JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!

1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Marko
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Luka
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na  alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

6.#Yakobo
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe.  Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadei)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

NOTE:
13. #Thadayo (au Mathia) ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Huyu alipigwa na mawe  hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka (A.D).

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:23

Nakutakia pasaka njema.!

Malisa Godlisten GJ.!

WAJUE MAADUI WA NYOKA.

WAJUE MAADUI WA NYOKA.

Nyoka wenye sumu ni hatari sana, lakini wao pia wana maadui. Maadui zao ni pamoja na karani tamba, tai wanaokula nyoka (crested serpent eagle), vicheche na mamba. Baadhi ya nyoka wanakula nyoka, kwa mfano King Cobra anaweza kumla cobra. Hivyo nyoka wenye sumu wanahitaji kuchukua hatua mbalimbali Ili kujilinda katika mazingira yenye maadui wengi.

Hatua ya kwanza ni kujifanya aonekane kuwa mkubwa na hatari. Nyoka aina ya Death Adder wanaoishi huko Australia ni moja kati ya nyoka wenye sumu kali zaidi duniani, Lakini hawawezi kushinda tai wanaokula nyoka. Death Adder akikutana na tai, anatulia, kupanusha mwili wake ili ionekane kama tai hataweza kumeza. Kama tai hana maarifa ya kutosha, atamwacha na kuondoka.

Hatua ya Pili ni kujificha. Nyoka aina ya Western diamondback rattlesnake anaweza kujificha vizuri. Kutokana na madoa ya rangi ya kijivu kwenye ngozi yake, anaonekana kama changarawe. Kwa nyoka huyu anayetembea polepole, anaweza kupumzika bila ya kugunduliwa na maadui.

Hatua ya tatu ni kutoa onyo.
Nyoka aina ya rattlesnake anaweza kupiga kelele kwa kutikisika mkia wake ili kuwaonya wanyama wengine wasiingie eneo lake. Na nyoka aina ya Gaboon viper anatoa mlio wa ‘sss’ ili kutoa onyo.

SHIRIKA LA KIJASUSI LA ISRAELI HUMTUMIA MWANAMKE KAMA SILAHA.

SHIRIKA LA KIJASUSI LA ISRAELI HUMTUMIA MWANAMKE KAMA SILAHA.

Mtandao wa Intaneti wa "Sauti ya Israel" umefichua kuwa, silaha ya hatari zaidi inayotumiwa na shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni MOSSAD ni mwili wa mwanamke wa Kiyahudi.

Televisheni ya al Alam imeunukuu mtandao wa habari wa Alsumaria News ukiripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mwili wa mwanamke wa Kiisraeli unahesabiwa kuwa moja ya silaha muhimu sana za kufanikishia malengo ya MOSSAD kiasi kwamba watu wenye ushawishi ndani ya utawala wa Kizayuni wanawashawishi wanawake wa Kiyahudi kutofungwa na maadili yoyote yale na wapewe uhuru kamili wa kutumia wanavyotaka miili yao kwa ajili ya utawala wa Kizayuni.

Mtandao huo umemnukuu kuhani mmoja wa Kiyahudi akisema: Ingawa jamii yetu imeshikamana na dini, lakini tuna wajibu wa kuwashawishi wanawake wa Kiyahudi kujichanganya na watu wa jamii nyingine ili kuenea ukafiri na ufisadi na kudhoofisha misingi muhimu ya jamii hizo, ili iwe rahisi kuzidhibiti.

Mtandao huo umeongeza kuwa, mwanamke wa Kiisraeli anahesabiwa kuwa nguzo moja muhimu sana ya Shirika la Kijasusi la Israel, MOSSAD na wanahesabiwa kuwa ni silaha ya nne muhimu zaidi ya utawala wa Kizayuni baada ya jeshi la majini, jeshi la anga na jeshi la nchi kavu la Israel.

Mtandao huo wa Intaneti umeongeza kuwa, kila mwaka maelfu ya wanawake wa Kiyahudi wanajiunga na MOSSAD na moja ya kazi zao kubwa ni kuuza miili yao, kuua na maovu mengineyo kwa ajili ya kuulinda utawala wa Kizayuni wa Israel.

WATU ZAIDI 69 WAMEKUFA KATIKA MLIPUKO PAKISTAN.

WATU ZAIDI 69 WAMEKUFA KATIKA MLIPUKO PAKISTAN.

Zaidi ya watu sitini na tisa wamekufa na wengine kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye eneo la wazi la kupumzikia lenye shughuli nyingi katika mji wa Lahore nchini Pakistan.

Polisi wanasema mlipuaji mwenye kujitoa mhanga alijilipua karibu na eneo la kuchezea watoto mahali wazazi walipokuwa wamejikusanya ambao baadhi yao walikuwa wakisherehekea siku kuu ya Pasaka.

Wengi ya waliokufa na kujeruhiwa katika tukio hilo ni watoto. Tayari kundi la Talbani la Pakistan la Jamaat ul Ahrar limekiri kuwa ndilo linalohusika na shambulizi hilo. Msemaji wa kundi hilo amesema walikusudia kuwalenga jamii ya wakristo waliopo katika mji huo.

Afzal ni mmoja ya wakazi wa mji wa Lahore yeye alikuwa ni miongoni mwa waliosaidia kuwasaidia majeruhi baada ya mlipuko kutokea.

" Nimewabeba zaidi ya watoto ishirini ambao walipelekwa hosptalini. Nilisaidia kubebe miili mitatu na kupakia kwenye gari la polisi. Wakati mlipuko ulipokuwa unatokea watoto walikuwa wakicheza kwenye uwanja huo wa wazi. Leo jamii ya wakristo walimaliza mfungo na kusherehekea Pasaka. Wakristo wengi walifika hapa katika tukio hili. Siwezi kuelezea jinsi tukio hilo la kusikitisha lilivyokuwa."

Naye Tariq Fatimi ambaye ni mshauri wa Waziri Mkuu wa Pakistani ameiambia BBC kuwa tukio hilo ni la kinyama bila kujali ni nchi gani imelengwa.

" Hata kama shambulizi hilo limetokea Peshawar au Lahore au Brussels au Paris au London, Sisi sote tunapaswa kuwa pamoja kwa sababu huu ni uhalifu ambao hauathiri nchi moja pekee, au jamii moja lakini inaathiri wanadamu wote."

PADRI ATIMULIWA KWA KULAWITI VIJANA ITALIA.

Padri wa Kikatoliki atimuliwa kwa kuwalawiti vijana Italia 

Padri mmoja wa Kanisa Katoliki mjini Milan nchini Italia amesimamishwa kazi baada ya kubainika kuwa amekuwa akimhonga kijana mmoja barobaro ili afanye naye ulawiti.

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo katika eneo la Muggiano mjini Milan, Kadinali Angelo Scola amesema kuwa amemsimamisha kazi Padri Alberto Paolo Lesmo wa kanisa hilo, kwa tuhuma za kumhadaa kijana aliyekuwa mraibu wa mihadarati kati ya mwaka 2009 na 2011 na kisha kufanya naye tendo la liwati.

Kadinali huyo amesema: “Ni majuzi tu tumegundua kuwa Padri Lesmo alikuwa anafanyiwa uchunguzi na vyombo vya dola kuhusu uozo huo tangu mwaka 2013; hata hivyo tumeanzisha uchunguzi wetu juu ya tuhuma hizo, lakini kwa sasa tumemvua Upadri na kumsimamisha kazi.”

Madai ya liwati na visa vya kushiriki ngono na watoto wadogo sio mapya kwa Kanisa Katoliki, na katika miaka ya hivi karibuni, waathiriwa wa vitendo hivyo vichafu wamekuwa wakijitokeza hadharani na kufichua kashfa hizo.

Licha ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kutoa dikrii ya kutaka kuchukuliwa hatua za kinidhamu maaskofu wanaoficha kashfa za kulawitiwa watoto wadogo na mapadri wa kanisa hilo, lakini visa hivyo vimekuwa vikiripotiwa kila uchao.

Miongoni mwa nchi ambazo zimerekodi idadi kubwa ya wakuu wa Kanisa Katoliki kugunduliwa kuwa wanawalawiti wavulana wadogo ni Marekani, Ireland, Uholanzi, Australia, Ufaransa, Ujerumani, Austria, Ubelgiji, Canada, Mexico na Poland.

ISRAELI KUSHIRIKIANA FBI KUDUKUA SIMU.

ISRAELI KUSHIRIKIANA FBI KUDUKUA SIMU.

