WITNES AFUNGUKA KUHUSU PICHA, ASEMA HAWEZI KUMRIDHISHA KILA MTU.

WITNES AFUNGUKA KUHUSU PICHA, ASEMA HAWEZI KUMRIDHISHA KILA MTU.

Witness ameyasema hayo katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa alipost picha hiyo akiwa na lengo la kuwaonyesha watu ni jinsi gani amepungua na kuwaelimisha nini cha kufanya, lakini watu wameichukulia tofauti.

Pia msanii huyo amesema hawezi kumzuia mtu kuwa na mtazamo tofauti kwa kupost picha hiyo, kwani binadamu wanatofautiana kimawazo.

“Ni kwamba sisi binadamu tuko tofauti hauwezi ukamridhisha kila mtu, mimi nimeweka kwa lengo la kuelimisha kuhusiana na masuala ya kupungua, mwengine anaona kwa lengo lake yeye mwenyewe tofauti, kwa hiyo malengo yanatofautiana, unaweza ukafanya kitu ukaona hiki kitu kizuri, mwengine akaona kitu kibaya, so now nimeweka hiyo picha kila mtu anasema kivyake, I dont real understand”, alisema Witness.

Pia Witness amewataka watu watambue kuwa pamoja na wao kuwa wasanii lakini wana maisha yao mengine, na kuwataka wamuache aishi maisha yake.

“Unatakiwa ufike wakati ambao watu wajue kabisa kwamba sometimes nina vitu ambavyo nnaweza nikaamua kuvifanya, so can they just leave me alone.”, alisema Witness.

OBAMA AJUTIA ALICHOKIFANYA LIBYA YEYE NA WAITIFAKI WAKE.

OBAMA AJUTIA ALICHOKIFANYA LIBYA YEYE NA WAITIFAKI WAKE.

Rais wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake ilifeli katika kutatua mzozo wa Libya.
Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake.

Bw Obama amesema Marekani haikua na mpango mahususi wa jinsi taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi.

Alisema haya katika mahojiano na runinga ya Fox News kuangazia mafanikio na mapungufu ya utawala wake.

Eneo la Sirte, alikozaliwa Gaddafi, lilishambuliwa sana na majeshi ya muungano. Hata hivyo ametetea hatua ya kuingilia kijeshi nchini Libya. Marekani na Muungano wa NATO zilitekeleza mashambulio ya anga kuwalinda raia baada ya kuzuka maasi dhidi ya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Lakini baada ya mauaji ya kiongozi huyo, Libya ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makundi ya waasi huku makundi mawili yakiunda serikali na mabunge tofauti.

Katika hatua za kurejesha utulivu serikali ya muungano wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewasili katika mji mkuu Tripoli ili kuanza mipango ya kuongoza nchi ya kurejesha hali ya kawaida.

Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika Novemba na Rais Obama atakabidhi madaraka kwa mrithi wake Januari mwakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.

MANYARA WAPEWA MWEZI MMOJA KUKUSANYA DAMU SALAMA.

MANYARA WAPEWA MWEZI MMOJA KUKUSANYA DAMU SALAMA.

Dkt. Kigwangala amesema hayo baada ya kutembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara, iliyopo mjini Babati na kushuhudia hospitali hiyo ikiwa haina damu ya kutosha kwenye benki yake.
Naibu Waziri huyo amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Ally Uledi, kuanisha mipango ya upatikani wa damu salama katika kipindi cha siku 30,baada ya kushuhudia benki ya damu ikiwa na unit 3 badala ya 150 zinazohitajika.

Aidha, Dkt. Kigwangala ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo ya rufaa ya mkoa kuwa na chumba maalumu cha kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum ambapo amesema wajenge walau vyumba viwili kwa ajili ya shughuli hiyo.

Dkt. Kigwangala amesema kuwa kutokana na hospitali kuhudimia idadi kubwa ya watu haiwezi kufanya kazi ikiwa haina damu ya kutosha vitanda vya kutosha na hata chumba maalum cha wagonja wanaohitaji uangilizi maalum hivyo mkoa huo hauna budi kufanya juu chini kuweza kutatua changamoto hiyo.

10% YA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE KITANZI KWA WAKURUGENZI.

10% YA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE KITANZI KWA WAKURUGENZI.

Amesema suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima na si hiari.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema ambako alifanya mikutano ya hadhara.

“Halmashauri ambayo itashindwa kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama, Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safari,” alisema Waziri Mkuu, Majaliwa.

Mhe. Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.
Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili zitakapofika shilingi milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.

Amesema fedha hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.

HALI MBAYA NA YA KUTISHA KATIKA MAGEREZA YA SAUDIA.

HALI MBAYA NA YA KUTISHA KATIKA MAGEREZA YA SAUDIA.

