nadhani,
Ninakujua ulivyo, hunipi tabu fatani,
Kila mchafua watu, huishia kuchafuka.

Dotto Chamchua Rangimoto (Njano5)
255762845394/255784845394
Mzalendo.njano5@gmail.com


SASA HAMSINI RASI, HAMSINI MAJINUNI.






















SASA HAMSINI RASI, HAMSINI MAJINUNI
                                               
1.
Niko na wino chupani, na ujiti mkononi,
Naandika ya moyoni, yalo nifika jamani,
Sikuwahi kuamini, kuna viumbe majini,
Visasili vya zamani, ndivyo nilivyodhani.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni
2.
Naanzia mwishoni, nilipokaa jamvini,
Fatma bint Subiani, akipandishwa rasini,
Niliketi kitangani, na chano kiko pembeni,
Lewa iko kilingeni, yanapungwa malohani.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
3.
Mloketi upenuni, na wa mbali sogeeni,
Muingie uwanjani, tuyapunge malohani,
Kiti apate amani, imtoke mitihani,
Alisema hadharani, Kachiki bint Ngonyani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
4.
Kachiki bint Ngonyani, aso mjua ni nani,
Wanasiasa nchini, na wauzaji sokoni,
Hufika kwake nyumbani, wapate ndele usoni,
Anaishi Magomeni, pale Kilosa Mjini,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
5.
Mshike vya mikononi, vilaji vya malohani,
Kitezo na zafarani, na udi wa malohani,
Manenane na ubani, na uvumba wa majini,
Shime viwepo chanoni, ni muhimu si utani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
6.
Maji ya zamda chupani, sanamaki ya kusini,
Uzire, giligilani, na vizimba vya barani,
Mafuta ya asumini, na mkongojo wa jini,
Ada za bint Sultani, visikose kitangani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni
7.
Rabi Mola Sultani, Muumba wa mitihani,
Raha, dhiki na huzuni, majaliwa ya Manani,
Ameumba mashetani, kwa siku ya ushetani?
Kaweka mwiba njiani, ili umchome nani?
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
8.
Niwe na mbawa tisini, nipae hata mbinguni,
Na nifike arshini, nitabaki kuwa chini,
Kudura haiwi chini, huwa juu tambueni?
Upatalo duniani, limeandikwa zamani.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
9.
Fatma mwana wa jini, ndio wangu mtihani.
Kwani niko shubuani, sijui nifanye nini,
Habanduki ubavuni, wala hatoki rasini.
Nifanyeje wenzanguni, initoke mitihani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
10.
Nimezama vitabuni, kazi za wanazuoni,
Biblia na furukani, maandishi ya zamani,
Naitafuta yakini, iliyopo vitabuni.
Hukumu yake n’ nini, sijaipata jamani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
10.
Fatma wewe ni nani, na hasa wataka nini?
Vilaji vipo chanoni, sema sasa ya moyoni,
Au nichore baoni, nijue ya ghaibuni?
Wewe ni wa baharini, au wale wa barani?
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
11.
Haya sasa sogeeni, msikie ya moyoni,
Ninayo mengi mtimani, yalo nifika zamani,
Sitochora ubaoni, kusema ya kifuani,
Haya yangu ya nguoni, wa kuyasema jirani?
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
12.
Ninayo mengi mtimani, yalo nifika zamani,
Nilikuwa darasani, mwaka ule wa huzuni,
Nikapigwa kichogoni, kiza nikawa sioni,
Kisunzu tele mwilini, puu nikabwagwa chini.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
13.
Kabla sijabwagwa chini, nilimuuliza jirani,
Aliyenipiga nani, cha mno hasa ni nini?
Nimewakera nini, hata nipigwe kichwani.
Wakanicheka jamani, nikaihisi tafrani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
14.
Dotto uko na nini? Akanishika begani,
Aliyekupiga nani? amekupiga na nini?
Una mawazo gani? Una wazimu kichwani?
Akaiomba amani, nisiizue tafrani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
16.
Nilipoanguka chini, Nikawa niko ndotoni,
Niko mwenyewe njiani, nchi ya ughaibuni,
Nakimbizwa na manyani, wenye mawe mikononi,
Nikasemea moyoni, Lile si Joka jamani?
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
17.
Joka hili joka gani? Mwenye kipembe kichwani,
Ana shanga shingoni, pete tano mkiani,
Mwale wa moto machoni, moshi watoka puani,
Akazichochea kuni, kwa kuungana na nyani,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
18.
Nilisoma vitabuni, habari ya maluuni,
Mwenye kipembe kichwani, ndiye huyo maluuni?
Aliyezua tafrani, duniani na mbinguni,
Ana matobo kichwani, hana jema asilani.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
19.
Mwenye pembe kichwani, alifukuzwa mbinguni,
Akashuka duniani, kama Amiri jeshini,
Watu hawaelewani, kisa huyu punguani,
Nilo soma vitabuni, leo dhahiri machoni,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
20.
Mwenye kipembe kichwani, likaungana na nyani,
Loo! niko hatarini, kutolewa duniani.
Na hawa mahayawani, watia ndimi puani,
Nikamuomba Manani, anitoe hatarini.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
21.
Jasho likanimwaika, na miguu ikachoka,
Manyani wakanifika, Joka likanizunguka,
Hakika nilitishika, mwili ukatetemeka,
Mama nikamkumbuka, na yowe likanitoka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
22.
Mkojo ukanitoka, bila mwenyewe kutaka,
Mwili wote ukachoka, nikahisi kuanguka,
Li Joka likajisuka, mwili akauzunguka,
Mwili ukasisimka, na woga ukanishika,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
23.
Sauti zikasikika, ya mifupa kuvunjika,
Nyani wakaongezeka, sijui walipotoka,
Wakawa wakinicheka, vile ninavyoteseka,
Tena wakirukaruka, duara wakizunguka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
24.
Miguu ilinyooka, ulimi ukanitoka,
Shingo ilivutika, koo likakabika,
Mwili ukatetemeka, baridi ikanishika,
Ningeweza kuanguka, ni joka lilonishika,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
25.
Roho iliangaika, nikahisi yanitoka,
Pumzi ziliathirika, kuruzo lilinitoka,
Mishipa ilipasuka, damu zikachuruzika,
Koo lilinikauka, na kiu ilinishika,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
26.
Mambo yaso kufika, masikio huyachoka,
Vigumu kuaminika, hadi yata’po kufika,
Kweli nimeona Joka, Baada ya kuzimika,
Hata nilipozinduka, kichwani hakunitoka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
27.
Ndotoni nikiteseka, Kwa waja nilizimika,
Nyuso zilifadhaika, huku wakiangaika,
Wapo walonishika, wakisema pepo toka,
Visomo vilifanyika, ili nipate zinduka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
28.
Waliomba kwa Rabuka, ili nipate ponyeka,
Maneno yakanitoka, sauti ikachujika,
Mimi si mwenye kutoka, hapa ndio nimefika,
Fanyeni mnalotaka, katu si mwenye kutoka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
29.
Watu waliongezeka, sauti iliwafika,
Dotto nataabika, joka limenizunguka,
Kumbe hovyo naboboka, na sauti zabadilika,
Macho yalinitoka, na shingo ilipindika,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
30.
Mrembo aloumbika, sijui alipotoka,
Manyani wakatishika, ajabu wakatoweka,
Joka likafokafoka, na ndimi ilimtoka,
Kipembe kikatamka, mambo yasoelezeka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
31.
Hatua akairuka, haraka akanifika,
Vitisho vyote vya joka, Mrembo hakutishika,
Machoni alinishika, nikayafumba haraka,
Macho yalipofumbuka, nikawa nimezinduka.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
32.
Loo amezinduka, mmoja akasikika,
Damu zinamtoka, ulimi umechanika,
Taratibu kapashika, damu zinaponitoka,
Kumbe hapajachimbika, ni kama amechubuka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
33.
Kivivu nikainuka, tayari kwa kuondoka,
Nguo zilivyochafuka, rangi zilibadilika,
Nyumbani nilifika, si kama niloanguka,
Wale walonipeleka, wala hawakusumbuka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
34.
Wala sikupumzika, nyumbani nilipofika,
Ndugu walonizunguka, niliwatoa mashaka,
Jinsi nilivyoanguka, kuwaficha sikutaka,
Yale yaliyo nifika, wala sikuyafutika,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
35.
Wala sikuyafutika, yote yaliyo nifika,
Kisunzu na kuanguka, kiza na kuzimika,
Habari za yule joka, na bint aloumbika,
Wale nyani walozuka, mwisho nilivyozinduka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
36.
Wote walifadhaika, huzuni iliwashika,
Hasa walipokumbuka, Bibi alivyoondoka,
Alianza kudondoka, na kisha akazimika,
Naye aliweweseka, na macho yalimtoka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
37.
Kitu alichotamka, Bibi alipozinduka,
Nilizingirwa na Joka, na nyani walonicheka,
Mwanamke alipozuka, machoni akanishika,
Roho nahisi yatoka, akaaga na kuwatoka,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
38.
Bibi aliyependeka, ndivyo alivyowatoka,
Kifo chake cha mashaka, sasa wakakikumbuka,
Wenzangu hawakutaka, yaleyale kunifika.
Hatimaye wakatoka, nami nikapumzika.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
39.
Jinsi walivyotishika, wala hapakukalika,
Nyumbani wakaondoka, wote wamehamanika
Hofu iliyowashika, mganga wakamsaka,
Wallahi hawakutaka, yale yale kunifika.
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.
40.
Majani ya mkirika, mizizi ya msanaka,
Buni zilizokauka, na mafuta ya mbarika,
Ndivyo vilivyotumika, mwili wangu kuzindika,
Lengo nipate epuka, matatizo kunifika,
Sasa hamsini rasi, hamsini majinuni.

