MCHEZO WA NEY NA WEMA SEPETU WAJULIKANA.





Hayawahi, hatimaye yamekuwa, msanii mtukutu na mshari Ndugu ney wa Mitego ameachia video yake iliyo zua gumzo kubwa...

Posted by Kisima cha Jangwani on Saturday, February 27, 2016

OLDUVAI GEORGE IKO TANZANIA AU KENYA?





MOMBASA NI ZANZIBAR, NA ZANZIBAR NI TANZANA. HUU NI UKWELI.Siku nyingi nimesikia kuwa wakenya wakisema mlima...

Posted by Kisima cha Jangwani on Saturday, February 27, 2016

AMIRI JESHI, IAMBIE CCM ISILAZIMISHE CUF IFUATE NJIA YA ASP.









AMIRI JESHI, IAMBIE CCM ISILAZIMISHE CUF IFUATE NJIA YA ASP.Salamu.Mie si mchambuzi wa mfano katika mambo ya kisiasa...

Posted by Kisima cha Jangwani on Sunday, February 21, 2016

SITUMII MKOROGO, WEUPE WANGU SABABU YA MAJI.




















SITUMII MKOROGO, WEUPE WANGU SABABU YA MAJI.

Ray ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV na kusema kwamba hua anakwenda salon mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.
Naye Mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba Mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.

Katika kipengele cha ''Cheche'' ambacho majirani hupewa nafasi ya kumzungumzia msanii au mgeni wa siku kwenye show wamesema kwamba Ray apunguze kutumia vipodozi kwani anakuwa kama mchina.
Pia wamemtaka mwigizaji huyo kuwa na moyo wa kusaidia wasanii chipukizi ilikukuza tasnia ya uigizaji hapa nchini.

NAMPENDA MMOJA, NAYE ANAJUA.


















NAMPENDA MMOJA, NAYE ANAJUA.

Kiumbe silete hoja, sikiza nakuambia,
Nimpendaye mmoja, moyoni alonitia,
Hao unao wataja, si wangu wanizushia.
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Apendeza bila koja, wallahi ametimia,
Si usoni hata paja, kila kitu avutia
Nikimuita yuaja, mtiifu wa tabia,
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Hili jambo lina tija, mimi nilo kusudia,
Nimeshatoa mkaja, mahari yafuatia,
Nimeuchoka useja, wa mito kukumbatia,
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Muogope sana mja, mama aliniusia
Haishiwi na harija, mapenzi kukuvunjia
Hatimaye huwa chaja, muhibu awe nokia,
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Kwahivyo sioni haja, ya jina kukutajia,
Kutotaja sikuroja, ni mafunzo ya nabia,
Naomba sikose kuja, hiyo siku kiwadia,
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Ukome kutajataja, njia ni'zo zipitia,
Hayo unayo bwabwaja, yasije kumfikia,
Tungule iwe tunguja, iso faa kupikia,
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Naapa sitakufuja, ulipo nyonda sikia,
Mahaba hayatachuja, kama safi zetu nia,
Lije vumba la kangaja, jua nitavumilia,
Jina sitakutajia, nimpendaye mmoja.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394
Morogoro.

ZITTO NA MAMBO KUMI YALO MSHINDA MAGUFULI
















Siku 100 za Utawala wa Awamu ya 5 chini ya Rais Magufuli
Mambo 10 ya Msingi ambayo Rais Magufuli ameshindwa kuyafanya tangu aingie madarakani.

1 Mikataba yote ya Rasilimali za Nchi - PSAs Kwa Mafuta na Gesi Asilia na MDAs Kwa Madini bado ni Siri na sio Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ambaye kaonyesha hata nia ya kutazama upya mikataba hii na kuiboresha Kwa maslahi ya watanzania. Mapato ya Nchi, makubwa kuliko ya utumbuaji majipu, yanaendelea kupotea. Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi. Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini. Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

2) Posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali bado zinalipwa bila kufutwa kama Mpango wa Maendeleo 2011/2012 - 2015/2016 unavyotaka na kuagiza. Serikali imeongeza posho za kujikimu mpaka tshs 120,000 Kwa siku na Kwa wabunge bado wanalipwa posho ya makalio ya tshs 220,000 Kwa siku. Posho ambazo zimeshalipwa tangu Rais aingie madarakani ni sawa na kujenga barabara zote viporo za lami kuunganisha mkoa wa Tabora ( Kaliua - Urambo na Nyahua - Itigi ).

3) Serikali bado inatumia mashangingi na kila Waziri, Katibu Mkuu na wakuu wa idara wanatumia mashangingi ya gharama kubwa.

4) Tanzania bado inaagiza Sukari kutoka Nje na Serikali haina Mpango wowote ule wa kuondoa tatizo hilo. Hata katika Mpango wa Maendeleo Serikali haisemei sukari kabisa. Uagizaji wa Sukari ni jipu ambalo limeiva Lakini mkamuaji analilea. Hivyo hivyo Kwa sekta ya Nguo bado viwanda vya ndani vinapata ushindani usio halali kutoka Kwa nguo kutoka Nje zenye kuingia nchini bila kodi.

