RUSSIA YASEMA UVAMIZI WA MAREKANI HUKO LIBYA NDIO CHANZO CHA KUVURUGIKA NCHI HIYO YA AFRIKA.

RUSSIA YASEMA UVAMIZI WA MAREKANI HUKO LIBYA NDIO CHANZO CHA KUVURUGIKA NCHI HIYO YA AFRIKA.

Serikali ya Russia imesema kuwa uvamizi wa kijeshi wa Marekani huko Libya ni hatua iliyovuruga uthabiti wa nchi hiyo.
Serikali ya Russia imesema kuwa hatua ya Marekani na waitifaki wake ya kuivamia kijeshi Libya na kupelekea kung'olewa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi, imesababisha kugawanyika Libya.

Serikali ya Russia imeutaja uvamizi wa kijeshi wa Marekani huko Libya, kuwa ni pigo kubwa kwa nchi hiyo.

Rais Vladimir Putin wa Russia mara kadhaa alishawahi kutahadharisha kuhusu athari za kuvamiwa kijeshi Libya na kile kinachoshuhudiwa hivi sasa nchini humo.

Akizungumza kwenye mahojiano na televisheni ya Fox News ya Marekani, Rais Barack Obama wa nchi hiyo juzi Jumapili alisema kuwa athari za kuishambulia kijeshi Libya, zilikuwa ni kosa lake kubwa, japokuwa wakati huo alikuwa akidhani kwamba uvamizi huo ulikuwa sahihi. Rais Obama aliyatamka hayo wakati alipoulizwa swali kuhusu kosa kubwa zaidi alilowahi kufanya katika kipindi cha utawala wake.

Baada ya mapinduzi ya wananchi wa Libya na kung'olewa madarakani kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi, baadhi ya nchi ziliyaunga mkono makundi ya kigaidi nchini humo, na kuzuia kuingia madarakani utawala wa kidemokrasia.

JIMMY CARTER: MAREKANI NI NCHI AMBAYO DAIMA IKO VITANI.

JIMMY CARTER: MAREKANI NI NCHI AMBAYO DAIMA IKO VITANI.

Sera za kijeshi na za kupenda vita za Marekani zinakosolewa kote duniani na hivi sasa hata wakuu wa nchi hiyo wameanza kukosoa sera hizo.

Jimmy Carter, rais wa 39 wa Marekani kutoka mwaka 1977 hadi 1981, katika mahojiano na jarida la Time amesema tokea kuanzishwa Umoja wa Mataifa baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia hadi sasa, Marekani daima imekuwa vitani.

Rais huyo wa zamani wa Marekani ambaye aliwahi kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel, amesema tangu kumalizika Vita Vikuu Vya Pili vya Dunia Marekani imeanzisha vita katika nchi 30 duniani.

Matamshi ya rais wa zamani wa Marekani ni dalili ya wazi kuwa nchi hiyo haiwezi kutekeleza mipango yake ya kiuchumi na kisiasa pasina kuwepo vita.

Kwa hakika, Marekani katika muundo wake wa sasa iliibuka katika nusu ya pili ya karne ya 18 baada ya kupigana vita vya uhuru na Ufalme wa Uingereza. Tokea wakati huo nchi hiyo kimsingi imekuwa vitani. Marekani ilipigana vita na Uingereza mwaka 1812, kisha ikaingia vitani na Mexico mwaka 1846 na vita na Uhispania mwaka 1898. Kisha iliingia katika Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia mwaka 1917 na baada ya hapo ikaingia katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia vilivyoanza mwaka 1941.

Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Marekani iliendeleza sera zake za kichokozi na vita kwa kisingizio cha kutetea kile inachodai kuwa ni uhuru duniani. Hapa tunaweza kutaja baadhi ya vita ambavyo Marekani imejihusisha navyo tokea wakati huo ambavyo ni, Vita vya

MKUTANO JUU YA NJIA IPI LIPITE BOMBA LA MAFUTA UNAFANYIKA UGANDA.

MKUTANO JUU YA NJIA IPI LIPITE BOMBA LA MAFUTA UNAFANYIKA UGANDA.

Mkutano unaohusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Bahari ya Hindi ulianza jana katika mji mkuu wa Uganda Kampala.

Taarifa zaidi kutoka Uganda zinasema kuwa, mkutano huo unayashirikisha mataifa waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaani Kenya, Uganda na Tanzania- ambapo baada ya siku tatu maafisa wa serikali kutoka mataifa hayo wataamua iwapo bomba hilo linafaa kutoka Uganda na kupitia nchini Tanzania hadi Bandari ya Tanga au kupitia Kenya hadi Bandari ya Lamu au Bandari ya Mombasa.

Bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda litakuwa na urefu wa kilometa 1,410 na litasafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima eneo la ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Bomba la kutoka Hoima na kwenda Lokichar kisha hadi Lamu litakuwa na urefu wa kilomita 1,476.

