RAIS AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU TRA
Taarifa iliyotolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano - Ikulu imesema kuwa alasiri ya leo, Rais Dk.
John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato nchini (TRA), Rished Bade.
Rais amemteua Kamishna Phillip
Mpango kukaimu nafasi hiyo; na amemtaka Rished Bade kumpa ushirikiano
Mpango hasa katika kutafuta ukweli kuhusu makontena 349 yenye thamani ya
shilingi bilioni 80/= yaliyotoweka bandarini pasipo TRA kuwa na
kumbukumbu zozote za makontena hayo.