Dotto Chamchua Rangimoto.(Njano5.)
255762845394/255762845394
mzalendo.njano5@gmail.com
Morogoro Tanzania.

KISA CHA MISHI, MAPENZI SI HESABU

KISA CHA MISHI, MAPENZI SI 
HESABU.     
                  
1.
Kwa jina naitwa Mishi, binti mwenye heshima,   
Mwenzenu ni mtumishi, nipo ofisi ya umma,
Kama hiyo haitoshi, mwanamke najituma,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
2.
Nina gari namiliki, mwenyewe sina dereva,
Ninayo nyumba Masaki, nina shamba Usariva,
Kwa fedha sibabaiki, nakula vilivyo iva,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
3.
Nina elimu si haba, UDSM nimesoma,
Shukurani zake baba, pongezi kwa wangu mama,
Kazi sasa yanibeba, umri nao wayoyoma,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
4.
Nimetafuta jamali, mwenzenu nataka mume,
Hata awe suruali, aso kitu kwa kuume,
Kikubwa awe rijali, simtaki gumegume,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
5.
Kila nilipo pakaa, matatizo hunipata
Tarasimu hazikufaa, kunikinga na matata,
Nikaja kata tamaa, huyo mtu sikumpata,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
6.
Penzi kiumbe habithi, mja naomba sikia,
Ninatendwa uhanithi, moyoni ninaumia,
Usije dhani hadithi, tena si tamthilia,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
7.
Sijui nianze mwisho, pale tulipogombana,
Na vile vyake vitisho, yaani vya kuachana,
Si lolote ni michosho, si ya leo si ya jana,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
8.
Vema nianzie mwanzo, pale tulipokutana,
Niwasimulie chanzo, mimi naye kushikana,
Mimi nilikuwa ponzo, alipogongwa kijana,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
9.
Ndipo ikanilazimu, mwili wake kuutibu,
Na ule umaamumu, ukamtoka taratibu,
Nikawa ninajihimu, kutazama matibabu,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
10.
Mgonjwa kawa mpenzi, bila hata kumaizi,
Akaanza kunienzi, taratibu kwa mapozi,
Nami nikawa mpanzi, sikuifanya ajizi,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
11.
Sijui nikawa wapi, sikuona mbalamwezi,
Nuru ilitoka vipi, na jua halichomozi,
Sijui dunia ipi, mapenzi kumbe uchizi,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
12.
Huyu Jamali muhibu, alikuwa yu chuoni,
Anasoma uhasibu, palepale Mlimani,
Bumu likileta tabu, humpiga kampani,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
13.
Sijiu ndio kudeka, au kuchuna jamani,
Mishi kile nakitaka, sina fedha mfukoni,
Ili nipate ridhika, nipatie wangu hani,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
14.
Nikakope kama sina, muhibu wangu apate,
Mwanafunzi kazi hana, niliwaza siku zote,
Kumbe mapenzi hakuna, kiumbe chuma ulete,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
15.
Pendo lake silipati, ubavuni hanitoki,
Pendo lake ni la chati, na kumuacha sitaki,
Nampenda kwa dhati, ila kwake sipendeki,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea..
16.
Kosa hakika si kosa, mbona atasema sana,
Ya zamani na ya sasa, wallahi yatajazana,
Mapenzi yananitesa, utulivu hata sina,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
17.
Huo wivu alonao, kama anipenda sana,
Situmii mitandao, uhuru mwenzenu sina,
Anipangia vikao, niende au hapana,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
18.
Kila siku twazozana, kama mafurusi sina,
Na leo tumegombana, sababu ni ndogo sana,
Akatalii uchina, nauli yenyewe hana,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
19.
Sina karma ya Mwasiti, mahaba ningeyavua,
Kama yangekua kiti, kalio ningeinua,
Nimezama katikati, mapenzi yaniumbua,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
20.
Kumuacha natamani, moyo wangu hautaki,
Hanipendi si utani, ila kwangu haondoki,
Anaruka kama Nyani, ubavuni habanduki,
Penzi halina kanuni, chunga usije kosea.
21.
Sijui niendelee, au hapa niishie,
Sasa twaenda uzee, yako mengi niwambie,
Naomba mtuombee, ndoa yetu itulie,
Shida ukizizoea, njia utajipatia.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
Mzalendo.njano5@gmail.com
784845394/764845394
Morogoro Tanzania