Bomba la kutoa mafuta Lokichar kisha kupitia Hoima nchini Uganda na kufika Tanga litakuwa na urefu wa kilomita 2,028.

Hivi karibuni Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania iliwahakikishia Watanzania kuwa serikali ya nchi hiyo ina uhakika wa asilimia 98 wa kupata mradi wa ujenzi wa bomba hilo la mafuta kutoka Uganda kuelekea bandari ya Tanga, mradi ambao unapiganiwa pia na nchi jirani ya Kenya.

WAZIRI MKUU WA ITALY YUKO JIJINI TEHRAN.

WAZIRI MKUU WA ITALY YUKO JIJINI TEHRAN.

Waziri Mkuu wa Italia Matteo Renzi amewasili mjini Tehran mapema leo akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa kisiasa na kiuchumi wa nchi yake.
Katika uwanja wa ndege, Waziri Mkuu wa Italia alilakiwa na Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara Muhammad Reza Neematzadeh.

Katika safari yake hiyo inayolenga kuinua na kustawisha kiwango cha uhusiano baina ya pande mbili baada ya kipindi cha vikwazo dhidi ya Iran, Matteo Renzi ameandamana na ujumbe wa watu 250 unaojumuisha maafisa wa kisiasa na kiuchumi wa nchi yake.

Imeelezwa kuwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Hassan Rouhani pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kustawisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa nchi mbili pamoja na kushiriki mashirika na wawekezaji wa Italia katika sekta ya uchumi na biashara ya Iran, ni miongoni mwa malengo ya safari ya Waziri Mkuu wa Italia hapa nchini.

Kabla ya safari yake hiyo, Matteo Renzi alisisitiza kuwa Italia imedhamiria kustawisha uhusiano wa pande mbili katika nyanja zote na kufidia fursa yake iliyopoteza ya biashara na Iran katika kipindi cha vikwazo vilivyowekwa na Magharibi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Italia inakusudia kurejesha kiwango cha mabadilishano ya kibiashara na Iran cha mwaka 2010, ambacho ni cha yuro bilioni saba kwa mwaka.

FUAD MASUM: ILI IRAQ IWEZE KUPAMBANA NA MAGAIDI INAHITAJI MISAADA YA KIMATAIFA.

FUAD MASUM: ILI IRAQ IWEZE KUPAMBANA NA MAGAIDI INAHITAJI MISAADA YA KIMATAIFA.

Rais wa Iraq amesema kuwa, ili nchi hiyo iweze kupambana na ugaidi inahitajia himaya ta kimataifa.

Rais Fuad Masum amesema hayo mjini Baghdad katika mazungumzo yake na Jean-Yves Le Drian Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa na kutoa wito wa kuongezwa ushirikiano mpana zaidi wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama na Iraq katika vita dhidi ya ugaidi.

Kwa upande wake Salim al-Jabouri, Spika wa Bunge la Iraq amesema katika mazungumzo yake na Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa kwamba, vikosi vya Iraq vimefanikiwa kupata ushindi muhimu na kuweza kuikomboa miji na maeneo ya mkoa wa al-Anbar na Nainawa na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwatimua wanachama wa kundi la kigaidi ambalo ni tishio kwa ulimwengu mzima.

Katika safari yake hiyo nchini Iraq, Jean-Yves Le Drian Waziri wa Ulinzi wea Ufaransa ametangaza himaya ya nchi yake kwa Iraq katika vita dhidi ya ugaidi.

Kundi la kigaidi la Daesh liliyateka maeneo mengi ya kaskazini na magharibi mwa Iraq mwezi Juni mwaka 2014 ambapo sanjari na kutenda jinai nyingi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo, limefanya uharibifu mkubwa katika maeneo ya kihistoria, kidini na turathi za kiutamaduni. Hata hivyo hivi sasa jeshi na vikosi vya wananchi huko Iraq vimefanikiwa kukomboa maeneo muhimu kutoka kwa kundi hilo la kigaidi na kila leo habari zinaonesha kuzidi kulemewa kundi hilo la kitakfiri.

WAMISRI WAJA JUU KWA RAIS WAO KUTOA VISIWA VIWILI KWA SAUDIA.

WAMISRI WAJA JUU KWA RAIS WAO KUTOA VISIWA VIWILI KWA SAUDIA.

Al Sisi akabiliwa na upinzani mkubwa wa Wamisri kwa hatua yake ya kuipatia Saudia visiwa viwili

Wananchi wa Misri kuanzia wale wa matabaka ya kawaida, wanaharakati hadi maafisa wa zamani na wanasiasa wameungana katika safu moja kuonyesha kukasirishwa kwao na uamuzi wa Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi hiyo wa kuipatia Saudi Arabia visiwa viwili vilivyoko katika bahari Nyekundu.