Baada ya Shirika la Simu za Apple kukataa kushirikiana na Idara ya Polisi ya Upelelezi Marekani FBI katika kuifungua simu aina ya iPhone iliyotumiwa na mtu anayedaiwa kutekeleza mauaji San Bernardino, California mwaka jana, shirika moja la Kizayuni limepewa jukumu la kuifungua simu hiyo.

FBI imesema kuwa imepata njia ya kuifungua simu hiyo ambayo imefungwa na nywila ya siri. Shirika la mitandao ya intaneti la Cellebrite ambalo huunda programu za kiusalama za simu za mkononi, limesema linashirikiana na FBI kuidukua simu hiyo.

Shirika la Cellebrite ambalo ni tawi la shirika la Sun Corp la Japan limesema linaweza kuunda programu mpya itakayowezesha kufunguliwa simu hiyo ya iPhone na hivyo kuhitimisha mvutano baina ya FBI na Apple.

FBI imekuwa ikilishinikiza shirika la Apple kufungua simu ya iPhone iliyokuwa ikitumiwa na mmoja kati ya waliotekeleza mauaji ya San Bernardino lakini Apple imekataa kufanya hivyo kwani huo utakuwa mwanzo wa kudukuliwa taarifa katika simu za watumiaji wa simu za iPhone.

Shirika la Apple limeishtaki FBI katika mahakama nchini Marekani lakini kesi hiyo ambayo ilikuwa imepangwa kusikilizwa Jumamosi iliyopita imeakhirishwa kufuatia ombi la serikali ya Marekani. Watetezi wa haki za binadamu wamelalamikia hatua ya kuakhirishwa kesi hiyo. Wiki mbili zilizopita pia, Rais Obama wa Marekani alisema anapinga kuundwa simu za mkononi ambazo maafisa wa serikali hawataweza kupata maelezo yaliyo ndani kila wanapotaka. Kwa m

VIONGOZI WA UPINZANI CONGO BRAZZAVILLE WAITISHIA KUANDAMANA NCHI NZIMA.

VIONGOZI WA UPINZANI CONGO BRAZZAVILLE WAITISHIA KUANDAMANA NCHI NZIMA.

Viongozi wa upinzani nchini Kongo Brazzaville wameitisha maandamano ya nchi nzima kupinga kuchaguliwa tena Rais Denis Sassou Nguesso mwenye umri wa miaka 72.

Viongozi watano wa upinzani nchini humo walioshindwa katika uchaguzi rais wa Jumapili iliyopita akiwemo Guy-Brice Parfit Kolelas aliyeibuka wa pili kwa kupata asilimia 15 ya kura na Jean-Marie Mokoko ambaye alishika nafasi ya tatu kwa asilimia 14 wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya nchi nzima mnamo Machi 29, kulaani kile walichokitaja kuwa ‘wizi wa kura na utumizi mbaya wa mamlaka.’

Wamewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi katika kila mji kupigania kile walichokiita kuhujumiwa haki zao za kidemokrasia na kushinikiza kuheshimiwa katiba.

Tume ya Uchaguzi nchini Kongo Brazzaville ilimtangaza Denis Sasso Nguesso kuwa mshindi wa kiti cha urais katika uchaguzi wa Machi 20 kwa kupata asilimia 60 ya kura zote halali zilizopigwa.

Nguesso ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, Oktoba mwaka jana alibadilisha katiba na kuondoa kipengee kinachoweka ukomo wa vipindi viwili kwa Rais na kujiandalia mazingira ya kubakia madarakani.

RAIS ASSAD ALIPONGEZA JESHI LA SYRIA KWA KUUKOMBOA MJI WA PALMYRA.

RAIS ASSAD ALIPONGEZA JESHI LA SYRIA KWA KUUKOMBOA MJI WA PALMYRA.

Rais Bashar al-Assad wa Syria amelipongeza jeshi la nchi hiyo kwa kuukomboa mji wa kihistoria wa Palmyra kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.

Rais Assad ameyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na wabunge wa Ufaransa mjini Damascus na kuongeza kuwa, kukombolewa mji huo ni mafanikio makubwa sana kwa taifa la Syria na kunaonyesha namna jeshi la nchi hiyo likishirikiana na makundi ya wananchi linavyoendelea kupata mafanikio na kuzidi kukomboa miji mbali mbali ambayo ilikuwa chini ya udhibiti wa matakfiri wa Daesh.

Wakati huo huo, jeshi la Syria limesema kuwa, baada ya kuukomboa na kuudhibiti mji wa Palmyra, sasa linajiandaa kusonga mbele kwa ajili ya kuikomboa mikoa ya Raqqah na Deir al-Zawr. Kamandi Kuu ya jeshi la Syria imepongeza kukombolewa mji huo wa kihistoria na kusema kuwa, huu ndio mwanzo wa kuporomoka kwa harakati za kundi la kigaidi na kitaifiri la Daesh nchini humo.

Itakumbukwa kuwa, Juni mwaka jana 2015, wanachama wa kundi la kitakfiri la Daesh walibomoa makaburi mawili ya kale ya Mawalii wa Allah katika mji wa kihistoria wa Palmyra mkoani Homs nchini Syria. Mkurugenzi wa Turathi za Kale nchini Syria, Maamoun Abdulkarim, alisema kuwa magaidi hao wa kitakfiri walilipua mabomu ndani ya majengo ya makaburi ya Mohammad bin Ali wa kizazi cha binamu yake Mtume Muhammad SAW na Nizar Abu Bahaaeddine, msomi mtajika wa Kiislamu kutoka Palmyra.

MAJESHI YA SYRIA YAUTEKA MJI WA PALMYRA.

MAJESHI YA SYRIA YAUTEKA MJI WA PALMYRA.

Vyombo vya habari na vilevile wanaharakati huko Syria vinasema vikosi vya serikali vimekamata na kuchukua tena udhibiti wa mji wa kale wa Palmyra uliokuwa mikononi mwa wanamgambo wa IS.

Majeshi ya serikali ya Syria yamekuwa yakipiga hatua kuteka maeneo yanayokaliwa na wapinzani wao na vilevile yaliyokuwa yametekwa na IS tangu majeshi ya Urusi yalipoingia Syira kuisaidia serikali ya Bashar al Asaad kwa mashambulizi makali ya angani .

Shirika la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for Human Rights limesema bado kuna milio ya ufyatulianaji risasi upande wa mashariki mwa mji huo lakini wengi wa wapiganaji wa IS wamefurushwa na kulazimika kurudi nyuma

Tangu IS wauteke mji wa Palmyra mwezi Mei mwaka uliopita wameharibu mengi ya maeneo ya kumbukumbu za zamani jambo lililokemewa na jamii ya kimataifa.

Ushindi huo wa majeshi ya Bashar al Assad ni pigo kwa harakati za waasi na vilevile ni ushindi kwa mbinu za Urusi dhidi ya serikali za kanda zinazowafadhili waasi.

Dotto Rangimoto Chamchua
0622845394/0784845394

KUKIMBIA HUKINGA WATU NA SARATANI.

Utafiti mpya waonesha kuwa kukimbia kweli kunasaidia kukinga saratani

Jarida la Cell Metabolism limetoa ripoti ya utafiti ikionesha kuwa kukimbia kunaweza kuinua kiwango cha mfumo wa kinga, kuzuia uvimbe mpya uibuke mwilini na kupunguza ukuaji wa seli za saratani kwa asilimia zaidi ya 50.

Mtaalamu kutoka chuo kikuu cha Copenhagen Dkt Pernille Hojman na timu yake ya utafiti waliwatumia panya wanaopata saratani kupima mchango wa mazoezi ya kukimbia katika saratani za aina tano ikiwemo saratani ya ini, ya mapafu na ya ngozi.

Katika jaribio, watafiti waliwagawanya panya kwa vikundi viwili, panya wa kikundi kimoja walikimbia kilomita 4 hadi 7 kila usika, na panya wengine hawakukimbia. Matokeo yalionesha kuwa panya waliokimbia kila siku walizuia kuibuka kwa uvimbe mpya, na ukuaji wa seli za saratani ulipungua kwa asilimia 60.

Dkt Hojman amesema, wamethibitisha kwa mara ya kwanza mazoezi ya kukimbia yanaweza kudhibiti moja kwa moja kasi ya ukuaji wa uvimbe. Watafiti wamegundua kuwa kukimbia kunahimiza uzalishaji wa epinephrine, ambayo inaweza kuchochea mfumo wa kinga kuzalisha seli ya NK inayoweza kukinga saratani.

Lakini Dkt Hojman ametambua kuwa kuhusu wagonjwa wa saratani, mazoezi ya kukimbia bado yanahitaji utafiti mwingi zaidi kuthibitisha na si rahisi kujua wagonjwa wa saratani wanahitaji idadi gani ya mazoezi.

