Wanajeshi wa Misri na maafisa wa Uigiriki wanatafuta ndege ya shirika la EgyptAir iliotoweka ikitoka mjini Paris Ufaransa kuelekea Cairo Misri ikiwa na abiria 66.
Ugiriki imetuma ndege mbili na pia itatuma meli moja eneo hilo ili kusaidia utafutaji kwenye bahari ya Mediterranean ambako inaaminika huenda ndege hiyo ilianguka.
Nchini Ufaransa mamlaka zinaandaa mkutano wa dharura kujadili kutoweka kwa ndege hiyo.
Waliokuwemo kwenye ndege hiyo aina ya Airbus A320, ni pamoja na Wamisri 30 Wafaransa 15, Mwingereza 1, Mbelgiji 1,Wairaqi 2, Mkuwait 1, Msaudi 1, Msudan 1,Raia wa Chad 1,Mreno 1,Raia wa Algeria 1, na raia wa Canada 1.
Ilikuwa ikisafiri kutoka Ufaransa kwenda Misri na kutoweka kwenye mtambo wa rada kilomita 280 hivi kabla ya kufika pwani ya Misri.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande na mwenzake wa Misri Abdul Fattah al-Sisi wamewasiliana na kuahidi kushirikiana katika uchunguzi, hayo ni kwa mujibu wa shirika la Reuters .