Serikali ya Misri Jumamosi wiki hii ilitangaza kuwa inaikabidhi Saudi Arabia mamlaka ya visiwa viwili vya kiistratejia kwa majina ya Tiran na Sanafir vinavyopatikana katika Ghuba ya Aqaba, baada ya Mfalme Salman wa nchi hiyo kuwasili mjini Cairo kwa ziara ya siku tano.

Tangazo hilo la kushtukiza limeamsha hasira na malalamiko ya Wamisri ambao walikuwa wakivitambua visiwa hivyo kuwa ni ardhi yao kwa miongo mingi.

Wanaharakati mbalimbali nchini Misri wametoa maoni yao wakisema kuwa Rais al Sisi anauza ardhi ya Misri kwa muitifaki tajiri kupitia mapatano ya udhalilishaji.

MLIPUKO WA BOMU UMETOKEA HUKO MOGADISHU.

MLIPUKO WA BOMU UMETOKEA HUKO MOGADISHU.

Mlipuko wa bomu umetokea leo nje ya mgahawa mmoja uliokuwa umejaa wateja wakipata chakula cha mchana huko Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo na kuuwa watu wasiopungua watano.
Mgahawa huo unaopatikana katika wilaya ya Hamarweyne, upo karibu na makao makuu ya manispaa ya serikali na katika eneo la kibiashara lenye shughuli nyingi.

Mohammed Mahdi ambaye ni mmoja wa watu walioshuhudia mlipuko huo amesema kuwa aliwaona watu wasiopungua watano wakiwa wametapakawa na damu nje ya makao makuu hiyo ya majengo ya manispaa ya serikali, huku shuhuda mwingine kwa jina la Yusuf Ali akisema kuwa mlipuko huo wa bomu la kutegwa garini ulitokea wakati eneo hilo likiwa limejaa watu wengi wakifanya manunuzi.

Kundi la kigaidi la al Shabab lenye uhusiano na mtandao wa al Qaida limekuwa likitekeleza mashambulizi makubwa dhidi ya maafisa wa serikali ya Somalia na vikosi vya kulinda amani vya kimataifa na vilevile kuzishambulia hoteli na migahawa huko Mogadishu. Nchi jirani ya Kenya pia ambayo imetuma wanajeshi wake kupambana na al Shabab huko Somalia imekumbwa na mashambulizi kadhaa kutoka kwa kundi hilo.

KWANINI NZI WANASUGUA MIKONO YAO MARA KWA MARA?

KWANINI NZI WANASUGUA MIKONO YAO MARA KWA MARA?

Ukiangalia kwa makini nzi wanaokaa jikoni, utaona wanasugua mikono yao kila wakati. Kitendo hiki ni kujisafisha.
Kujisafisha ni jambo muhimu kwa viumbe vyote wakiwemo binadamu. Lakini ni sehemu gani mwilini ina uchafu mwingi zaidi? Ni manyoya.

Idadi ya manyoya ya nyuki ni karibu sawa na kuchakuro, wote wana manyoya milioni 3 hivi. Lakini bado wana manyoya machache kuliko kipepeo. Inaonekana kwamba kipepeo hana manyoya mengi, lakini ukweli ni kwamba ana manyoya bilioni 10! Unataka kujua una nywele ngapi kichwani mwako? Ni laki moja tu.
Baada ya kuoga, mbwa anatikisa mwili wake ili kujikausha.

Kitendo chake kinafanana na mashine ya kufulia nguo inapokausha nguo. Maji ya mwilini mwake yanakabiliwa na mchapuko (Gravitational acceleration) wa 10G hadi 70G. Ndege mvumaji anapopiga mabawa yake, mchapuko ni 200G. Lakini uwezo wa ndege huyu bado mdogo kuliko mbu. Wakati mbu anapopiga mabawa yake, mchapuko unafikia 2500G! Mchapuko huo unatosha kuondoa uchafu wote katika mabawa yake.

Paka pia anajisafisha mara kwa mara. Anajiramba kwa ulimi wake wenye miimba mingi. Kujiramba si kama tu kunasaidia kuondoa vumbi, bali pia kunasaidia kuua vijidudu, kubadili joto la mwilini na kuwasiliana na paka wengine.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA USA YUKO JAPANI.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA USA YUKO JAPANI.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. John Kerry atahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 7 unaofanyika mjini Hiroshima, Japani.

Akiwa nchini humo, Bw. Kerry atatembelea bustani ya kumbukumbu ya amani ya Hiroshima, lakini hataomba radhi kutokana na kitendo cha Marekani cha kushambulia Hiroshima kwa bomu la nyuklia katika Vita ya Pili ya Dunia.

Agosti 6 mwaka 1945 jeshi la Marekani lilishambulia Hiroshima kwa bomu la nyuklia lililoitwa "Little Boy", ili kuifanya Japan iliyofanya uvamizi wakati wa vita hiyo kujisalimisha haraka. Takwimu kutoka serikali ya Japan zinaonesha kuwa, mlipuko wa bomu hilo ulisababisha watu zaidi ya laki 1.4 kufariki papo hapo.