UFARANSA: MARUFUKU KUWEKA PICHA ZA WATOTO ZENU MTANDAONI.

UFARANSA: MARUFUKU KUWEKA PICHA ZA WATOTO ZENU MTANDAONI.

Je wajua mwanaKisima? Ngoja nikujuze sasa!

Wazazi wa Ufaransa wapigwa marufuku kuweka picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii.

Ufaransa imeweka sheria mpya inayozuia wazazi kuweka picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii bila idhini yao. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kuweka picha ya mtoto kwenye mtandao wa kijamii ni kosa ambalo adhabu yake ni faini ya Euro elfu 45, au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja.

Polisi wa Ufaransa wana wasiwasi kuwa kuna uwezekano picha zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii zikatumiwa na wahalifu na kuwaathiri watoto.

Na watoto wengine huwa wanataka wazazi wao waheshimu faragha zao, na hawataki picha ziwekwe kwenye social media. Je, uliwahi kuweka picha ya mtoto wako kwenye mtandao wa jamii? Uamuzi wa wafaransa unafaa au umevuka mipaka na kuingilia wajibu na majukumu ya mzazi?

JESHI LA SOMALIA LIMEWAUWA ALSHABABI 60.

JESHI LA SOMALIA LIMEWAUWA ALSHABABI 60.

Jeshi la Serikali nchini Somalia limewauwa wanamgambo 60 wa kundi la kigaidi la Al- Shabaab na kuwakamata wengine 38 katika Somalia ya kati.
Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa askari wa Galmudug Abdikarim Hussein Guled.

Guled amesema kuwa wanamgambo wa Al-Shabaab wamepata kipigo kikubwa katika mikono ya vikosi vya Galmudug na aliapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao mpaka waondolewe kutoka jimbo lote la Galmudug.

BUNDUKI ZAIDI YA 100 ZASALIMISHWA ARUSHA

Utekelezaji wa  zoezi la uhakiki wa Silaha  unaoendelea Mkoani Arusha  limewezesha kupatikana kwa Bunduki zaidi ya mia moja zikiwemo za kivita zilizokuwa zinamilikiwa na wananchi kinyume cha sheria katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama  ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw. Hashim Mgandila  amesema  Bunduki sita za kivita zilitelekezwa kwenye ofisi za vijiji. Na waliokuwa wanazimiki na kwamba zingine za kawaida licha ya wamiliki wake kuwa na vibali asilimia kubwa matumizi yake yanaonekana kuwa na utata.

Zoezi la kuhakiki silaha ni maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Daud Ntabenda linalolenga kudhibiti ongezeko la  matumizi mabaya ya silaha ambazo zimekuwa zikitumika kuua  wananchi wasio na hatia  tatizo ambalo ni kubwa zaidi katika wilaya ya Ngorongoro.

Mkoa wa Arusha unatajwa kuwa miongoni mwa Mikoa yenye watu wengi wanaomiliki silaha  ambazo asilimia kubwa licha ya wamiliki kuwa na vibali upatikanaji wake na matumiz yake yanadaiwa kuwa na utata.

UJUE UKWELI WA UCHAWI NA UNABII WA FIDEL CASTRO.

UJUE UKWELI WA UCHAWI NA UNABII WA FIDEL CASTRO.

"The US will come talk to us when it has a black president and the world has a Latin American Pope.”

Picha ya Fidel Castro ilo andikwa maneno hayo imekuwa ikisimbaa duniani kupitia mitandao ya kijamii, hasa hasa baada Katoliki kupata Papa wa Kilatin.

Pia nimeona rafiki zangu humu facebook wakiendelea kusambaza hiyo picha, leo hii nimeona nizame na kuchimbua ukweli wa utabiri huo, naam, nimelazimika kutafuta ukweli wa hiki kinaochoitwa unabii au uchawi wa Fidel Castro wa kuweza kuona mambo yajayo kabla hayajatukia.

Awali ya yote hakuna ukweli wowote juu ya kauli hii, huu ni uzushi kama uzushi mwingine wa mtandaoni na wa kwenye magazeti na majarida ambayo naweza kusema ya UDAKU. Ambayo siku zote hujitafutia umaarufu kwa kuwalisha maneno wasanii na wanasiasa maarufu.

Nukuu hiyo kumhusu Fidel Castro iliandikwa kwa mara ya kwanza na mwaandishi wa Kiagertina Bwa Pedro Jorge Silans katika jarida la "The Journal Of Carlos Paz" tarehe 10/03/2015.

Uzushi huu wa Bw Solans juu ya Fidel Castro ulimaanisha dhihaka ama istizai lakini katu hauwezi kuuita unabii sababu wakati unaandikwa kwa mara ya kwanza tayari Obama yuko ndani ya White House na Papa Fransis yuko Vatican akihudumu upapa. Nasema ni dhihaka na si unabii kutokana na sababu zifuatazo.

Mosi: Kwanini haya yajulikane baada ya miaka 40?

Tangu mwaka 1973 unaosemekana hayo maneno katamka Fidel Castro hayakujulikana au kuandikwa popote hadi  miaka 40 baadae tena ikiwa tayari Marekani ikiwa na rais mweusi na Katoliki kuwa na Papa wa kilatini? Kwanini mitandao au hilo jarida lilo andika kwa mara ya kwanza lilisubiri Whit house kuwa na rais mweusi na katoliki kuwa na papa wa kilatini?

Pili kwanini mwaka tu?

Solans anasema Mwaka ambao Fidel Castro amesema maneno hayo ni 1973, lakini hataji tarehe na mwezi. Maneno kama haya na tena utabiri mzito na hasahasa ukizingatia kupamba moto kwa vita baridi, iweje tarehe na mwezi wake usijulikane? Hiki ni kiashiria cha urongo na uzushi.

Tatu, Chanzo Cha Habari
Tarehe 10/03/2015 jarida la El Diario de Carlos Paz( The Journal Of Carlos Paz) liliandika makala yenye kichwa kisemacho " Cuba through changing times: The End Of the blockade?"

Mwandishi wa makala hiyo anaitwa Pedro Jorge Solans, pamoja na mambo mengine alo yaandika juu ya USA na CUBA, lakini pia alizungumzia huo utabiri wa Fidel Castro.

Solans amesema mwaka 1973 Kamanda Fidel Castro akiwa ndio kwanza akiwasili Havana akitokea Vietnam alizungumza na wanahabari wa kimataifa. Kipindi hicho vita baridi ilikuwa ndio imepamba moto, mwanahabari kiingereza aitwaye Bryan Davis akamuuliza Castro.

"Unafikiri ni lini hasa mahusiano kati ya Cuba na USA yatarejea tena?"

Fidel Castro akamkazia macho Davis kisha akamjibu.

"Marekani itakuja kukiri kwetu pindi wakiwa na rais Mweusi na Dunia ikwa na Papa wa kilatini" Hiyo nukuu iko kwa kiingereza ila nimeitafasiri hivyo.

Kwa mujibu wa Clarin gazeti maarufu la Argentina, wakati Solan akigundua kauli hiyo ya Caatro alikuwa Havana akifuatilia habari za mahusiano kati ya USA na Cuba.

Solan anasema alipokuwa Cuba alifanya mazungumzo na Dereva wa Tax Eduardo de la Torre aliyemhudumia , na katika mazungumzo hayo ndipo Solan akasikia kwa mara ya kwanza nukuu hiyo ya Castro kutoka kwa Eduardo. Eduard de la Torre ambaye kwa sasa ni Dereva Tax mwaka huo wa 1973 alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Eduardo ni shabiki mkubwa wa Fidel Castro, yeye alimuona Castro kama nabii na alifananisha na Yesu Kristu pale alipomwambia Bw Solan

"Fidel Castro alifufuka mara nyingi kuliko hata Yesu Kristu, hivi unafikiri mara ngapi vyombo habari vya kimataifa viliripoti kuwa kamanda kafa lakini inatokea mzima?" Eduardo alisema kwa mtindo wa kutupia swali kwa Solans. Kwa ushabiki huu na utungaji huu wa hekaya Bwa Eduardo hafai kuwa chanzo cha habari cha kuaminiwa sana hususani habari hiyo ikimuhusu Castro.

