SAUDIA INA LENGO YA KUTOHESHIMU USITISHWAJI VITA YEMEN.

SAUDIA INA LENGO YA KUTOHESHIMU USITISHWAJI VITA YEMEN.

Licha ya kutiwa saini mapatano ya usitishaji vita nchini Yemen kati ya Saudia na Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo ya Answarullah, lakini bado mashambulizi ya Saudia na waitifaki wake yangali yanaendelea.

Kabla ya hapo ilikuwa imetangazwa kuwa, usitishaji vita nchini Yemen ungeanza kutekelezwa usiku wa manane wa kuamkia Jumapili, hata hivyo habari zinaripoti kuwa usitishaji vita huo umesogezwa mbele hadi usiku wa manane wa kuamkia Jumatatu.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, mazungumzo ya amani ya Yemen huko nchini Kuwait, yatakayosimamiwa na Ismail Ould Cheikh Ahmed, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya nchi hiyo, yatafanyika tarehe 18 ya mwezi huu wa Aprili.

Licha ya kukaribia muda wa usitishaji vita nchini Yemen, lakini bado mashambulizi ya kikatili ya Saudia yameendelea kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Ndege za kivita za Saudia zimefanya mashambulizi katika mji wa Taiz, kusini mwa nchi hiyo na mikoa ya Ma'rib na Al Jawf, ambapo watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa.

Uzoefu wa siasa za Saudia kuhusu Yemen unaonyesha kwamba, usitishaji vita ndio fursa ya kufikiwa malengo ambayo watawala wa Aal-Saud kwa kutumia majeshi wameshindwa kuyafikia hadi sasa nchini humo. Hii ni katika hali ambayo makubaliano ya usitishaji vita yaliyopita yalishindwa kutekelezwa kutokana na kupenda kujitanua kwa Saudia.

Pamoja na hayo chaguo la Riyadh la kutumia nguvu ya kijeshi kwa ajili ya kufikia malengo yake ya mwi

WANANCHI NA WANAJESHI WAONYESHANA UBAVU MASHARIKI YA DRC

WANANCHI NA WANAJESHI WAONYESHANA UBAVU MASHARIKI YA DRC

Habari kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema kuwa, kumezuka machafuko baina ya wananchi na wanajeshi wa serikali baada ya kuuawa kiongozi mmoja wa kieneo katika eneo hilo.

Machafuko hayo yameripotiwa kutokea katika eneo la Nyamilima katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Machafuko hayo yaliyoanza siku ya Jumamosi yameripotiwa kuendelea hadi leo (Jumatatu).

Machafuko hayo yamezuka baada ya kuuliwa kiongozi wa jamii ya Wahutu katika eneo la Binza, moja ya maeneo ya mji wa Nyamilima.

Ingawa hadi hivi sasa watu waliomuua kiongozi huyo wa Wahutu hajajulikana, lakini wananchi wa eneo hilo wanailaumu serikali kwa kushindwa kuwalinda.

Baadhi ya duru za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimedai kuwa, waasi wa Mai Mai ndio waliofanya mauaji hayo.

Wakazi wa eneo la Binza walimpiga vikali mwanajeshi mmoja wa serikali siku ya Jumamosi, mara baada ya mwanajeshi huyo kuingia eneo hilo. Mwanajeshi huyo aliyelazimika kujitetea mbele ya wakazi wenye hasira, alilazimika kuwafyatulia risasi watu hao na kuwajeruhi watu wawili wakati alipokuwa anakimbilia usalama wake.

Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limezama kwenye machafuko na mapigano kwa muda wa miaka 20 sasa.

RAIS WA IRANI ASISITIZA MASHIRIKIANO KATIKA KUPAMBANA NA MAKUNDI YA KIGAIDI.

RAIS WA IRANI ASISITIZA MASHIRIKIANO KATIKA KUPAMBANA NA MAKUNDI YA KIGAIDI.

Rais Hassan Rouhani wa Iran kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za pamoja kukabiliana na makundi ya kigaidi.

Rais Rouhani amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina wasiwasi kutokana na machafuko yanayoenezwa na magaidi katika baadhi ya nchi barani Afrika na nchi kadhaa Mashariki ya Kati.

Akizungumza mjini Tehran katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Estonia Marina Kaljurand, Rais Rouhani amesema, jitihada za kurejesha utulivu na usalama katika nchi zinazolengwa na ugaidi ni jambo litakalochangia kuimarisha usalama kote duniani.