RIZIKI NI MAJALIWA.

RIZIKI NI MAJALIWA                                                                  
1Haku muumba kilema, akamkosesha mwendo,
Huyo ni Mola Karima, mfalme wa vishindo,
Usijifanye yatima, fungua yako mafundo,
Rauka fanya hima, nyumbani haliji windo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
2.
Mwenye kupewa ukwasi, katu hakupendelewa,
Masikini hasi asi, wallahi hakuonewa,
Mitihani ya Qudusi, mola wa majaliwa,
Alichopewa pungusi, chaa hakuruzukiwa.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
3.
Rauka wahi kazini, upate yako ijara,
Changamoto za windoni, na zikufanye imara,
Toa simanzi moyoni, tena sifanye harara,
Bosi avimbe kichwani, tuli sipoteze dira.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
4.
Ukiri mwenzangu kiri, hebu acha kusonona,
Wazoee waajiri, kama wataka kunona,
Shetwani asikughuri, ingawa dhiki waona,
Subiri ndugu subiri, lisilo mwisho hakuna.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
5.
Niseme na waajiri, wenye pembe vichwani,
Wana kifanya kiburi, hawana heri moyoni,
Mbaya hawana habari, shida haina maskani,
Tabu haina tajiri, wala si ya masikini.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
6.
Ewe ndugu mwajiriwa, sema na wako moyo,
Jukumu ulilopewa, litimize pasi choyo,
Ridhika na unachopewa, huno wangu mgogoyo,
Rushwa katu si ngekewa, yataka ushinda moyo.
Riziki nimajaliwa, kuipata si ngekewa.
7.
Wote wategemeana, mwajiri na mwajiriwa,
Kubwa kuheshimiana, mwerevu kanielewa,
Pia mkiaminiana, kazi haitachezewa,
Tara mkifanyiana, lengo halitafikiwa,
Riziki ni majaliwa, kuipata si ngekewa.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5.)
Mzalendo.njano5@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania


TAMKO LA MUFTI JUU YA TUKIO LA KIGAIDI UFARANS













Matukio ya Ufaransa,
Mufti (BAKWATA) atoa tamko.

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh
Kwa niaba ya waislamu wa Tanzania, napenda kutoa rambi rambi na pole kwa watu wa Ufaransa ambao ndani yake wapo waislamu na wasio waislamu, wenye dini na wasio na dini.

Napenda kutoa pole sana kwao kwa tukio la kihalifu na kigaidi lililotokea huko hivi karibuni na kuwaathiri wakazi wa huko Ufaransa na kiukweli kabisa tukio hili pia limetuathiri sote ulimwenguni.
Hapa napenda kusema kwamba tukio lolote la kihalifu dhidi ya raia wasio na hatia popote pale ulimwenguni ni tukio la kihalifu dhidi ya wasio na hatia ulimwenguni kote.
Ulinzi na usalama na zawadi iliyo kubwa mno kutoka kwa Mwenye ezi Mungu kwa wanadamu popote pale walipo. Kwani kwa kuwepo ulinzi na usalama ndio tunaweza kuendesha sughuli zetu za ibada,uchumi na maendeleo mbalimbali katika nchi zetu.

Hivyo basi yeyote yule anaejaribu kuchezea Ulinzi na Usalama wetu huyo anafanya kitendo cha kumfurahisha Shetani na kamwe hafanyi kitendo cha kumfurahisha Mwenye ezi Mungu.
Natambua katika kipindi hiki wapo watakaojaribu kuhalalisha kitendo hiki kwa visingizio mbalimbali ambavyo kwa hakika hakuna njia yeyote ya kuhalalisha vitendo vya namna hii kwani hakuna mafundisho yeyote ya dini yanayohalalisha kuuwawa watu wasio na hatia.
Wajibu wetu katika kipindi hiki ni sote kwa pamoja na kuungana na wenzetu waliopoteza ndugu na jamaa katika tukio lile la kihalifu.

Kama ambavyo tunatoa pole kwa waathirika wa tukio hili huko ufaransa vilevile tunatoa pole kwa waathirika wa matukio ya namna hii popote pale ulimwenguni.
Kwani natambua wapo wanadamu ambao wamo ndani ya mateso na shida mbalimbali katika sehemu mbalimbali ulimwenguni. Sehemu kama vile Syria, Yemen, Afrika ya kati, Myanmar, Palestine, Libya, Mali, Somalia nk.
Na mwisho niwakumbushe waislamu wa Tanzania na watanzania wenzangu kwa ujumla umuhimu wa kuilinda Amani ya nchi yetu na kuendelea kushikamana katika kuilinda kwa nguvu zetu zote Amani hii.
Wabillahi ttawfiiq.
MUFTI WA Tanzania
Sheikh Abu Bakari Zubeir

YU WAPI ASKARI MBEBA GHARAMA ZAKE?

