MAMBO USO YAJUA KUHUSU NYOTA JUA NA MWISHO WA SAYARI DUNIA.
Jua ndio kitu pekee ambacho kiko katikati ya mfumo wa jua. Jua ni 99.86% ya uzito(mass) wa mfumo wa jua.
Kimsingi jua ni mkusanyiko wa hydrogen na helium, 74.49% hydrogen na 23.8% helium.
Joto la kitovu cha jua linakadiriwa kufikia nyuzi joto milioni 15, wakati tabaka la nje lina nyuzi joto 5500.
Jua huchukua mwezi mmoja kumaliza mzunguko wake katika mhimili wake, na
hii inakadiriwa tu na sababu kubwa umbo la jua ni kama mpira wa plasma.
Kutokana na umbile lake, mzunguko hutofatiana tabaka na tabaka.
Mathalani, sehemu ya tabaka la nje karibu na ikweta yake, humaliza
mzunguko wake kwa siku 25.4 wakati karibu na "poles" huchukua siku 36.
Imethibitika tabaka la ndani la jua huzunguka sana kuzidi tabaka la nje.
Wastani wa umbali kati ya jua na dunia ni km milioni 150 na mwanga
husafiri kwa spidi ya km 300,000 kwa sekunde, teh, ukiwa mwanahisabati
kama mimi na ukikokotoa utagundua mwanga wa jua hutumia dakika 8
kisafiri kutoka katika jua na kutufikia duniani.
Cha kufurahisha
hapa, hii nishati hutumia dakika nane kutufikia duniani, lakini pia
hutumia mamilioni ya miaka kusafiri kutoka katika kitovu cha jua na
kufika katika tabaka la nje la jua(ambapo kutoka hapo ndio hutumia
dakika 8 kufika duniani)
Hii ina maanisha nini? ina maanisha
mwanga wa jua unao uona sasa si wasasa bali ulianza safari yake hadi
kukufukia hapo ulipo mamilioni ya miaka.
Katikati ya kitovu cha
jua asilimia kubwa ya nishati ya jua huzalishwa kutokana na mlipuko wa
kinyuklia ambao huvunja hydrogen (converts into) kuwa helium. 99% ya
nishati ya joto(thermal energy) inayotengenezwa na jua hutokea katika
kitovu chake.
Wanasayansi wanasema kuwa jua iliundwa(formed)
miaka bilioni 4.57 iliyopita kutokana kupasuka na kusambaratika kwa
"giant molecular cloud" lilosheheni kwa wingi hydrogen na helium.
Mpasuko huo ndio ukazaa nyota nyingi ikiwemo na nyota jua
Ikiwa
sasa na umri wa miaka bilioni 4.5 jua iko nusu ya umri wake kama vile
mtanzania akiwa na miaka 30 yuko nusu ya umri wake. Dunia imeshachoma
nusu ya akiba yake ya hydrogen na kiasi kilichobaki kinakadiriwa
kumalizika miaka bilioni 5 ijayo.
Kwakuwa nyota jua iko katika
jamii ya nyota zinazojulikana Yellow Dwarf, hivyo kuisha kwa hydrogen
hakutasababisha kutokea kwa supernova(mlipuko mkubwa wa nyota), bali jua
litabadilika na kuwa jekundu na kubwa zaidi kiasi cha kumeza sayari za
karibu kama zebaki, zuhuru na dunia.
Kwa vyovyote vile
hatutashuhudia kumezwa kwa kudunia, sababu kabla hata ya dunia kumezwa
maji yote juu ya uso wa dunia na chini ya ardhi yatakuwa yamepotelea
angani kama gesi, dunia haitakuwa na maji tena na joto lake litakuwa
kubwa sana kiasi kila kiumbe hai afe. MWISHO WA DUNIA.
Hydrogen
ikiisha na helium itaendelea kuchomeka kwa miaka milioni 130, kwa
kupindi hicho jua na mfumo wa jua utakuwa umebadilika sana, na hilo
likitokea orbiti ya dunia inakuwa si sehemu salama ya dunia.
Mambo yatakayo weza kufanyika ili kuwe na usalama ni kwa orbit hiyo
kuahamishwa kabisa kutoka ilipo sasa, na kwakuwa jua litapoteza kabisa
nishati yake ya sasa na kama tujuavyo uhai uliopo duniani unategemea
sana nishati ya jua, hivyo salama zaidi ni kwa dunia na orbiti yake
kuahamishwa kutoka katika mfumo wa jua na kwenda katika nyota nyingine
ili mradi tu hiyo nyote iwe katika kundi la nyota za likenia katika
galaxy ya milky way.
Inasemekana katika galaxy zote, ni galaxy ya milky way ndio kuna uhai(milky way is only known galaxy dat support life).
Wanaanga bado wanaendelea kuifanyia utafiti anga na ulimwengu kwa
ujumla, tafiti zao huenda zitakuwa msingi mzuri kwa vizazi vijavyo kujua
namna ya kuihamisha dunia au kugundua nyota nyingine yenye sayari
inayoweza kuwa sawa na dunia hata watu wapate kuhamia huko pindi dunia
ikifikia mwisho.
Wanasayansi wanakubali uwepo wa mwisho wa dunia
na wanakubali kuwa nyota jua ina mwisho wake, lakini hakubali kuwa hayo
yanasabishwa na mungu. Hata hivyo, wako busy kuhakikisha dunia haifikii
mwisho.
Njano5
784845394/762845394