5 Taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha Nje bado imefichwa na haijafikishwa bungeni. Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kudhibiti utoroshaji fedha na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa Kwa wahusika.

7 TAKUKURU bado haina mamlaka ya kukamata na kushtaki wenye makosa ya kifisadi. Vile vile mfumo wa kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje ( reverse burden of proof ) haujaanzishwa nchini na matokeo yake ni kuzorota Kwa juhudi za kumaliza ufisadi Kwa kuboresha mifumo. Kinachoendelea ni kutumbua majipu kimkakati bila kuzuia majipu kuota tena.

8 Mali na Madeni ya Viongozi bado ni Siri. Wananchi hawajui Rais Wao anamiliki nini AMA anadaiwa nini. Hivyo hivyo Kwa viongozi waandamizi wote. Serikali ya Awamu ya Tano imeendeleza mfumo ule ule wa maadili ulio dhaifu na wenye kulea vitendo vya rushwa.

9 Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeshindwa kabisa kushughulikia suala la Zanzibar na matokeo yake ni kuiweka Nchi kwenye hatari kubwa ya kuvunjika Amani. Mshindi wa Uchaguzi Zanzibar hajatangazwa na Rais ametishia wananchi kuwa atatumia majeshi kukandamiza madai halali ya wananchi wa Zanzibar.

10 Hakuna hatua zozote zimechukuliwa kuanza mchakato wa Katiba. Inaonyesha Serikali haina mpango kabisa na Katiba mpya.

IJUE SARATANI(CANCER)















IJUE SARATANI(CANCER)

Saratani ni mkusanyiko wa magonjwa yanayo husiana ambayo huanza mara baada ya seli za mwili kuongezeka na kugawanyika kupita mahitaji ya mwili.
Kwa aina zote za kansa, hutokea pale baadhi ya seli za mwili kuanza kugawanyika bila kukoma na kusambaa katika tishu zingine kutoka pale zilipo anzia!
Saratani ikoje?

Awali ya yote vema mjue kuwa mwili wa mwanadamu una seli zaidi tirioni 37, na zote hizo zina kazi maalum, huchoka, huaribika, na hatimaye hufa! Seli zinapokufa zingine huzalishwa ili kuchukua nafasi ya seli zilizo kufa. Kwa hivyo ili mifumo ya mwili ifanye kazi zake vizuri ni lazima seli zilizochakaa na kuharibika zife.

Saratani huweza kuanza sehemu yoyote ya mwili wa mwanadamu. Saratani inapozuka ule mchakato wa kawaida unaotawala na kuratibu seli huacha kufanya kazi kama inavyotakiwa.
Matokeo ya mchakato kufeli, hupelekea seli kuwa si za kawaida(more and more abnormal). Seli zilizo zeeka, kuchakaa na zilizoharibika huendelea kuishi badala ya kufa kama ilivyo kawaida, na kubwa zaidi seli mpya kuzalishwa kwa wingi sana kuzidi mahitaji ya mwili.
Seli mpya hugawanyika kwa kasi na kwa wingi bila kukoma, na matokeo yake hufanya uvimbe(tumors)

Saratani nyingi hufanya uvimbe ambao ukiugusa huwa mgumu, si wenye kubonyea. Uvimbe huu huwa ni mkusanyiko wa tishu uliotokana na seli za saratani. Saratani ya damu kama vile leukemias huwa haifanyi uvimbe.

Kuna aina mbili za uvimbe wa saratani.
Kuna uvimbe wa saratani unaoitwa malignant: Uvimbe wa namna hii una uwezo kusambaa katika mwili mathalani kwa kupitia mfumo wa damu.

Kuna uvimbe unaoitwa benign ambao wenyewe seli zake hazisambai na kushambulia tishu zingine toka pale ulipozukia, uvimbe huu unaweza kuwa mkubwa lakini ukitolewa kwa upasuaji mara nyingi haurudi tena! uvimbe wa benign huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini isiwe tatizo isipokuwa tu kama ukitokea kwenye ubongo maisha ya mgonjwa huwa hatarini.
Kuna tafauti gani kati ya seli za saratani na seli za kawaida? Saratani huzuka vipi? Kuna uhusiano gani kati ya vinasaba na seli za saratani? Dalili za saratani ndio zipi? Matibabu ya saratani yakoje? Tunajikingaje na saratani?

Leo naomba niishie hapa, nikipata nafasi inshallah nitaendelea huku nikiongozwa na maswali hayo.
Nimeandika makala haya kwa msaada wa tovuti ya National Cancer Institute ya Marekani na tovuti ya American Cancer Society.
Dotto Rangimoto Chamchua (Njano5)
Admin
0622845394