YU WAPI ASKARI MBEBA GHARAMA ZAKE?           
 1
Anunue makombati, kwa pesaze mfukoni,
Vifaru na guruneti, vitoke mwake kwapani,
Yaani hata mabuti, na silaha za vitani,
Mnitajie askari, mbeba gharama zake.
2
Pesa zake za manati, anunue darubini,
Familia si thabiti, pesa ziende vitani,
Nimeshikwa kibuhuti, dunia iko rasini,
Mnitajie askari, mbeba gharama zake.
3
Watoto hawana njuti, wako peku miguuni,
Hawana hata mashati, wala ada ya shuleni,
Tena pana hatihati, kukosa pango jueni,
Mnitajie askari, mbeba gharama zake.
4
Hazipikwi kalimati, wala hando si utani,
Wana chai hawapati, paka kalala jikoni,
Hawachezi na ukuti, chango zalia tumboni,
Mnitajie askari, mbeba gharama zake.
5
Sinunue utondoti, na vivalo vya mwandani,
Kitanda kikose shiti, baba uende vitani,
Si bure uko na shoti, hazijatimu kichwani,
Mnitajie askari, mbeba gharama zake.
6
Waume na mabanati, walimtoa mkoloni,
Walishikana mashati, kubeba walo vitani,
Nyerere kapewa hati, akaruka Marekani,
Mnitajie askari, mbeba gharama zake.
7
Kuna kufuja wakati, kubeba vita begani,
Nadhani hawanipati, subuhi sio jioni,
Sijakunywa spiriti, sina ulevi kichwani,
Nimeijaza sleti, siko na wino chupani.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5.)
mzalendo.njano5@gmail.com
0762845394/0784845394
Morogoro Tanzania.


NILIDHANI KARANGA, KUMBE MAVI YA MBUZI.





SI KARANGA, MAVI YA MBUZI.
1.
Nilidhani ni karanga, kumbe ni mavi ya mbuzi,
Sikudhani ni pakanga, katika wangu mchuzi,
Kuamini mtu janga, jiandae na mauzi.
Kuna mambo ya kuchunga, wakati wa maamuzi.
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
2.
Nilidhani ni maziwa, kumbe ni tui la nazi,
Ati nimependelewa, na mola wangu Azizi,
Kumbe janga nimepewa, wallahi si kumaizi,
Yale niliyotendewa, mlipaji ni mwenyezi.
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
3.
Nilidhani ni malaika, kumbe adui shetani,
Mimi nilimchunuka, tena nilimuamini,
Kumbe vile anicheka, aniingize mjini,
Akapanga kuchomoka, na sanduku la thamani.
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
4.
Nilidhani muumini, alo na sifa stahiki,
Kumbe najenga imani, kwa kiumbe mnafiki,
Akafanya ushetani, kanirushia mkuki,
Namshukuru Manani, yu mtupu mnafiki,
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
5.
Nilidhani ni kitanda, kumbe tusi la maiti,
Kule kote kunikanda, ni mbinu zake afriti,
Ili apate niponda, aibe japo katiti,
Mja alivyonitenda, nilitamani mauti,
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
6.
Aheri shetani jini, kuliko shetani mtu,
Mbago hata subiani, mtumaji hawi chatu,
Hata ndugu wa ndani, kumwamini sithubutu,
Aweza kuwa shetwani, anipige na mtutu.
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
7.
Unapoweka imani, uweke na tahadhari,
Silaha iwe bindoni, si msaahu Qahari
Ujue wafanya nini, inapotokea shari,
Kilio chafaa nini, mtenda hana habari,
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
8.
Yupo fanani bubusa, katika sanaa zake?
Yaani aso yagusa, mambo ya jamii yake?
Au ashindwe papasa, sakafu ya moyo wake?
Kama yupo ni tutusa, kina shida kichwa chake,
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
9.
Niliuchonga ujiti, nichore yalo nisibu,
Nikafuata shuruti, pamoja na taratibu,
Wino wa chani kiwiti, ukakinakshi kitabu,
Mwisho ikawa kunuti, nipate chuma thawabu,
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.
10.
Sijui niweke koma, ama niweke mkato,
Wenye kutendwa hukoma, ama hukwepa kong'oto,
Sitarudia pogoma, kama mwendo wa kitoto,
Kuwa boya nimekoma, sikiza msaka sato.
Usimwamini yeyote, amini kivuli chako.


Dotto Rangimoto Chamchua.(Njano5)
mzalendo.njano5@gmail.com
0762845394/0784845394 Morogoro

KUNA MANENO YENYE MENO.

KUNA MANENO YENYE MENO.
1.
Neno limekuwa neno, kiziwi kalisikia,
Neno liwe la mfano, tupate kujifunzia,
Neno lisiwe ndoano, kooni likanasia,
Kuna neno na maneno, kuna neno lenye meno,
2.
Lipo neno la uchungu, kiasi bubu aseme,
Mja apigwe kirungu, achapwe hata umeme,
Tayatoa kwa uvungu, na machungu ayateme,
Kuna neno na maneno, kuna neno lenye meno.
3.
Lipo neno la furaha, hata yatima acheke,
Neno jema ni tufaha, kiasi na lipendeke,
Kinyume chake karaha, wanangwa na mpulike,
Kuna neno na meneno, kuna neno lenye meno.
4.
Kuna neno la asili, kwa hilo tumeumbiwa,
Hilo neno ni Jalali, akisema kuwa huwa,
Neno hili ndio kweli, werevu wanatambuwa,
Kuna neno na maneno, kuna neno lenye meno.
5.
Kuna maneno makali, kuliko hata jambia,
Yanawaua makuli, watumwa na malikia,
Hayachagui jahili, na rahimu humshukia,
Kuna neno na maneno, kuna neno lenye meno.
6.
Kuna maneno matamu, asali iwe pembeni,
Tena hayaishi hamu, tayapenda ulimini,
Kuyakosa talaumu, ukose raha moyoni,
Kuna neno na maneno, kuna neno lenye meno.
7.
Kuna maneno hutibu, magonjwa yaso dawa,
Yanasemwa taratibu, maradhi yapate powa,
Humtuliza mahabubu, maneno akiambiwa,
Kuna neno na maneno, kuna neno lenye meno.

Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5.)
mzalendo.njano@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania.


