Ieleweke tu kuwa alichokifanya Zitto bungeni jana ni msimamo wa Chama chetu cha ACT Wazalendo. Tunaamini kwamba matatizo ya Zanzibar yatatatuliwa kwa njia za kisheria na kisiasa. Na tusingeweza kushiriki kutekeleza mpango ambao hatukushiriki kuupanga. Sisi pia tunamtambua DK Magufuli kama mshindi halali wa kiti cha urais na Mgombea wetu alikubali matokeo. Sisi sio mazuzu au nyumbu hata tujiegeshe katika mipango tusioijua. We're a political party with a clear set of principles, values and mode of operations.
Tutaendelea kushirikiana pale ambapo hoja zinashabihiana. Lakini pia
hatutaogopa kutofautiana pale ambapo hatuamini katika msingi wa hoja au
njia za utekelezaji. Katika hili la Zanzibar tunafanana katika msingi wa
hoja lakini tunatofautiana katika mkakati wa utekelezaji wa hoja
husika. Na hii haina ubaya wowote, ni afya kabisa kwa demokrasia yetu.
Kuwaita watu mnaotofautiana mitazamo kwamba ni wasaliti ni kielelezo
kamili cha ujinga wa kisiasa. Na Sisi tumedhamiria kupambana na ujinga
wa kisiasa popote ulipo.