Sasa ni ajabu sana maneno ya Dereva wa Tax katika mitaa  kubebwa na mwandishi huyu mazimamazima ikiwa jiji la Havana linasifika kwa nukuu za kuwalisha maneno watu maarufu. Bw Solan hakutakiwa kumtegemea Eduardo pekee kama chanzo sahihi cha habari yake ikiwa mwandishi anayeaminiwa kumuuliza swali hilo Castro yuko katika jijini London na sasa hiv mlevi mbwa, namaanisha angejiridhisha japo kwa kumuuliza Bryn Davis pia.

Nne: Kwanini vyombo vya habari vya Cuba na kimataifa havijaripoti?

Huenda nukuu hiyo ya Fidel Castro ni sahihi, lakini naingiwa na shaka kwasababu hakuna kumbukumbu rasmi ya kiserikali ikionesha kuwa Fidel Castro aliwahi kuzungumza na wanahabari kisha akatamka maneno hayo, lakini pia hakuna chombo chochote kilicho ripoti mkutano huo na maneno hayo hadi pale yalipokuja kuandikwa kwa mara ya Kwanza na Bw Solan.

Tumeona Whitehouse kuna rais mweusi na dunia ina papa wa kilatini, na hivi majuzi tu tumeona Obama akizulu Cuba, hivi kwanini vyombo vya kimataifa havijarejea maneno haya ya Castro wakati vikiripoti ziara ya Obama Cuba? Hiki ni kiashiria tosha kuwa Bw Solan aliamua tu kudanganya ulimwengu.

Hata hivyo, Bw Solans hakujishughulisha kuthibitisha maneno ya Eduardo kwa kutumia kumbukumbu za kihistoria au huenda alifanya hivyo lakini akawa amekosa kumbukumbu hizo, na kubwa zaidi hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha madai yake.

Rafael Rojas, author of A Brief of tha Cuban Revolution aliliambia gazeti la Mexico El Universal kuwa "Siamini hata kidogo kuwa Fidel Castro aliwahi kuzungumza maneno haya ya kinabii"

Rojas anasema iwe Castro au mtu yeyote lakini maneno hayo yamezushwa kama masihara mengine tu, kuonesha jambo fulani ni muhari kutokea, mathalani Cuba kuna msemo maarufu "it will happen when a frog grows hair"

Tano: Fidel Castro ni mbovu katika utabiri.

Wengine wanasema maneno hayo ya uzushi yanauhusishwa na mahojiano kati ya Fidel Castro na Barbara Walter yalofanyika mwaka 1977. Katika mahojiano hayo Feidel Castro alimwambia Barbara huenda USA na Cuba zitarudisha mahusiano  kati ya mwaka 1980 na 1984  kipindi ambacho Jimmy Carter akihudumu awamu yake pili Whitehouse.

Mahojiano ambayo yalibatilisha unabii wowote wa fidel Castro alio wahi kuutoa sababu mwaka 1980 Ronald Reagan alimuondoa Carter Whitehouse kwa ushindi wa kishindo. Kwa hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwa Castro kuwa sahihi na utabiri huu ikiwa utabiri kama huo alio uhusisha na Jimmy Carter ulifeli.

Bofya link hiyo kuona video ya mahojiano kati ya Castro na Barbara ya mwaka 1977.

http://abcnews.go.com/International/video/fidel-castros-prediction-normal-relations-us-27703096

Mwisho.

Ni aibu sana kwa mtu yeyote, kuokota kitu katika mtandao na kisha ukakisambaza bila kukifanyia utafiti, inakuwa aibu kubwa sana jambo hili likifanywa na masomi, lakini fedheha likifanywa na anayetegemewa na anayeigizwa.

Njano5
0622845394

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUUNDA JESHI LA PAMOJA

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUUNDA JESHI LA PAMOJA.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ,EAC, inakaribia kuunda jeshi la pamoja kwa lengo la kulinda taasisi muhimu za kiuchumi za nchi wanachama.

Hayo yamebainika wakati wa mafunzo ya pamoja mjini Nairobi ya wanajeshi 300 kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda.

Kamanda wa Majeshi ya Kenya Jenerali Samson Mwathethe amesema kikosi hicho cha pamoja ni muhimu kwa kuzingatia matarajio makubwa ya ustawi wa kiuchumi Uganda na Kenya kutokana na uzalishaji mafuta na gesi asilia Tanzania.

Akizungumza Ijumaa wakati wa mazoezi hayo Jenerali Mwatheteh amesema, “Shirikisho limeanza kupata muundo wake hatua kwa hatua kama ilivyopangwa na nchi zote za EAC ikiwemo Sudan Kusini. Eneo hili lina ukubwa wa mita mraba milioni 2.4 na idadi ya watu milioni 170. Nchi zote wanachama zinafungamana na udumishwaji amani na usalama katika eneo.”

Mkuu wa Jeshi la Kenya amesema ugaidi ni tishio kubwa zaidi la usalama katika eneo na hivyo nchi zote zinapaswa kushirikiana. Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Ulinzi wa Kenya Raychelle Omamo amesema mafunzo hayo ya maafisa wa kijeshi ni katika fremu ya ushirikiano wa kiulinzi baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha amesema vikosi vya usalama vinapaswa kufahami mbinu za makundi ya kigaidi yanayolenga kuvuruga uchumi wa eneo hilo.

KWANINI NDEGE ZA ABIRIA HAZINA PARACHUTI?

NGOJA NIKUJUZE mwanaKISIMA.

Kwa nini ndege ya abiria haina parashuti?

Ndege ya kivita si kama tu ina parashuti, bali pia ina kiti chenye parashuti kinachomrusha rubani, kama dharura itatokea, kiti hicho kitanmrusha rubani, kisha parashuti itafunguka ili kuhakikisha rubani anashuka kwa usalama. Kiti hiki ni kizito kuliko mtu.

Kuweka viti hivi katika ndege inayoweza kubeba abiria zaidi ya 100 ni jambo lisilowezekana, kwa sababu viti zaidi ya 100 ni vizito kupita kiasi.

Aidha, rubani wa ndege ya kivita akirushwa nje, atapita kwenye kitu kama kifuniko kilicho juu yake, na jambo hili haliwezekani kufanyika kwenye ndege za abiria.

Baadhi ya wahandisi wanajaribu kusanifu ndege ya abiria ambayo paa lake linaweza kufunguliwa na parachuti kubwa itakayoweza kurusha chumba kizima cha abiria. Lakini mpango huo una utatanishi mkubwa. Idadi ya abiria itapunguzwa kwa kiasi kikubwa, na bado haijajulikana kama parachuti kubwa inaweza kufunguliwa na chumba kurushwa kwa mafanikio. Hivi sasa hakuna kiwanda chochote kinachopenda kutengeneza ndege za aina hiyo, na pia hakuna mashirika yoyote ya ndege yanayopenda kutumia ndege zinazobeba abiria wachache.

Kutokana na sababu hizi, parashuti hazitumiwi katika ndege za abiria, bali zinatumiwa katika ndege ndogo zinazobeba watu wachache tu.

KWANINI NDEGE HAFI ANAPOSIMAMA KWENYE UMEME?

Kwa nini ndege hauawi anaposimama kwenye waya wa umeme?

Umeme unaotumika majumbani kwetu una nyanya mbili, moja ina moto na nyingine haina moto. Umeme unaopita kwenye nyaya za Tanzania ni voti 230. Kama mtu akigusa nyaya mbili, au waya wenye moto na ardhi kwa wakati  mmoja, tofauti ya shinikizo la umeme kati ya pande mbili itasababisha mkondo wa umeme kupita mwili wake, na anaweza kuumia au hata kufa. Lakini ni kwanini ndege wanagusa nyaya hizo bila kuumia? Ni kwa sababu anasimama kwenye waya mmoja tu, mkondo wa umeme hautapita mwili wake.

Lakini kama ndege akisimama kwenye waya wenye shinikizo kubwa sana, tofauti ya shinikizo la umeme kati ya miguu  yake miwili itasababisha umeme kupita mwili wake na kumdhuru?

Tofauti ya shinikizo la umeme iko kati ya miguu yake, lakini ni dogo sana, hivyo ni umeme mdogo sana unaopita mwili wake, hivyo hautamdhuru hata kidogo.

PRINCE MURO YAKIVAA KITUO CHA BRT

Proncess Muro ilifanya yake kwa kuingia kituo cha BRT. kwa vyovyote vile itakuwa ilikuwa inashuka na ile road ya kati ya brt sasa kafika down nahis akapitiliza mpk ndan ya kibanda.

Hakuna aliyekufa, huenda ndio majaribio ya mradi wa mabasi yaendayo kasi!! Tutakufa wengi.