MAONI YA KIGWANGALA JUU YA HOTUBA YA RAIS

MAONI YA KIGWANGALA JUU YA HOTUBA YA RAIS



Huu ni ‪#‎WakatiWaKazi‬ , hotuba ya Rais ya jana imedhihirisha hilo. Kilichonifurahisha jana mimi ni ukweli kwamba kama Taifa tumepata Rais ambaye ataweza kutukimbiza kuelekea kuyafikia matamanio na matarajio yetu. Hotuba ya Rais inadhihirisha kuwa huu kwa hakika ni #WakatiWaKazi.
Sisi sote ni lazima tuamke tujue kuwa ‪#‎TunaKazi‬ ya kufanya mbele yetu, na tuifanye. Tumepata mtu wa kutusukuma kufanya kazi, basi tufanye kazi, tusimuangushe. Na sisi wabunge tumuunge mkono, 'tusimshike' mkono, tumsaidie afanye kazi. Maana kwa hakika ‪#‎MabadilikoYaKweli‬ yamefika. Tuyapokee!

Kuna sheria 21, kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Ndg. Kinana, zinazokwamisha wananchi ama zinazowakandamiza, ama zinachelewesha harakati za kuleta maendeleo, zinapaswa kufutwa ama kufanyiwa marekebisho kwa haraka, basi ziletwe Bungeni zirekebishwe kwa haraka, nchi ianze kukimbia sasa.

Tuna changamoto mbalimbali zinazosababishwa na muundo wa serikali, mahusiano na muingiliano wa wizara moja na nyingine, taasisi moja na nyingine, haya nayo yanapaswa kushughulikiwa kabla Rais wetu hajafika mbali. Namna ya kuratibu uwekezaji - kuondoa mindset potofu kwamba wawekezaji ni lazima wawe watu wa kutoka nje tu, kuwa na taasisi ya EPZA, TIC, Wizara ya uwekezaji na uwezeshaji, viwanda na biashara, kilimo na mifugo (ukizingatia uwekezaji mkubwa tunaohitaji kwa sasa ni unaohusiana na sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwagusa wananchi walio wengi kwa haraka) yote haya yanachanganya na kuifanya process ya uwekezaji nchini mwetu iwe ndefu na complex kuliko kuwa ya haraka na rahisi n.k.

Tuna mkanganyiko mkubwa sana kwenye mahusiano kiutendaji kati ya wizara ya TAMISEMI na wizara za kisekta...

PROF KITILA MKUMBO ATOA UFAFANUZI JUU YA KILICHOTOKEA JANA BUNGENI.

PROF KITILA MKUMBO ATOA UFAFANUZI JUU YA KILICHOTOKEA JANA BUNGENI.


Ieleweke tu kuwa alichokifanya Zitto bungeni jana ni msimamo wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Tunaamini kwamba matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa kwa njia za kisheria na kisiasa. Na tusingeweza kushiriki kutekeleza mpango ambao hatukushiriki kuupanga. Sisi pia tunamtambua DK Magufuli kama mshindi halali wa kiti cha urais na Mgombea wetu alikubali matokeo. Sisi sio mazuzu au nyumbu hata tujiegeshe katika mipango tusioijua. We're a political party with a clear set of principles, values and mode of operations.

Tutaendelea kushirikiana pale ambapo hoja zinashabihiana. Lakini pia hatutaogopa kutofautiana pale ambapo hatuamini katika msingi wa hoja au njia za utekelezaji. Katika hili la Zanzibar tunafanana katika msingi wa hoja lakini tunatofautiana katika mkakati wa utekelezaji wa hoja husika. Na hii haina ubaya wowote, ni afya kabisa kwa demokrasia yetu. Kuwaita watu mnaotofautiana mitazamo kwamba ni wasaliti ni kielelezo kamili cha ujinga wa kisiasa. Na Sisi tumedhamiria kupambana na ujinga wa kisiasa popote ulipo.

KAMA PARIS INAULIWA NA MIZIMU YA SYRIA, WACHA IFE, SITALIA!

KAMA PARIS INAULIWA NA MIZIMU YA SYRIA, WACHA IFE, SITALIA!
Hakika nimeumia sana kwa yaliyotokea Paris, watu waso na hatia wakifa bure bila sababu yoyote au kwa makosa yalo fanywa na wanasiasa.
Hata hivyo, ni dhahiri kuwa haya yote ni matukio ya kigaidi, ni mwendelezo tu ya matukio mengi ya kigaidi yanayo endelea kutokea duniani.                     