Maafisa wa utawala wa Kifalme wa Saudi Arabia wameendela kuzuia huduma ya tiba kwa wafungwa wa kisaisa wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa, maafisa wa magereza za Saudia wameendelea kuzuia huduma za tiba kwa Sheikh Hussein Radhi, mmoja wa wanazuoni wa nchi hiyo anayeshikiliwa gerezani.

Sheikh Hussein Radhi anayesumbuliwa na maradhi ya moyo alitiwa nguvuni na vyombo vya usalama vya Saudi Arabia tarehe 22 Machi baada tu ya kutoa hotuba akipinga siasa za ukandamizaji za serikali ya nchi hiyo.

Baada ya kuuawa kidhulma mwanazuoni mashuhuri wa Saudia, Sheikh Nimr Baqir Nimr Januari mwaka huu, Sheikh Hussein Radhi amekuwa akipaza sauti mara kwa mara kupinga siasa za kidhalimu za watawala wa kizazi cha Aal Saudi katika mji wa Ihsaa huko mashariki mwa Saudi Arabia. Katika miaka ya hivi karibuni utawala wa Saudia umezidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wake na maelfui miongoni mwao wanashikiliwa katika jela za nchi hiyo.

Siku chache zilizopita shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilitoa ripoti likieleza wasiwasi wake kuhusu ongezeko la utekelezaji wa hukumu ya kifo nchini Saudi Arabia na kutangaza kuwa, idadi ya watu waliouawa na vyombo vya mahakama vya nchi hiyo katika mwaka uliopita wa 2015 imeongezeka mara mbili ikilinganishwa na mwaka 2014.

Wakati huo huo kituo cha habari cha Nahrein kimeripoti kuwa, baadhi ya vijana wa Saudi Arabia wamelazimika kuacha nchi yao na kukhitari kuishi nje ya nchi kutokana na mbinu mbaya zinazotumiwa na mawahabi wenye misimamo mikali wanaotawala nchi hiyo katika kuhubiri mafundisho ya kidini.

Ripoti za mashirika la kutetea haki za binadamu nchini Saudia pia zinasema kuwa, utawala wa Aal Saudi umezidisha sana ukiukwaji wa haki za binadamu katika miaka miwili ya hivi karibuni kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na unafanya jitihada za kuhalalisha ukandamizaji wao dhidi ya raia hususan wapinzani.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Ulaya pia siku kadhaa zilizopita yalitangaza kuwa watawala wa kizazi cha Aal Saud wamepanua zaidi ukandamiza na dhulma dhidi ya wapinzani katika miaka ya hivi karibuni. Jumuiya hizo zimelaani mauaji ya kijana Makki al Aridh aliyekuwa na umri wa miaka 20 nchini Saudi Arabia na kutoa wito wa kufikishwa mahakamani watu waliohusika na mauaji hayo.

Ni vyema kukumbusha hapa kuwa, siku chache zilizopita askari wa Saudi Arabia walimtia nguvuni Makki al Aridh katika kituo cha ukaguzi barababarani bila ya kutoa taarifa kwa wazazi wake na kumpa mateso makali. Baada ya kumuua kijana huyo, maafisa wa Saudi Arabia waliwaamuru wazazi wake watangaze kwamba, kijana huyo amefariki dunia kifo cha kawaida.

Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu ya Ulaya imesisitiza kuwa vitendo vya ukandamizaji na mateso limekuwa jambo la kawaida katika jela za Saudi Arabia.

Takwimu zinaonesha kuwa, wafungwa elfu 30 wa kisiasa wanashikiliwa katika jela za kutisha za Saudia. Ikumbukwe pia kwamba ukandamizaji mkubwa unaofanyika nchini Saudi Arabia dhidi ya wapinzani wa dhulma na ufuska wa watawala wa kifalme wa nchi hiyo umeifanya Saudia kuwa miongoni mwa vituo vikuu vya ukiukwaji wa haki za binadamu kote duniani.

VIONGOZI WA DUNIA WAMETUMA RAMBIRAMBI KWA INDIA KUFUATIA AJALI YA MOTO.

VIONGOZI WA DUNIA WAMETUMA RAMBIRAMBI KWA INDIA KUFUATIA AJALI YA MOTO.

Viongozi duniani wametuma rambirambi kwa taifa la India baada ya moto uliotokea katika hekalu la Wahindu kusababisha vifo vya watu wasiopungua 110 na mamia ya wengine kujeruhiwa siku ya jumapili (Jana).

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alituma ujumbe katika mtandao wa kijamii na kusema kuwa moto huo mkubwa ilikuwa “wa kuvunja moyo na kushtua” aliongeza kuwa mawazo yake na sala zilikuwa kwa waathirika wa janga. Modi alielekea jimbo la Kusini la Kerala ili kukutana na waliojeruhiwa akiwa na timu ya madaktari wataalamu 15 kutoka Mji Mkuu New Delhi.