VIDEO: HIVI NDIVYO MKUU MKOA ALIYETEMWA NA ALIVYO JIDHALILISHA



UNAJIDHALILISHA KISA UKUU WA MKOA.Unaweza kuwaMtu mzima, yaani si kijanaMsomi, yaani unadegree zakolakini ukafanya mambo ambayo hata mtoto akakushangaa, na yule wa darasa la saba kama mimi pia nikakushangaa!Hivi nini hasa cha mno hata mtu ujidhalilishe? Sasa huyu msomi hapa anaongea pumba tu kama vile cheo cha ukuu wa mkoa kina hati miliki.Full kujipendekeza, sijui ataka apewe shavu lingine, "ati anaomba radhi" pumbavu, kama angekuwa baba yangu nyumbani angekutana na makofi.

Posted by Kisima cha Jangwani on Friday, March 25, 2016

AJALI YAUA WAWILI KENYA

Watu wawili wamefariki na wengine 16 kujeruhiwa baada ya Matatu kugongana ana kwa ana na basi kwenye barabara ya Kakamega-Mumias nchini Kenya. 

Waliofariki ni pamoja na dereva wa matatu hiyo na abiria aliyekuwa amekaa kwenye kiti ya mbele.
Ajali hiyo imetokea karibu na mji wa Joyland kilomita 3 kutoka mji wa Kakamega.

KOREA YA KASKAZINI YATIA JAMBAJAMBA BLUE HOUSE.











KOREA YA KASKAZINI YATIA JAMBAJAMBA BLUE HOUSE.

Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.
Zoezi hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong-un,kulingana na chombo cha habari cha KCNA ambaye alilitaka jeshi kujiandaaa kuivamia na kuiharibu serikali ya kusini.
Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za Pyongyang.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi lake kuwa katika hali ya tahadhari.
Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa Korea Kaskazini.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.
Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani, kusini mwa mpaka wake.

Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake ,ripoti hiyo iliotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House hadi kuwa jivu.
Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini.

Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa,lakini ripoti hiyo ilionya mwisho mbaya wa rais Park.
Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.
Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park Chung-hee halikufanikiwa,raia saba wa Korea Kusini pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini waliuawa.

MBINGU, ANGA, JUA, NA UUMBAJI.













MBINGU, ANGA, JUA, NA UUMBAJI.
Rejea mada yangu juu ya vitu sita ambavyo havikuumbwa na MUNGU.
Wakati wakichangia mada yangu juu vitu sita ambavyo Mungu hakuviumba, watu kadha wa kadha Jamii Forum, whatsapp na facebook walisema kuwa hoja zangu zilijielekeza kama vile kabla ya Mungu kuumba Dunia hakuumba vitu vingine.

Wamejenga hoja kwa kusema kuwa mwanzo sura ya kwanza yote ilikuwa makhususi kwaajili ya kuelezea jinsi Dunia ilivyo umbwa na si ulimwengu. Kabla ya kuumbwa Dunia, tayari ulimwengu ulikuwa ushaaumbwa, na kwasababu hiyo wanahitimisha kwa kusema KIZA ni sehemu ya ulimwengu na kiliumbwa kabla ya Dunia, na Kabla ya Nuru.
Awali ya yote, naelewa kuna galaxy zisizo pungua bilion 100, na kuna matirioni ya nyota. Najua fikra zao kuwa Mwanzo Sura ya kwanza inazungumzia uumbaji wa dunia na si uumbaji wa ulimwengu, kwa hivyo wanasema Kiza kiliumbwa siku nyingi kabla ya matukio yalihotajwa na mwanzo sura ya kwanza.

Kabla sijawajibu hoja zao, naomba tujiulize, kwa mujibu wa mwanzo 1:1 na kwa kuzingatia maandiko mengine ya biblia, Mbingu ni nini? na mbinguni wapi? Kisha tujiulize nch ni nini?
Mbingu ni neno la kiroho zaidi lenye maana ya anga.(space). Wana sayansi wanatumia neno "anga" wakati Mungu anatumia neno "mbingu". Kwa hivyo tukijua maana ya anga kwa vyovyote vile pia tutajua maana ya mbingu.

Anga ni eneo kubwa sana(three dimensional region) ambalo huanzia pale atmosphere inapoishia. Naomba mfahamu kuwa atmosphere ni moja kati ya matabaka ya dunia. Hii ina maanisha pale dunia inapoishia ndipo anga huanza. Kwasababu hiyo, ndio maana wanasayansi wanasema Dunia iko angani.

Anga ndio ulimwengu wenyewe, sababu vitu ambavyo vipo angani galaxy, nyota, sayari, vimondo, setelaiti, na nk ndio hufanya ulimwengu. Anga, ambayo kimsingi ndio ulimwengu umeundwa na vitu vifuatavyo.
1. Normal Matter
Ambayo ni asilimia tano ya ulimwengu wote. Galaxy, nyota, sayari, vimondo, na hata viumbe hai vimetokana na NORMAL MATTER.
2. Dark Energy
Ambayo yenyewe ni asilimia 25
3 Dark Matter
Ambayo yenyewe ni asilimia 70 ya ulimwengu wote.
Kwa hivyo nyota zote ziko angani, na nimesema hapo juu kuwa anga ndio mbingu. Kama wanasayansi wanasema nyota ziko angani, tujiulize Mungu anasema nyota ziko wapi?
"Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze"
Isaya 13:10
"Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni;...."
Nahumu 3:16
"katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni,..."
Mwanzo 22:17
"Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao ng'ara."
Quran 25:61
"Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota."
Quran 37:6

Quran na biblia zote zinasema nyota ziko mbinguni, kama nyota ziko mbinguni kwa mujibu wa Mungu, na kama nyota pia ziko angani kwa mujibu wa sayansi, je nikisema kuwa MBINGU na ANGA ni kitu kimoja nitakosea? Kwa vyovyote vile sitakosea.
Kwahivyo naomba muelewe, mwanzo 1:1 iliposema Mungu aliziumba mbingu ilimaanisha Mungu aliuumba ULIMWENGU. Sababu tumeona mbingu ni mkusanyiko wa matirioni ya nyota na mifumo yake ambayo kwa pamoja hufanya ulimwengu.

Ukisoma astronomy jinsi inavyo zielezea nyota, hasa vile zilivyo undwa, utagundua hazikuanza tu kuwa na Nuru(Mwanga) na Joto kali, bali kuna mambo na michakato ilikuwa inafanyika, na matokeo ya mambo hayo ndio yakapelekea nyota kuwa na mwanga. Kwa hivyo Mungu aliposema iwe Nuru ndio aliruhusu michakato hiyo kuanza kufanya kazi na hatimaye tukapata jua. Lakini kabla ya NURU kuja kulikuwa na nini? jibu KIZA.

"Nchi" maana yake Dunia, lakini lazima tujue na kukubali kuwa kila nyota ina mfumo wake, na katika kila mfumo wa nyota una sayari zake, na kila sayari ina usiku na machana. Kwa hivyo Mungu aliposema iwe NURU, basi hapo hapo nyota zote ulimwenguni zikatoa Nuru au zikawa na uwezo wa kuwa na mwanga.
Kuna baadhi ya mambo yalifanyika maalum kwaajili ya sayari moja moja, lakini kuna baadhi ya mambo yalifanyika kwa sayari zote kwa ujumla. Kwa hivyo siku iliyoumbwa "mchana" katika sayari ya dunia, ndio siku iliyo umbwa mchana katika sayari zote za ulimwengu. Ninasema hili kutokana na sababu kubwa ifuatayo.

Mfumo wa Nyota Jua una jumla ya sayari nane, na dunia ni moja katia ya sayari hizo nane. Kwa hivyo kipindi Jua lilipopewa NURU, ile Nuru yake ilifika katika sayari zote nane. Pale Mungu aliposema Nuru ijitenge na giza, na giza liwe usiku na Nuru iwe mchana, tukio hilo lilitokea kwa Sayari zote. Kwasababu hiyo si kweli hata kidogo kuwa NURU na MCHANA uliotajwa katika mwanzo 1:3-5 ulikuwa makhususi kwaajili ya Sayari Dunia pekee.

Ili useme ile NURU ni makhususi kwaajili ya dunia tu, ni lazima utuambie Nuru hiyo imetoka katika Nyota gani tafauti na nyota jua. Sababu Nyota Jua ndio huangazia sayari zote katika mfumo wa Jua. Hivyo ni dhahiri kuwa wakati Jua lilipoanza kuangazia dunia ndio wakati huohuo lilipoangazia sayari zingine pia.

