KUVURUGA KWA SIMBA, MO ATOA YA MOYONI.


Michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imemalizika hapo jana na Simba SC ikijikuta ikiangukia nafasi ya tatu baada ya kupokea kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa JKT Ruvu na hivyo kusalia na alama 62 huku Azam wakifikisha alama 64 na kushika nafasi ya pili baada ya kutoa sare ya goli 1-1 na Mgambo JKT,

Shabiki wa damu wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ ameamua kufunguka yaliyo moyoni mwake kutokana na matokeo hayo.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Simba na JKT Ruvu, MO ambaye pia ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group) alitoa yaliyo moyoni kwake kuhusu Simba kupitia ukurasa wake wa Twitter, ujumbe ambao ulionekana kuwagusa mashabiki wa Simba na wadau wengine wa michezo nchini.

MO aliandika

“#Simba mnatunyima raha, tumechoka kutaniwa na kutukanwa mitaani”

BREAKING NEWS: KITWANGA ATUMBULIWA


Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Charles Kitwanga kwa kosa la kuingia Bungeni akiwa amelewa

ALIYEANDIKA MWANYANGE APINDUE NCHI ATIWA MBARONI.

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha linamshikilia mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 17 mwaka huu saa 09:00 asubuhi .
Ameeleza kuwa mtuhumiwa alaindika haya katika mtandao wa Facebook

“Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti.”

Aidha mtuhumiwa aliandika ujumbe mwingine kuwa

,”Dkt Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kushtuka naomba Mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”.

Kamanda wa Polisi alisema kuwa, ni vyema wananchi wakatumia mitandao kwa njia iyakayolisaidia taifa badaala ya kutumia kusambaza jumbe za matusi au uchochezi kwani watajikutaka katika mazingira magumu.  

WEMA SEPETU: ALI KIBA WANGU MUMUACHE TU.

Wema Sepetu amezidi kuonyesha mapenzi aliyonayo kwenye kazi za msanii Alikiba na kusema huwa zinamkosha sana na kudai hajawahi kumuangusha siku zote

"Ila huyu bichwa wangu mimi ananikoshaga sana. Na mumuachage tu kwakweli. Bichwa una sifa lakini maana si kwa Vocal hizi. Halafu mimi siwezi kukubania namba bana. Naupenda sana huu wimbo jamani. Wajua kutukunaga mashabiki wako. Good work Bichwa wangu Officialalikiba did it again ladiez & Gentlemen"  aliandika Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu amempa pongezi msanii Alikiba kwa kuweza kusaini mkataba chini ya kampuni ya muziki ya 'Sony Music' na kusema kuwa alistahili hilo na zaidi ya hilo kwani anakipaji kikubwa.

" God Grants accordingly... Congrats Bichwa wangu for that Big Contract... You deserve it & more... Time Heals all wounds... The Sky remains to be the only Limit for u baba..." 

NDEGE YA MISRI YASEMEKANA ILIDUNGULIWA NA MAGAIDI.


Maafisa nchini Uigiriki wanasema vipande viwili “vinavyodhaniwa kuwa mabaki ya ndege ya iliotoweka ya Misri

"yameonekanayakielea katika bahari ya Mediterranean", bado haijabainika kama kweli ni ya ndege hiyo.

Waziri wa uchukuzi wa Misri r Sharif Fathi anasema kuna uwezekano mkubwa kwamba ndege hiyo “iliangushwa na magaidi”, lakini hakuna uwezekano mkubwa wa matatizo ya kiufundi.

Maafisa nchini Uigiriki wanasema ndege hiyo Airbus A320, iligeuka “ nyuzi 90 kushoto na kisha nyuzi 360 kulia kabla ya kutumbukia baharini kutoka umbali wa futi 27, 000.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema ndege hiyo nambari MS804, ilianguka.

HATIMAYE, NDEGE YA MISRI IMEANGUKA BAHARINI.

Hatimaye imethibitika ndege ya Misri imeanguka baharin,juhud za kusaka mabak zaendelea huku kukiwa na hisia za kigaidi.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo awali iliripotiwa kutoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 66,na miongoni mwao kulikuwa na watoto 3,wafanyakazi watatu wa usalama na wahudumu saba.

Ndege hiyo ilipaa angani saa 11:09 usiku na ilitoweka ikiwa kilomita 16 ndani ya anga ya Misri na kupoteza mitambo ya rada saa 2:45 asubuhi,afisa mmoja katika shirika hilo la ndege alisema.

Sasa imethibitika ndega hiyo kuanguka bagarini na Operesheni ya kutafuta ndege hiyo imeanzishwa.