Mwana wa kifalme wa Uingereza Prince William na mke wake kupitia msemaji walisema “walihuzunishwa na habari” baada ya kuwasili nchini India siku ya Jumapili kwa ziara rasmi.

"Catherine na mimi tungependa kutoa rambirambi zetu kwa wote walioathirika na moto mkubwa katika hekaluni," alisema William katika sherehe uliofanyika Mumbai.

KENYA YAANZA MSAKO WA AL SHABABI WALIO VAMIA KITUO CHA POLIS.

KENYA YAANZA MSAKO WA AL SHABABI WALIO VAMIA KITUO CHA POLIS.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wameanza msako wa wapiganaji wa Al Shabaab ambao walivamia kituo cha polisi katika kaunti ya Wajir mapema jana (Jumapili).

Kamanda wa polisi wa Wajir mashariki Benson Makumbi alithibisha kisa hicho na kusema kuwa wapiganaji hao walivamia kituo cha polisi cha Diff kilichoko katika mpaka wa Kenya na Somalia, na kutoweka na gari moja la polisi. Alisema kuwa kisa hicho kilitokea majira ya saa tisa asubuhi wapiganaji 100 walipovamia kituo hicho. Kisa hicho kiliwacha maafisa 3 na majeraha ndogo ndogo.

Duru za kuaminika zimesema kuwa stesheni hiyo ambayo kwa kawaida huwa na maafisa 24 ilikuwa na maafisa 18 pekee wakati wa uvamizi huo.

SERIKALI YA NIGERIA IMEMKAMATA KAMANDA WA BOKO HARAM.

SERIKALI YA NIGERIA IMEMKAMATA KAMANDA WA BOKO HARAM.

Serikali ya Nigeria imesema kuwa imekamata kamanda wa kundi la kigaidi la Boko Haram ambaye anashukiwa kuongoza shambulizi la bomu katika jengo la umoja wa mataifa (UN) mjini Abuja mnamo Agosti 26, 2011.

Kwa mujibu wa taarifa uliotolewa na msemaji wa wizara ya usalama wa ndani,Tony Opuiyo, mshukiwa huyo kwa jina Mohammed Usman au Khalid Al-Barnawi kwa jina lingine, alitiwa mbaroni mjini Lokoja katika jimbo la Kogi nchini humo. Opuiyo alisema kuwa kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua muhimu katika vita dhidi ya ugaidi.

Kulingana na Opuiyo, Al-Barnawi amekuwa akiongoza mashambulizi ya kigaidi nchini Nigeria na kupeleka vijana kwa mafunzo ya kigaidi mashariki ya kati na Afrika kaskazini.

AU YASEMA UCHAGUZI WA DJIBOUTI ULIKUWA HURU NA HAKI.

AU YASEMA UCHAGUZI WA DJIBOUTI ULIKUWA HURU NA HAKI.

Licha ya lalama kutoka vyama vya upinzani, lakini Umoja wa Afrika AU umesema uchaguzi mkuu wa Djibouti wa Ijumaa iliyopita ulikuwa huru na wa haki.
Mkuu wa timu ya waangalizi wa AU katika uchaguzi huo, Soumana Sako amesema licha ya uchaguzi huo kukabiliwa na kasoro za hapa na pale, lakini ulikuwa huru na wa haki. Amesema vyombo husika vilionyesha uwazi wa hali ya juu, jambo ambalo linaufanya uchaguzi huo kuhesabiwa kuwa huru.

Viongozi wa upinzani nchini Djibouti wametangaza kutotambua ushindi wa Rais Ismail Omar Guelleh katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa iliyopita. Muhammed Tourtour, mmoja wa wagombea watano wa upinzani katika uchaguzi huo ametaja kama kichekesho na ndoto tangazo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kwamba Rais Guelleh alishinda kiti hicho kwa asilimia 86 na kusisitiza kuwa, uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu na kasoro nyingi.

Licha ya vyama vingi vya upinzani kususia uchaguzi huo, lakini Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi imesema kuwa asilimia 68 ya watu laki 1 na 87 elfu waliotimiza masharti ya kupiga kura walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo, madai ambayo upinzani unasema kuwa hayaingii akilini. Rais Guelleh mwenye umri wa miaka 68, amekuwa madarakani tokea mwaka 1999.

Djibouti ambayo ni nchi ndogo ya Pembe ya Afrika yenye idadi ya watu wasiofikia hata milioni moja, mwaka 2011 ilishuhudia wimbi la maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena Rais Guelleh ambaye ilisemakana kuwa alipata asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Maandamano hayo yalijiri baada ya Rais Guelleh kuifanyia marekebisho katiba ya nchi, ili kumruhusu kugombea kiti hicho kwa mara ya tatu mfululizo.