Mambo mkhususi ya Dunia katika mwanzo sura ya kwanza ni uumbaji wa mito, bahari, miti, wanyama, nk. Haya ndio yalikuwa makhususi kwaajili ya Dunia, na kila sayari ilikuwa na mambo yake makhususi kadiri ya Mungu mwenyewe alivyoona vema, ndio maana tabia na sifa za dunia ziko tafauti na sayari Zuhura, lakini zote zinategemea NURU ya Jua na zote zina usiku na mchana.
Kwa hivyo bado niko katika hoja yangu, kuwa Mungu aliposema kaumba mbingu alimaanisha kaumba ulimwengu. Akaumba Nuru kwa kulifanya jua litoe mwanga, lakini Mungu hakuumba Kiza, bali aliumba Nuru ili kukipiga KIZA, na kwasababu hiyo hakuna ushahidi Mungu akisema ameumba Kiza, hivyo basi KIZA KILIZUKA siku nyingi sana kabla ya kuumbwa kwa ilimwengu.
Njano5
0622845394

KIZA, MUNGU, KIFO, VITA, NJAA NA MARADHI.















KIZA, MUNGU, KIFO, VITA, NJAA NA MARADHI.
Mungu(light) na Kiza(Darkness) ni ndugu. Hakuna aliyeumba, wametokea tu, lakini wa kwanza kutokea KIZA kisha akafuatia NURU (Mungu).

Kiza ni mwanamke, Mungu ni mwanaume, wakati Kiza ni mkubwa kwa umri na hata nguvu kumzidi Mungu, Mungu yeye ni mwingi wa hila na ujanja, kwa hivyo ni mwerevu kumzidi KIZA.
Mungu alifanya hila, na kwa hila yake hiyo akaweza kuumba ulimwengu na malaika wakubwa wanne, ambao ni Mikaeli, Lusifa, Rafaeli na Gabrieli.
KIZA akachukia na kwahivyo pakazuka mapigano kati ya KIZA na Mungu. KIZA anaamini kuwa ulimwengu ambao angeumba yeye ungekuwa bora kuliko huu alio uumba Mungu, na ya kwamba Mungu alijua hilo na alimuonea wivu KIZA.

Inasemekana KIFO(Death) kilizuka pamoja na MUNGU, au kilianza kabla ya Mungu, au kilizuka muda mfupi sana baada ya kuumbwa malaika wanne. Ila mjue KIFO ni moja kitu kikongwe kuwapo, na haijulikani kati ya KIFO na Mungu nani mkubwa, wanaweza kuwa sawa kwa umri au KIFO akawa mkubwa au Mungu akawa mkubwa. Yote ya yote, wakongwe wa wakongwe kabla hata ya ulimwengu haujaumbwa ni KIZA, MUNGU na KIFO.

Kwakuwa Kiza kina nguvu kuliko Mungu, ili mlazimu Mungu kusaidiana na malaika wakubwa kupambana na Kiza, katika mapambano hayo Mungu na malaika wake hawakufanikiwa kumuua Kiza, walichoweza kumfunga Kiza kwa kutumia chapa(mark) ambayo baadae ilijulikana kama chapa ya Kaini(Mark of Cain)

Kitendo cha mapigano hayo kati ya MUNGU na KIZA, kina maanisha kuwa "VITA" ni kitu cha nne kikongwe kikiwa nyuma ya KIFO, MUNGU na KIZA.
Baada Mungu kufanikiwa, KIZA chini ya kifungo chake akawa juu vilindi vya maji, Mungu akaketi juu ya uso wa maji, na wakati huo asilimia kubwa ya ulimwengu ulikuwa ushafanyika kasoro sayari dunia ilikuwa bado haijakamilika. Hata hivyo, kimsingi hata sasa ulimwengu unaendelea kutanuka na kukua na kila siku nyota zinapasuka na kila siku mifumo ya nyota inazaliwa, yote yanafanyika chini ya pumzi ya Mungu(physical laws)

Chapa ikawa ndio kifungo na funguo kwa GEREZA alilofungiwa DARKNESS, na funguo ambazo alikabidhiwa mtoto mpendwa, mtiifu na mnyenyekevu wa Mungu, mtoto huyo ni Lucifer.
Chapa(funguo) ikageuka laana, hajulikani kwanini iligeuka laana, ila inasemekana MFUNGWA(KIZA) alifanya funguo kuwa LAANA kama mbinu ya kutoka kifungoni. LAANA ikamfanya Lucifer kuwa na kibli, na kibli kilionekana pale Mungu alipomuumba mwanadamu, Lucifer alichukia na alikataa kumsujudia Adamu. Naam LAANA IKAWA UASI, na baadaye Lucifer akatimuliwa mbinguni na jeshi la Mikaeli(Michael)

Wanyama wa kwanza kuumbwa walikuwa wanaitwa leviathians, hawa wanyama walikuwa na njaa sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, na kwasababu hiyo basi tunagundua kuwa "NJAA" ni kitu cha tano kikongwe nyuma ya VITA, ingawa kiumri Levithians alianza kisha ndio akafuatia "NJAA"
Baada ya hapo Mungu akamilisha sayari dunia kwa kumuumba mwanadamu, mwanadamu ambaye tuliona Lucifa aligoma kumsujudia. Binadamu anashikwa na maradhi na udhohofika kwa kuugua. Kwasababu hii basi tunagundua "MARADHI" ni kitu cha sita nyuma ya "NJAA"

KIZA, MUNGU, KIFO, VITA, NJAA na MARADHI hivi vyote viko na vilizuka tu na hakuna aliyeviumba. Viumbe wa kwanza kuumbwa na mungu ni malaika, na wanyama wa kwanza kuumbwa na mungu Levithans ambao pia wanatajwa katika Isaya 27:1

Kwakuwa Mungu aliumba binadamu, na kwakuwa Levithans walikuwa ni wanyama hatari sana kwa uhai wa binadamu hasa hasa kutokana na kuathiriwa zaidi na njaa, Mungu akaumba Purgatory kisha akamuagiza Malaika Mikaeli awafukuze levithians duniani na kuwafungia Purgatory. Katika Purgatory Levithians wanaendelea kuishi huku wakiendelea kulana wenyewe kwa wenyewe na huku wakizaana.

Unafikiri ile mijusi mikubwa unayo iona katika filamu imepotea tu? Akina GodZilla wajua wameenda wapi? Elewa hawakupotea bali wamefungiwa katika Purgatory! Ndio Levithians wenyewe hao, na ili waweze kufungiwa "VITA" ilitamalaki na Mikaeli akafanikiwa kuwafungia, waliokufa ndio mnaona masalia yao ya mifupa katika majumba ya makumbusho.
Baadae dunia itaenda mwisho, nakumbuka nilishawahi kuwaandikia juu ya mwisho wa dunia, kitakacho fanya dunia iishe ni kuripuka kwa nyota jua, likitokea hilo uhai katika dunia utatoweka kabisa, lakini huo sio mwisho wa ulimwengu.

Ulimwengu nao utaisha ama utafikia mwisho. Mkumbuke kuwa ulimwengu unaendelea kutanuka na sababu ya kutanuka ni kuendelea kushikilia misingi ya mlango uliotumika kumfungia KIZA. Hata hivyo, kutanuka huku kutapelekea ulimwengu kupasuka na kusambaratika, hapa wana sayansi wanasema kuwa ule mchakato wa BING BANG unaanza tena na kwa hivyo ulimwengu na galaxy zake kuumbika tena.

Kwa upande wa wanasayansi Bing Bang kutokea tena ni mchakato wa matirioni ya miaka, na mchakato huo unahusisha physical law, matters, dark matters, energy, na dark energy. Tukija upande wa kiroho huu ndio wakati ambapo "KIZA" kimetoka kifungoni na kiko vitani na MUNGU.
Kama Mungu akishinda ulimwengu utarudi tena na dunia kuwa Paradiso, na kama KIZA akishinda basi ataumba ulimwengu wake na kwa vyovyote vile wakati huo MUNGU atakuwa amefungwa au ameuliwa.

Mwisho wa dunia utakuwa na dalili nyingi lakini dalili kuu nne ni hizi zufuatazo.