TAARIFA ZA SASA KUHUSU NDEGE YA MISRI ILOPOTEA.


Wanajeshi wa Misri na maafisa wa Uigiriki wanatafuta ndege ya shirika la EgyptAir iliotoweka ikitoka mjini Paris Ufaransa kuelekea Cairo Misri ikiwa na abiria 66.

Ugiriki imetuma ndege mbili na pia itatuma meli moja eneo hilo ili kusaidia utafutaji kwenye bahari ya Mediterranean ambako inaaminika huenda ndege hiyo ilianguka.

Nchini Ufaransa mamlaka zinaandaa mkutano wa dharura kujadili kutoweka kwa ndege hiyo.

Waliokuwemo kwenye ndege hiyo aina ya Airbus A320, ni pamoja na Wamisri 30 Wafaransa 15, Mwingereza 1, Mbelgiji 1,Wairaqi 2, Mkuwait 1, Msaudi 1, Msudan 1,Raia wa Chad 1,Mreno 1,Raia wa Algeria 1, na raia wa Canada 1.

Ilikuwa ikisafiri kutoka Ufaransa kwenda Misri na kutoweka kwenye mtambo wa rada kilomita 280 hivi kabla ya kufika pwani ya Misri.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande na mwenzake wa Misri Abdul Fattah al-Sisi wamewasiliana na kuahidi kushirikiana katika uchunguzi, hayo ni kwa mujibu wa shirika la Reuters .

NDEGE YA MISRI YAPOTEA KWENYE RADA, HAUJULIKANI ILIPO

Ndege ya abiria ya shirika la EgyptAir iliyokuwa imebea abiria 56 na wahudumu 10 wakiwemo marubani imetoweka kwenye rada, ikitokea mji mkuu wa Ufaransa Paris kuelekea Cairo, mji mkuu wa Misri.

Gazeti la serikali la Ahram limeripoti kuwa, ndege hiyo yenye nambari ya usajili A320, ilikuwa inaruka umbali wa mita 11,300 kabla ya kutoweka kwenye rada, mashariki mwa bahari ya Mediterranean, maili 10 kabla ya kuingia kwenye anga ya Misri. Maafisa wa Idara ya Safari za Anga nchini Misri wamesema yumkini ndege hiyo imeanguka katika bahari hiyo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi ya Misri, abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo ni pamoja na Wamisri 30, raia 15 wa Ufaransa na Muingereza mmoja.

Itakumbukuwa kuwa, ndege nyingine ya abiria ya shirika la Metrojet la Russia nambari A321, ilianguka katika Peninsula ya Sinai nchini Misri Oktoba 31 mwaka jana, na kuua watu wote 224 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Aidha ndege nyingine ya abiria ya shirika la EgyptAir iliyokuwa na abiria 55 na wahudumu 7 ambayo ilikuwa inatoka Alexandria kwenda jijini Cairo, ilitekwa nyara na raia wa Misri ambaye aliaminika kuwa na akili taahira kwa jina Seifuddin Mustafa ambaye alidai kuwa alifanya hivyo ili kuishinikiza serikali ya Cairo iwaachie huru wafungwa wa kisiasa kabla ya kubadili kauli yake na kusema kuwa alitaka aletewe mtalaka wake raia wa Cyprus waonane katika uwanja wa ndege wa kisiwa hicho.  

Mama mzazi wa binti aliyebakwa Morogoro alitumiwa video na kuipeleka polisi

Mama mzazi wa binti mmoja mkazi wa Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro hivi karibuni alipokea ujumbe wa picha ya video katika simu yake ya mkononi na haraka aliifungua akiwa na shauku ya kuitazama.

Lahaula! Shauku yake ya kuitazama video hiyo aliyodhani ni sawa na nyingine za matukio ambazo amekuwa akiziona zikisambazwa mitandaoni, iligeuka huzuni na fedheha kubwa alipoona ikimwonyesha bintiye akidhalilishwa na wanaume huku akilalamika asirekodiwe bila mafanikio.

Mama huyo alijizoazoa haraka na simu yake akatimua mbio hadi Polisi kuripoti tukio hilo lililolenga kumdhalilisha binti yake na kuifedhehesha familia nzima. Hicho ndiyo kiini cha vijana 11 wa Dakawa kukamatwa ili waisaidie Polisi kuhusu walioshiriki tukio hilo na walioisambaza video hiyo kwa mama huyo na kwenye mitandao ya kijamii hasa WhatsApp.

