TETEMEKO LINGINE LIMETOKEA JAPANI.
Tetemeko lignine la ardhi lenye nguvu ya 7.3 kwenye vipimo vya Richter limetokea nchini Japan na kuuwa watu 19 na kusababisha uharibifu mkubwa hayo ni kwa mujibu wa mamlaka nchini humo.
Tetemeko hilo lilikukumba kisiwa cha Kyushu ndani ya siku mbili, na kusa sababisha kuporomoka kwa majengo, barabara, mifumo ya maji na umeme.
Wanajeshi 20,000 wametumwa kusaidia juhudi za uokoaji lakini jitihada za uokoaji zimetatizwa na mitetemeko mingine midogo midogo.
Hivi majuzi lilitokea tetemeko Kumamoto hukohuko Japan na kuleta uharibufu na kuua watu, hili sasa lingine, nchi ya Japan inakumbwa na majanga haya kwa mara na kupelekea nchi hiyo kuwa na sheria kali za ujenzi.