1. NJAA atapata nguvu sana, na chakula kitakuwa hakitoshi ulimwenguni. Hakitoshi haimaanishi chakula cha kutosha hakuna, hapana, bali watu na wanyama watakula lakini hawatashiba.
2. MARADHI naye atapata nguvu sana, si kwamba magonjwa yatakuwa mengi, bali magonjwa yaliyo kuwa yanatibika yataanza kuwa sugu na kukataa dawa, lakini pia yatazuka magonjwa mapya yaso na dawa wala chanjo.
3. VITA naye atapata nguvu, itakuwa ni vita kati usasa na uzamani, ukristo na uislamu, weusi na weupe, magharibi na mashariki, shia na suni, katoliki nautherani, taifa na taifa, kabila kabila.
4. KIFO naye atapata nguvu, na vitu hivyo vitatu vya juu vinaonesha uwepo wa KIFO, na uwepo wake utadhihirishwa na mauji ya halaiki yatakayo sababishwa na NJAA, MARADHI na VITA.
Hata hivyo na hasa kwa mujibu wa biblia kuwa "KIFO" atauliwa na MUNGU, na hili linathibitishwa na nadharia ya biblia kuwa YESU ameshinda MAUTI na ya kwamba atakayemuamini YESU na BABA aliyemtuma HATAKUFA bali ataishi milele. Sasa ili kuwe na maisha ya milele ni lazima "KIFO" afe, yaani asiwepo!
Yohana 5:24

Je Mungu ataweza kumuua "KIFO"?? je kama Mungu anampango wa kumuua "KIFO" je "KIFO" hatofanya hila kwa kumfungulia "KIZA" toka gerezani? Kwa maana hakuna kitu ambacho Mungu anakihofia kama "KIZA" Je katika haya yote, mitume na manabii wana nafasi gani? Je vitabu kama Quran na Biblia pia vina nafasi gani? Kuna tafauti gani kati ya Hell na Purgatory?

Itaendelea
Njano5
0622845394

CHAI YA KIJANI HUPUNGUZA HATARI YA KIFO














Utafiti uliofanyika Japani wathibitisha kuwa kunywa chai ya kijani kunaweza kupunguza hatari ya kifo

Kituo cha taifa cha utafiti wa saratani cha Japani kimesema, watafiti wa kituo hicho wamethibitisha kuwa kunywa chai ya kijani sio tu kunaweza kupunguza hatari ya kifo, bali pia kunatoa mchango wa kidhahiri katika kupunguza hatari ya magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo na ubongo.

Ili kutambua uhusiano kati ya unywaji wa chai ya kijani na kifo, watafiti walifanya utaifiti wa miaka 19 uliowashirikisha watu elfu 90 wenye umri wa miaka 40 hadi 69.
Katika miaka 19 iliyopita, watu 12,874 walioshiriki kwenye utafiti huo walifariki.

Watafiti waligundua kuwa, kwa watu wanaokunywa vikombe zaidi ya vitano vya chai ya kijani kwa siku kwa wanaume, hatari ya kifo ilipungua kwa asilimia 13 na kwa wanawake kwa asilimia 17.

Ingawa unywaji wa chai ya kijani hauna uhusiano na vifo vilivyosababishwa na saratani, lakini hatari ya ugonjwa wa moyo ilipungua.

Kwa nini unywaji wa chai ya kijani unaweza kupunguza hatari hiyo? Watafiti wamesema, catechin iliyoko ndani ya chai ya kijani inaweza kurekebisha shinikizo la damu na mafuta mwilini.

Haya ndugu zangu wanyalu na wabena Lusitu, Luponde, na kwengineko, chai ya kijani ipo huko, kunyweni kwa wingi kama mnataka kukihadaa kifo.

KIZA, MUNGU, KIFO, VITA, NJAA NA MARADHI.


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
VITU SITA AMBAVYO SI VIUMBE VYA MUNGU.

Tarehe Mar 2016 niliandika makala juu mahusiano kati Kiza, Mungu, Kifo, Vita, Njaa, na Maradhi. Makala ile ilizua mjadala mkubwa facebook na whatsapp nilipoiweka, na moja jambo kubwa lilotuvuruga ni uwezo na mamlaka ya Mungu katika uumbaji, na hasahasa ile nadharia ya kuwa MUNGU ni muumbaji wa viumbe vyote ilitumiwa sana watu katika kuikosoa makala yangu.

Awali ya yote nakubali bila kigegezi chochote kuwa Mungu ni muumbaji wa viumbe vyote na ya kwamba ni Mola wa viumbe hivyo. Nakubali kuwa ulimwengu haukuzuka tu wenyewe katika tukio la lisilo ratibiwa. Bali yupo injinia wa Ulimwengu huu ambaye si mwingine bali ni MUNGU.

Misaahafu ya dini za Ibrahim, yaan uislamu, uyaudi na ukristo yote kwa pamoja bila kukhitililafiana inasema ulimwengu na vilivyomo ndani yake havikuzuka kwa bahati mbaya bali vimeumbwa na Mungu.

Kuna viumbe hai kama wanyama na mimea, lakini pia kuna viumbe ambavyo havina uhai kama mawe na mchanga. Vyote hivi Muumbaji wake ni Mungu.

"Mwenyezi Mungu ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Kwa hakika katika hayo ipo Ishara kwa Waumini. " Quran 29:44

"...Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!..." Quran 13:16

"Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake. Kaskazini na kusini ndiwe uliyeziumba....." Zaburi 89:11-12

Hiyo quran 13:16 inatutanabaisha kuwa Mungu ameumba kila kitu, lakini tujiulize, kitu kilichoumbwa na Mungu kinaitwaje? Kwa vyovyote vile kinaitwa kiumbe. Kama ndivyo tunaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Mungu ameumba viumbe vyote badala ya kusema kuwa Mungu ameumba kila kitu.

Twasema kuwa viumbe vyote vimeumbwa na Mungu, je vile ambavyo si viumbe tuna vizungumziaje? Naomba mjue Mungu ameumba viumbe vyote, lakini haimaanishi kuwa ameumba kila kitu. Kuna baadhi ya vitu ambavyo Mungu hakuviumba aidha hakutaka kuviumba au ameshindwa kuviumba.

VITU VIKUU SITA AMBAVYO MUNGU HAKUVIUMBA.

1. MUNGU
Ukisoma misahafu yote mikuu miwili quran na biblia hakuna ushahidi hata mmoja unaonesha kuwa Mungu kaumba Mungu(namaanisha Mungu kujiumba).

Kubwa zaidi katika misahafu hiyo ambayo imeandikwa kwa matakwa yake MUNGU, inaonesha ukuu Mungu, uwezo wake, mamlaka yake, utukufu wake, usafi wake na kila aina ya sifa nzuri na tukufu, lakini hatuoni chanzo chake kikiandikwa humo na hatuoni mwisho wake ukiandikwa humo, zaidi ya vitabu hivyo kusema ufalme wa MUNGU na Nguvu zake hazina mwanzo wala mwisho.

"Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi" Ufunuo 1:8

"Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza. Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni zake Yeye, mwanzo na mwisho...." Quran 28:69-70

Kwa aya hizi, na mafundisho mengine ya kinabii kama haya, yanathibitisha bila shaka kuwa ni kweli kuna mambo au vitu ambavyo Mungu hakuviumba na kwasababu hiyo vitu hivyo haviwezi kuitwa viumbe na ingawa viko. Kitu cha kwanza MUNGU, kipo na hakija umbwa.

Wanaosema kuwa MUNGU ameumba kila kitu waje hapa watuambie "MUNGU" kaumbwa na nani? Wakishindwa kututajia basi waishie kusema Mungu kaumba viumbe vyote lakini si vitu vyote.

2. KIZA
Ukisoma hiyo quran 28:69-70 na ukisoma vizuri ufunuo 1:8 utagundua mambo yote na habari zote kabla ya uwepo wa MUNGU hayajulikani na huenda anayajua Mungu mwenyewe, lakini kwetu sisi tunaona mambo hayo kwetu ni KIZA.

Kwa hivyo tunaweza kusema kabla ya Mungu hajaumba chochote alikuwako yeye na Kiza, Kiza ni mwanamke na Mungu ni mwanaume. Kwakuwa kwa kipindi hicho walikuwa wenyewe, na wanajuana wenyewe, jambo jepesi twaweza kusema hivi vitu ni ndugu. Ipo siku inshallah nitakuja kufafanua kwanini nasema Kiza mwanamke na Mungu mwanaume.

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Mwanzo 1:1-4

Katika andika hilo la juu tunajifunza yafuatayo.

A. Mbingu na nchi zimeumbwa na Mungu. Maji, ardhi na vitu vya kufananayo ni sehemu ya mbingu ya nchi.

B. Mungu aliumba NURU lakini hakuumba KIZA, tunaambiwa tu Kiza kilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji lakini hatuambiwi Mungu aliumba Kiza.
Hiyo mwanzo 1:3 "Mungu akasema, iwe Nuru; ikawa Nuru"

Alijuaje kuwa Nuru imekuwa kama kabla ya Nuru hiyo kulikuwa hakuna Kiza? Je, mbona hatuoni maandiko yakionesha Mungu akisema iwe Kiza kisha kikawa Kiza?