Pamoja na kulaani hili la Paris na mengi yenye kufanana na hili, naomba tujiulize hivi zile silaha za maangamizi ambazo Saddam Hussen alituhumiwa nazo hata akavimiwa kijeshi NATO ziko wapi? Iweje hadi leo pasionekane dalili yoyote ya nchi ya Iraq kumiliki silaha zile?
Dhahiri kuwa NATO walizusha hili la silaha za maangamizi ili wapate uhalali wa kuivamia Iraq, baada ya vita ile hadi leo hii Iraq hakuna salama ukilinganisha na enzi za Saddam.
Wairaq 165,000 ambao si wapiganaji walikufa wakati vita, wengi wao wanawake na watoto, na baada ya vita na hata sasa wairaq wasiopungua milioni moja wamekufa kutokana na kutotengamaa kwa hali ya usalama tangu uangushwe utawala wa Saddam.
Ukiniambia nani aliyewaua wairaq hawa wasio kuwa na hatia, jibu langu ni NATO na washirika wake, sababu wairaq hawa hawakuuliwa na silaha za maangamizi za Saddam bali waliuliwa na silaha za NATO na washirika wake, pia kwakuwa Saddam hakukutwa na silaha za maangamizi, kwa vyovyote vile ule uvamizi ulosababisha vifo hivi hakuwa halali na ulishinikizwa zaidi na mgongano wa kisiasa kati Baghadad na Washington.
Walioshiriki kufanya mauaji Iraq, dunia haioni kama walikosea, na kwa hivyo hakuna shinikizo lolote la kutaka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria hata haki ya waliopoteza maisha ipatikane. Linaloonekana ni kupongezwa kwa watu hao.
Kwa vyovyote vile waliopoteza wapendwa wao wanatafuta haki za ndugu zao kwa namna nyingine, na ninaweza kusema Paris, London, Washington, nk imevamiwa na mizimu(ghost) ya watu walikufa bila hatia katika ardhi ya Iraq, nami nasema kama ni mizimu ya wafu wa kivita, wacha iwatafune wao na vizazi vyao!
Baada ya kuanguka utawala Saddam, ndipo yalipo zuka makundi ya kigaidi kama vile ISLAMIC STATE, makundi ambayo yasingezuka kama kungekuwa na usalama nchini Iraq, na kwa vyovyote vile yalianzishwa ili kulipiza kisasi kwa kile kilichotokea Iraq au makundi haya yana ajenda yao ya siri sema wanajipatia uhalali kwa watu waliopoteza wapendwa wao kwa jina la "kisasi dhidi ya madhalimu wa kimagharibi."
Rais Bush hakupelekwa ICC kwa kile alichokifanya Iraq, sababu Marekani si mwanachama ICC, lakini ajabu Marekani hiyo inaishinikiza mahakama hiyo kuwashughulika bila ajizi viongozi wa Afrika kwa uhalifu wa kivita. Hapo ndipo inapo ibuka shaka. Uovu wa NATO dhidi ya binadamu unaitwa vita dhidi ya ugaidi, na wale wanaolipiza kisasi kwa uovu wa NATO wanaitwa magaidi.
Kuku na yai kipi kilianza? Uovu magharibi(NATO) dhidi ya ubinadamu na ugaidi, si swali la kuku na yai hata tusijue kipi kilianza. NATO ndio iliyoanza kufanya dhuluma kwa binaadamu kwa tamaa za malighafi, ndipo ukafuata ugaidi ambao lengo lake ni kupigania haki iliyoporwa kutokana na uovu wa NATO.
Mathalani, Ulaya ilivamia Afrika na kujigawia kama mali yao, watawala wa jadi waliopinga hili walionekana magaidi kama magaidi wa sasa, chini ya sheria zao na mahakama zao walinyongwa. Alichofanyiwa Saddam Hussen akina tafauti na alichofanyiwa Kinjetile Ngwale.
Kinachotokea sasa duniani ni ukoloni uliovaa joho jipya, ni mwendelezo wa ULAYA chini ya NATO kuendelea kutaka kupora malighafi katika nchi za Afrika na za kiarabu, ni mwendelezo wa kutafuta masoko ya silaha zao kwa lazima kwa kuzusha vita au kuvuruga utulivu na usalama. Vurugu zote za ULAYA zinafanyika mbali na Ulaya kwaajili ya usalama wa watu wao, sasa wanastuka watu 153 kufa wakati hadi sasa wairaq waso pungua milioni moja wamekufa sababu ya UVAMIZI WA NATO.
Mkwawa aliyedhulumiwa, kama huko aliko anasikia kilichotokea Paris, atahuzunika kidogo sababu walokufa si ng'ombe, lakini kwa vyovyote vile atasema "afadhali na waendelee kuuliwa huenda watajua machungu ya kuondokewa na wapendwa wao hata waache kuzusha vita katika mataifa ya wenzao"
Kama ukiketi na kujiuliza, utagundua asilimia kubwa ya kile kinachoitwa ugaidi kimetokana na dhuluma, dhuluma ambayo haina njia ya kuidai mahakamani. Kwa kukosekana hilo, mdhulumiwa hubaki na fundo rohoni, fundo ambalo humlazimisha kufanya lolote ili mradi tu yule aliyemdhulumu alipe na ajue ni kwa kiwango gani ameumia. Washirika wa NATO wanajua nini walikifanya au wanaendelea kukifanya mashariki, kwa kugundua hilo ndio maana kimenuka Paris, lakini Obama, Cameron na Angela Mack wametaharuki uku wakijipanga kwa lolote ambalo laweza tokea katika nchi zao.
Kama ukiketi na ukichunguza, utagundua kila sehemu ambayo ina Civil war kwa namna moja ama nyingine kuna mkono wa nchi za magharibi.
SYRIA, UWANJA WA VITA KATI YA NATO NA URUS.
Huyo mtoto aliyeliyesukumwa maji katika fukwe amekufa maji baada ya kukimbia vita ya Syria kwa njia ya bahari, na huyo mtoto mwingine ni mhanga toka katika uwanja wa mapambano. Watu wengi wamekufa katika uwanja wa kivita na wengi wamekufa maji katika bahari meditarania.
Kinachotokea Syria sasa ni vita ya WAKUBWA WA DUNIA wakigombea rasilima za Syria, Vita Syria ni vita kati NATO(Ufaransa na USA) kwa upande mmoja na URUSI kwa upande mwingine chini ya mwavuli wa civil war inayoendelea sasa Syria.
NATO inawafadhili waasi dhidi ya serikali.
URUSI inaifadhili serikali ya Assad.
Makundi yote haya, NATO na Urusi wanachofikiria mafuta ya tu! Kushindwa kwa waasi ndio kushindwa kwa NATO na kushindwa kwa Assad ndio kushindwa kwa Urusi, vita itaisha endapo NATO na Urusi wakiamua iishe! Makundi yote haya mawili yanataka ipatikane serikali thabiti ya Syria ambayo wataweza kuiendesha watakavyo, na kila kundi halikubali kushindwa hadi pale hiyo serikali itakapo patukana!
Ufaransa na Marekani wanajua wanachokifanya Syria kimesababisha vifo vya watu wasiopungua mil 1, na mimi na wewe pia tunajua, alafu watu 153 waliokufa Ufaransa wasabaishe nami nilie?? nina wazimu? hao 153 waliokufa nitahuzunika sababu si ng'ombe lakini siwezi kuwalilia na kuomboleza ikiwa wao wamesabisha mamilioni ya watu kufa katika maeneo tafauti duniani, heri nao waonje machungu huenda watajifunza utu na sio utu wa bandia wanao tuonesha.
Wengi tumeshangaa Facebook kuanzisha utaratibu wa kuweka kivuli cha bendera ya Ufaransa juu ya profile picha kama njia ya kuoneaha kuguswa na msiba wa Paris, lakini hakufanya hivyo siku mbili kabla ya Paris pale lilipofanyika shambulio la kigaidi Beiruti, ukiuliza kwanini? Hawakufanya hivyo lilipotokea Wastegate na Garrisa? Washatoa jibu la kisiasa, lakini ukweli utabaki kuwa hayo mengine hakukufanyika Ulaya.
Kwanini mshituko wa Magharibi juu ya Paris ni mkubwa zaidi ukilinganisha wa China au Urusi? jibu ni jepesi, Dola ovu zimeshuhudia mwovu mwenzao akishughulikiwa kiasi na wao wajipange sababu uovu wao ni mkubwa kuliko hata wa Paris.
Pamoja na kwamba ushiriki wa Ufaransa katika vita ya Iraq haukuwa na madhara kwa wairaq, lakini hakuondoi ukweli kuwa Ufaransa ilishiriki Afghanstan, na sasa inashiriki katika vita vya Syria, na haiondoi ukweli kuwa huwezi kuitenganisha na NATO na Ufaransa.
Poleni wairaq na ulimwengu wa kiarabu kwa kile kilichotokea Iraq na Syria, poleni wafaransa kwa yalotokea Paris, lakini pia naomba mjue vita ilo sababishwa na uvamizi wa NATO Iraq bado haijaisha, vita imenzia kupiganwa Iraq lakini imekwisha sambaa, sasa imefika Paris, poleni wahanga, vita haina macho.
NINI KIFANYIKE
MOSI.
NATO na dunia chini ya UN iombe radhi kwa kilichotokea Iraq naSyria, lakini isiishie kuomba radhi tu lakini pia isijaribu tena kufanya uovu kama ule.
PILI.
NATO na dunia isidhani demokrasia ndio mwarobaini wa matatizo ya watu, hususani waafrika na waraabu. Zipo nchi nyingi za kidemokrasia lakini zina matatizo mengi kuliko hata Libya ya Ghadafi. Watu waachwe waishi kwa utaratibu wao waliouzoea, kabda kwa hiyari wao waamue kubadilika.
TATU.
Wasililazimshe kufanya biashara na nchi ambayo haitaki kufanya biashara nao juu ya malighafi fulani. Sababu hadi sasa imeshakuwa dhahiri, kilicho mgharimu Ghadaf na Saddam ni utajiri wa mafuta katika nchi zao.
Kinyume na hivyo, tutaendelea kushuhudia matukio ya kigaidi katika nchi za NATO na mimi binafsi siwezi kuwa na huruma zaidi juu mamia ya watu dhidi ya maelfu ya watu watakao kufa kwa chokochoko za NATO.
Njano5
0784845394