Katika video hiyo, wakati mwanamme mmoja akimdhalilisha huyo binti, mwingine alikuwa akirekodi na baada ya kukamilisha tendo hilo lisilo na utu tena bila huruma waliwatumia watu wengine katika eneo la Dakawa.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa aliliambia gazeti hili jana kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuona video ile alikuwa mama wa msichana. “Alikimbia polisi kwenda kutoa taarifa,”alisema Betty.

Baada ya kufika Polisi, Betty alisema polisi walimwambia mama huyo hawawezi kuandika maelezo hadi mhusika ambaye ni binti yake afike kituoni. Walisema hivyo kwa sababu ni mtu mzima hivyo anatakiwa kutoa maelezo mwenyewe. Saa chache baada ya kuandikisha maelezo yake, polisi waliwakamata vijana wawili kwa tuhuma za kuhusika na unyama huo. Betty alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na leo watafikishwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na kwamba hadi jana watuhumiwa 11 walikamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Matei alisema tisa kati yao wanaoshikiliwa ni kwa kosa la kusambaza picha za utupu huku vijana wawili ambao ni Zuberi Thabiti (30) na Iddy Adamu (32) ni kwa kosa la kufanya mapenzi na msichana huyo kwa nguvu huku wakirekodi.

Ilivyokuwa

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walifanya kitendo hicho Aprili 28 mwaka huu majira ya saa 1.00 usiku katika nyumba ya kulala wageni yenye jina la ‘Titii’ iliyopo Dakawa.

Kamanda Matei alisema kuwa binti huyo aliitwa kwenye nyumba hiyo ya wageni na Thabiti ambaye ni mkazi wa Mbarali wilaya ya Mbeya ambaye alikuwa na uhusiano naye kimapenzi. Baada ya kuingia chumbani alimkuta pia Adamu mkazi wa Makambako, Njombe ambao walimlazimisha kufanya mapenzi huku mmoja akimrekodi picha za video na baadaye kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Wanaoshikiliwa kwa kosa la kusambaza picha za utupu ni Rajabu Salehe (26), Said Athman (26), Musi Ngai (36), Said Muhammed (24), John Peter (24), Hassan Ramadhan (27), Ramadhan Ally (26), Lulu Peter (38) na Magreth Njonjone (30).

Wote ni wakazi wa Dakawa, Morogoro na wamevunja Sheria ya Makosa ya Mitandao, kifungu namba 14, kifungu kidogo (1) (a)

Kamanda Matei alisema wakati wa tukio hilo watuhumiwa hao walimtisha binti huyo kwa kisu ili asipige kelele wakati akidhalilishwa na walimtaka asitoe siri hiyo vinginevyo watamuua.

Kamanda alisema wawili hao ni marafiki wa msichana huyo na kwamba Thabiti ambaye ni mpenzi wa sasa wa msichana huyo alipanga na Adamu ambaye ni mpenzi wake wa zamani kumkomesha.

Alisema Thabiti alimwambia mpenzi wake wakutane hotelini. Msichana alipofika aliwakuta chumbani huku Adamu akiwa ameshika kisu na kamera. “Wakamlazimisha afanye vile na kumtishia kumuua kama angekataa,”alisema Matei.

Hata hivyo, Betty alisimulia kisa hicho na kusema watuhumiwa hao walifanya unyama huo kwa sababu ya usaliti wa mapenzi. Alisema msichana alidaiwa kujihusisha kimapenzi na dereva wa mpenzi wake.

Kwa mujibu wa Betty, baada ya mpenzi wake kugundua alipanga njama ili kuwakomoa wote wawili. Alisema mpenzi wake alimwambia wakutane hotelini na alipofika alimkuta Zuberi pamoja na dereva wa mchumba wake hotelini.

“Akawambia wafanye kile kitendo huku akirekodi video,”alisema Betty. “Nia yake ilikuwa kuwakomoa…kwa nini atembee na dereva wake,”alisema Betty na kwamba baada ya hapo picha hizo zilianza kusambaa.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema hali hiyo inaonyesha jinsi maadili yanavyozidi kuporomoka katika jamii.

“Hilo siyo kosa la kisheria peke yake ni udhalilishaji mkubwa,”alisema.

Dk Hellen alisema licha ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kukemea suala hilo ni vyema jamii ikazingatia suala la maadili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Edda Sanga alisema vyama vya kutetea haki za wanawake vinafanya mkutano wa pamoja kujadili suala hilo.

“Leo (jana) tumekutana ili tujadili na kuja na tamko la pamoja,”alisema Sanga na kuongeza kwamba jambo hilo halivumiliki kwa sababu vitendo kama hivyo vinaendelea kujitokeza mara kwa mara.
  • Imenukuliwa kutoka gazeti MWANANCHI