C. Ukisoma mwanzo 1:2 tunaona Mungu akiumba mbingu na nchi kisha Kiza alikaa juu ya uso wa vilindi vya maji, kwasababu hiyo, nikisema kuwa Kiza alikuwako kabla ya mbingu na nchi nitakosea? Kama alikuwako kabla ya mbigu na nchi, ama kabla ya ulimwengu, nikisema kuwa Kiza na Mungu waliishi wenyewe kabla ya ulimwengu pia nitakosea?

D. Baada ya Mungu kuumba Nuru, hapo ndipo alipofanikiwa, kumfungia KIZA, na athari za Kiza akaziita USIKU na athari za NURU akaziita MCHANA. Kwahivyo Mungu hakumuumba KIZA, ila Mungu kaumba Nuru, Mchana, na Usiku.

Kwahivyo kama tuko pamoja, utakubaliana na mimi kuwa KIZA ni moja ya kitu ambacho Mungu hakukiumba. KIZA si kiumbe, KIZA kimezuka tu kama alivyozuka Mungu mwenyewe. Tafauti kubwa kati ya MUNGU na KIZA ni kuwa Mungu kaumba na ni Mola wa viumbe vyote, lakini Kiza hakuumba kitu chochote kwa hivyo si MUUMBAJI.

Astronomy inatuambia kuwa ulimwemgu umeundwa na vitu vikuu vitatu, normal matter, dark matter na dark energy. Normal matter ndio hujumuisha zile atoms zilizo tumika kuumba Nyota,sayari, na vitu vingine.

Normal matter ni asilimia 5 tu ya ulimwengu wote, 25% ni dark energy na 70% dark matter. Hiyo dark energy na dark matter athari zake zinaonekana katika zenyewe hazionekane. Hii huenda ndio KIZA ambacho kimetajwa katika mwanzo 1:1

Astronomy pia yatuambia ulimwengu unatanuka kwa kasi, na ya kwamba unazidi kuongezeka kutokana ile motion iliyosababishwa na BING BANG, kutanuka kwake ina maanisha unazidi kumeza au ama kuingia katika sehemu mbele zaidi kutokea kule ulipo anzia(kipind cha dark age) Swali kule unapoelekea kuna nini kama si Kiza??

Astronomy pia yatuambia hakuna empty space, kama inavyo onekana, katika space waweza kuona ama kudhani hakuna maada yoyote, lakini kimsingi asilimia kubwa ya space ina dark energy na dark matter. Vitu hivi vinaashiria uwepo KIZA mbali na ulimwengu tunao ujua.

3. KIFO
Kwanza naomba tukumbuke wakati Mungu anafikiria kuumba ulimwengu tayari kulikuwako na KIZA. Ili Mungu awe kuumba ulimwengu ilikuwa lazima kwanza amuondoshe au amuue KIZA. Ili Kiza kiweze kufa shuruti pawe na "KIFO" Hata hivyo, kutokana na nguvu za Kiza, basi kikawa hakijakufa bali kilifungiwa.(Rejea mwanzo 1:3 Mungu akatenga giza na nuru)

Pili naomba mjue kuwa kiumbe hai cha kwanza kuumbwa na Mungu ni "NENO" kisha wakafuatia malaika wakubwa wanne(four Arc Angels) ambao ni Mikaeli, Raphaeli, Rucifer na Gabrieli. Hoja inakuja, Mungu alitumia kipimo gani kujua kwamba amefanikiwa kuumba kiumbe hai? Kwa vyovyote vile ili ajue kuwa amefanikiwa kuumba kiumbe hai ni lazima alinganishe uhai uliopo ndani ya kiumbe hai na mauti(KIFO). Kwa hivyo kilianza KIFO kabla ya UHAI, na bahati nzuri maandiko yanakubali kuwa Mungu kaumba uhai, lakini hayaoneshi kuwa Mungu kaumba KIFO.

Wachungaji wetu katika makanisa wanakataa katakata kuwa Mungu kaumba KIFO, wao wanasema KIFO kilisababishwa na shetani, bi maana shetani ndio kaumba KIFO. Huku ni kutokujua, lakini hakuna aliyeumba KIFO, KIFO sio kiumbe na alizuka tu kama alivyo zuka Mungu.

Kama nilivyosema ule muda Mungu anafikiria kuumba uhai, tayari kifo kilikuwako, na kwasababu hiyo, pia haijulikani kati ya Mungu na Kifo na mkubwa(kiumri).

Mungu aliumba uhai, na kwa kupitia huo uhai akaumba mwanadamu, lengo lake lilikuwa mwanadamu aishi milele, lakini kifo kikawa kikwazo katika lengo hili.

Sivyo tu, kwakuwa siku zote KIZA anataka atoke kifungoni, hivyo kila siku anapambana na Mungu kwa lengo la kutaka kumuua, na wakati huohuo Mungu naye anataka kumuua KIZA, mshindi wa pambano hili lazima amtumie "KIFO" na hapa ndipo tunapoona nafasi ya KIFO katika mahusiano ya NURU na KIZA.

Lakini Mungu anasema atakuja kumshinda KIZA na KIFO, na pindi atakapo shinda hakuna roho au mwili utakao kufa.

"na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. " Ufunuo 1:18

4. VITA na NJAA
KIZA baada ya kugundua Mungu ameumba malaika wakubwa wanne, KIZA alichukia na hapo yakazuka mapambano kati ya MUNGU na KIZA. Kwa mapambano hayo ndipo ilipozuka "VITA" mungu alichofanikiwa ni kumfungia KIZA, na funguo zake akakabidhiwa Rucifer. Mark of Darkness ndio Funguo na sehemu alofungiwa KIZA, chapa hii baadae iliitwa mark of cain.

Mnyama wa kwanza kuumbwa na Mungu kabla hata ya wanadamu ni Levithans, hawa ndio ile mijusi mikubwa na Magodizilla. hawa walikuwa na "NJAA" sana kiasi walane wenyewe kwa wenyewe, Hapa Mungu kwa kutumia jeshi lake la malaika waliwaondoa dunia na kuwafungua Purgatory. Hapa pia VITA alihitajika kufanikisha hili.

Tembo na vufaru wanapungua kwa kuuliwa na binadamu, hivi Magodizilla na Levithans waliuliwa na nani? Ikiwa wao walikuwako miaka mingi kabla ya wanadamu? Jibu jepesi ni upanga wa Malaika Mikael na jeshi lakd.

Wakati hayo yakitokea, Darkness akaigeuza ile mark kuwa laana, na laana ile ikasababisha hali ya uasi kwa mtunza funguo. Wakati Mungu anamuumba mwanadamu, na malaika kuambiwa wamsujudie, Rucifer akiwa kesha athiriwa na laana ya funguo akagoma kumsujidia adamu.

Kwa mara nyingine "VITA" ilihitajika katika kumdhibiti Rucifer na kundi lake.

6 MARADHI
mungu hakuumba maradhi, na wala si lengo mungu mwanadamu aumwe na kuteseka kwa maradhi. Ila pale mwanadamu alipoumbwa na afya bora kabisa, na maradhi yakazuka hapo hapo. Baada ya Mungu kuja kumshinda KIFO, pia atakuja kuyashinda MARADHI, na hayo yakitokea katika maisha Paradiso hakutakuwa na KIFO wala MARADHI.

MWISHO.
makala hii haina tafauti na ya juzi, ila leo baadhi ya nukta nimemua kuziongelea kwa undani zaidi ili iweze kujibu maswali na hoja zilizo jitokeza katika makala ya msingi.

Njano5
0622845394

MWANANGU SEMA AMINI.














MWANANGU SEMA AMINI.
1
Mwana ninaye kupenda, naomba sema amini,
Mungu anaye tulinda, akukinge na majini,
Wale wanao kuwinda, Rabi awabwage chini.
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
2
Uvune ulichopanda, shuke moja themanini,
Kama ni nyavu watanda, uwe kingi baharini,
Iwe unafuga kunda, watotoe ishirini,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
3
Wanotaka kukuponda, wasiweze abadani,
Viumbe wafanya inda, hasa wale mafatani,
Mwanangu utawashinda, kwa uwezo wa Manani,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
4
Tazama unavyoenda, sema na wayo njiani,
Njia ni sawa kupinda, isikutoe imani,
Allah atakulinda, uishinde mitihani,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.
5
Kiti usije kukonda, kwa kudekeza lohani
Yote unayoyatenda, yakufae maishani,
Usije ukawa punda, faida ya Baniani,
Namuomba Rahmani, akupe walau shinda.


Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
0622845394/0784845394 Morogoro
MWANANGU SEMA AMINI