MUUNGANO WETU NA NENO

MUUNGANO WETU NA NENO                                        

1
Neno limeota meno, naiona tafarani,
Siyaoni mapatano, sote vipembe kichwani,
Mwana ashikwe mkono, asipotee njiani,
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.

2
Hakika nimekubali, heshima kwa muungano,
Usitafute kibali, hubiri utengamano,
Tuwashinde majahili, wanotaka utengano,
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.
3
Hekima zao wahenga, zimenikumbusha mbali,
Nimezikumbuka ngenga, za wenzetu majahili,
Wanawaza kujitenga, sasa wamekuwa nduli,
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.
4
Niambie yafaani, maneno ya utengano,
Liwapi yenye thamani, nataka yako maono,
Zanzibar ya Sultani, au wetu Muungano?
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.
5
Zanzibar si thamani, kuuzidi muungano,
Tanganyika izikeni, hatutaki utengano,
Mipaka ya wakoloni, isilete mapambano,
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno,
6
Tanganyika ni Berlini, ni zao la wakoloni,
Zenj mno ithamini, ni fahari ya Sultani,
Tanzania ya Amani, na Nyerere tambueni,
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.
7
Tanzania imefuta, mipaka ya wakoloni,
Pomoya imetuleta, wa bara na visiwani,
Waasisi mwawateta, mna wazimu rasini?
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.
8
Kila nikiyatazama, naona yako na meno,
Na kinywa mmehasama, ndimi kama msumeno,
Chombo chaenda mrama, chungeni yenu maneno,
Halikidhi mahitaji, neno likiota meno.

Dotto Rangimoto Chamchua.(Njano5)
255762845394/255784845394
mzalendo.njano5@gmail.com
Morogoro Tanzania

SIONE UKADHANI.

SIONE UKADHANI.
1.
Sione nimenyamaza, mwenzio sina furaha,
Mambo ulo yatangaza, mie yanipa karaha,
Allah aniongoza, ulidhani nitahaha,
Waja ndio walewale, hakika hayana budi.
2.
Sione nimetulia, moyoni nahangaika,
Mwenzio nafikiria, namna ya kuongoka,
Ubaya wanifanyia, inshallah tastirika,
Waja ndio walewale, hakika hayana budi.
3.
Sione natabasamu, moyoni naungulika,
Nikiwaza sina hamu, mambo yalivyo pinduka,
Mie nimepigwa bomu, najuta kumchunuka,
Waja ndio walewale, hakika hayana budi.
4.
Sione nimeduwaa, ujue ninayajenga,
Hata niipate taa, lipendeze langu anga,
Wajashikwa na butwaa, zipotee zako ngenga,
Waja ndio walewale, hakika hayana budi.
5.
Sione sijakujibu, sidhani sijalipata,
Umetumwa si ajabu, fikisha umenikuta,
Sema halinipi tabu, si joto likafukuta,
Waja ndio walewale, hakika hayana budi.
6.
Sione abwata juu, yupo alo mpandisha,
Hata kwa yake miguu, na ngazi ya kuegesha,
Mgude sio chuguu, kobe hawezi pandisha,
Waja ndio walewale, hakika hayana budi. 


Dotto Rangimoto Chamchua.(Njano5)
255762845394/255784845394
mzalendo.njano5@gmail.com
Morogoro Tanzania

WAAFRIKA TUNA MAMBO.

WAAFRIKA TUNA MAMBO.                                            
1.
Mwajua mimi sijambo, namshukuru manani,
Nimeamka kitambo, shafika kibaruani,
Ila kuna kubwa jambo, kuuliza natamani,
Hivi nyie hamjambo? Mliopo kisimani.
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
2.
Mambo yakiwa si mambo, siweke fundo moyoni,
Kubwa sicheke utumbo, kwa maini ya jirani,
Sitaki ule makombo, kwa hamu ya biriani,
Bure taitwa mtambo, mwenye wazimu rasini.
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
3.
Kuna mambo ya mkumbo, kuyafuata acheni,
Mambo mengine urimbo, mchunge siwanaseni,
Kijana kimbie ng'ambo, nchini abaki nani?
Mwisho apigwe taimbo, kwa bata za ghaibuni.
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
4.
Memkumbuka Setembo, babu yangu wa moyoni,
Aliniusia mambo, kuwaambia natamani,
Rijali haumwi tumbo, wala chango kinenani,
Hakika hafanyi tambo, bila vitendo jueni,
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
5.
Nawasema wa kiambo, hata wale wa mjini.
Mlioamkia tembo, mloiota ndotoni,
Hamkuogeshwa jimbo, wakati wa utotoni,
Sawa mfanye utumbo, subuhi mko hewani,
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
6.
Twasisitiza kimombo, kiswahili taabani,
Vizuri kuiga mambo, si kila kitu jamani,
Sawa kuacha kiyombo, kwa suti za Marekani,
Kukiabudu kimombo, ni wazimu jueni.
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
7.
Kanisani kuna mambo, pia na msikitini,
Tuna itukana gombo, nalia utamaduni,
Miungu kutoka ng'ambo, Ulaya na Arabuni,
Imetupiga kikumbo, jadi haina thamani,
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani,
8.
Tufani yapiga sambo, istizai yafaani,
Mjue twaenda kombo, naomba zindukeni,
Sote tumelewa tembo, kutoka ughaibuni,
Sasa ni wana wa kambo, baba wa kijerumani
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
9.
Nimesema kimafumbo, hilo kwanza lijueni,
Maneno haya si shombo, ukutani andikeni,
Msiyafiche kwa rambo, hadharani yawekeni,
Jeuri ataka fimbo, awekwe sawa jamani,
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.
10.
Nimeliza la mgambo, lengo mtoke shimoni,
Ninawaita kwa wimbo, wahafidhina njooni,
Mwanagenzi nina mambo, majagina nifunzeni,
Naomba nifunge gombo, nilosema yashikeni,
Waafrika tuna mambo, nawambia si utani.


Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5.)
Mzalendo.njano5@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania.

MWANANGU SITAKABARI

MWANANGU SITAKABARI                                      
                           
1.
Mwanangu ewe mwanangu, leo nataka kulonga        
Kila jambo lina Mungu, heri na shari hupanga,
Tamu ligeuke chungu, asali iwe pakanga,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
2.
Mwanangu sicheke ufa, kumbuka kuna Jalia,
Siringe kutaka sifa, kiburi ukajitia
Aliye na afya hufa, mgonjwa akabakia,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
3.
Mwanangu hebu elewa, nakuomba zingatia,
Ugonjwa ni majaliwa, mauti ni yetu njia,
Hupona mkusudiwa,hufa mshika jambia,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
4.
Mwanangu naomba shika,nisemayo sio siri,
Haya yamethibitika, kitambo tena dahari,
Mbichi unanyauka, mkavu una nawiri,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari
5.
Mwanangu sifanye ngenga, usitambie ukwasi,
Mambo ukiyabananga, tamkufuru Qudusi,
Mbio hushinda kinyonga, aachwe mbali farasi,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
6.
Mwanangu usiwe chizi, cheo huwezi miliki,
Nataka ujue wazi, hakina hatimiliki,
Chifu awe mjakazi, mtumwa awe maliki,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
7.
Mwanangu yana Karima, kupanda hata kushuka,
Uwende mbele na nyuma, ufanye unavyotaka,
Mla chunga hula nyama, mla nazi hula daka,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
8.
Mwanangu sicheke mamba, nawe mto hujavuka,
Kwa kiburi ungatamba,hupindui la Rabuka,
Hukosa aliyeomba, hupata asiyetaka,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
9.
Mwanangu sifanye inda, aliyepewa kapewa,
Ujue heri ya shinda, kiumbe ulojaliwa,
Ukijua vya kutenda, sisaahu kutendewa,
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.
10.
Mwanangu niendelee, ama kikomo nitie,
Nilosema sichezee, wallahi sipuuzie,
Kitaka uogelee, wasia uzingatie.
Dunia hino dunia, mwanangu sitakabari.


Dotto Chamchua Rangimoto.(Njano5)
784845394/762845394
Mzalendo.njano5@gmail.com
Morogoro Tanzania.

SINA HIYARI,SIKO MWENYEWE.

SINA HIYARI,SIKO MWENYEWE.
1
Swadakta kaka Mwimbe,kongole rafiki yangu,
Kwanza karibu mkembe,mlenda na nyanya chungu,
Sharubati ya maembe,yakungoja ndugu yangu.
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
2
Hiyo heshima ya kwetu,ndugu nilokupatia,
Chakula hicho ni utu,na mahaba asilia,
Kukupa nimethubutu,ujue menivutia,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
3
Upupu uloniweka,leo nautia kucha,
Mama aliponitoka, naye baba kuniacha,
Ndipo mengi yakazuka, yasolitosha pakacha,
Natunga yalo nisibu, mengine nabahatisha.
4
Mambo yakawa magumu,hakuna mfano wake,
Kila nifanyalo sumu,niso jua ponyo lake,
Nikaomba kwa Karimu,anihafu mja wake,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
5
Ukaja umaamumu,niso jua chanzo chake,
Vidonge na talasimu,nikapewa usitoke,
Hivyo ikanilazimu,masomo nipumzike,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
6
Kichwa cha chezo chauma,wallahi kinatatiza,
Nikaanza kulalama,na fahamu kupoteza,
MoroSeko nilisoma,kwa tabu nilimaliza,
Natunga yalo nisibu,mengine na bahatisha.
7
Haya yote si urongo,ni kweli yajulikana,
Pale shule ya Mazengo,vitimbi vikaja tena,
Nikatumbukia nyongo,kusoma sitaki tena,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
8
Sijui mauzauza,ama uwendaazimu,
Mrembo ajitokeza,asema shika kalamu,
Tena akasisitiza,asemayo ni muhimu,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
9
Peke yangu namuona,akizileta habari,
Nikaziandika sana,bila kuhisi hatari,
Kusoma alicho nena,kumbe ule ushairi,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
10
Sasa hamsini rasi,hamsini majinuni,
Ni kisa kichoakisi,yalotokea zamani,
Namshukuru Qudusi,bado niko duniani,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
11
Mimi sio mshairi,leo nataka mjue,
Napelekwa ka tairi,natamani nijiue,
Kufanya yaso hiyari,yataka moyo mjue,
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.
12
Swali ulio uliza,nahisi nimelijibu,
Kama sijatosheleza,sema usione tabu,
Dunia yaeleleza, kucheka usithubutu.
Natunga yalo nisibu,mengine nabahatisha.


Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
mzalendo.njano5@gmail.com
0784845394/0762845394
Morogoro Tanzania.