Kwingineko katika kikao hicho, Rais Rouhani amesema Iran inakaribisha kuimarisha uhusiano na Umoja wa Ulaya na kusema pande mbili zinaweza kushauriania kuhusu kudumisha utulivu na usalama duniani.

Kwa upande wake, Marina Kaljurand Waziri wa Mambo ya Nje wa Estonia amesema, Iran ina nafasi muhimu kieneo na kimataifa na kwamba nchi yake ina hamu kuimarisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu katika sekta mbali mbali.

ZOEZI LA USITISHWAJI VITA YEMEN LIMEANZA RASMI.

ZOEZI LA USITISHWAJI VITA YEMEN LIMEANZA RASMI.

Usitishwaji vita unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa Yemen ulianza jana usiku (Jumapili) kabla ya kuanza mazungumzo ya amani baina ya pande hasimu nchini Kuwait. Usitishwaji mapigano huo ulitarajiwa kuanza saa sita usiku Jumapili kwa majira ya Yemen (2100 GMT).

Katika hatua ya awali usitishwaji vita huo utaanza katika mikoa yenye mapigano makali ya Ta’iz na Hajjah. Hayo yanajiri katika hali ambayo ndege za kivita za Saudia jana Jumapili ziliendelea kudondosha mabomu katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Sana’aa.

Usitishwaji vita umetangazwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed kama njia ya kutuliza hali ya mambo kabla ya mazungumzo ya amani yanayoanza tarehe 18 Aprili nchini Kuwait.

Hadi hivi sasa watu wasiopungua 9,400 wameshauawa na wengine zaidi ya 16,000 wamejeruhiwa tangu Saudia na washirika wake walipoanzisha mashambulio na uvamizi wa kijeshi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuisambaratisha Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wa utawala wa Aal Saud,

Rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi. Mashambulio hayo yameshindwa kufikia malengo hayo zaidi ya kuangamiza na kusababisha hasara kubwa kwa miundombinu ya Yemen, mbali na kulenga na kubomoa hospitali, shule, misikiti na turathi za kihistoria za nchi hiyo.

PENZI JINI HATARI.

PENZI JINI HATARI.
1
Penzi ni jini hatari, wa kutesa na kuua,
Huzibeba zote shari, za kiangazi na mvua,
Nina kuomba Qahari, miye asije niua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
2
Penzi mganga mzuri, huponya wanougua,
Hukusanya nyingi heri, za mwezi hata za jua,
Kwa idhini Ya Jabari, aponye changu kifua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
3
Mapenzi istiimari, hakika nimetambua
Baridi naona hari, meli mwenzenu mashua,
Asali kwangu shubiri, ninajuta kuyajua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
4
Mapenzi ni zingifuri, kwa mja anayejua,
Narauka Alfajiri, naswali naomba dua,
Yarabi penzi la siri, lisije kuniumbua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
5
Penzi si kama johari, huwezi kulinunua,
Si mchanga wa bahari, bure ukalichukua,
Thamaniye si mahari, mkaja hata jazua.
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
6
Penzi halina jabari, si chuma la kuinua,
Uwe bondia hodari, pia laweza sumbua,
Huba zataka sukari, moyo upate kutua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
7
Mapenzi jua qadari, uwaze na kuwazua
Alo lipanga Ghafuri, hakuna wa kupangua,
Hivyo hatuna hiyari, hata kama twaamua
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
8
Mapenzi si kibatari, ni mshumaa tambua,
Nyonda apate fahari, mwenyewe unaungua,
Yengekuwa samsuri, wallahi ningeyavua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394

WANAJESHI WATANZANIA DRC WATUHUMIWA KWA UBAKAJI.


Wanajeshi wa Tanzania walioko katika kikosi cha Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika na ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi habari kuwa tayari kuna kesi 11 za madai ya ubakaji yaliyowasilishwa dhidi ya askari wa Tanzania walioko DRC na hata wale ambao waliwahi kuhudumu nchini humo. Ameongeza kuwa kamanda wa batalioni ya Tanzania amewaweka kizuizini wanajeshi wanaokabiliwa na tuhuma hizo huku uchunguzi ukiendelea.

Umoja wa Mataifa haujataja majina wa askari wanaotuhumiwa lakini imebainika kuwa wote wako au waliwahi kuwa katika kikosi cha umoja huo nchini DRC. Askari wa Tanzania DRC wanakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika vitendo vya ngono na watoto na pia kutoa vishawishi kadhaa ili kupata ngono. Dujarric amesema kuna kesi nne za wanajeshi wa sasa kushikisha mimba na kesi zilizosalia ni za askari Watanzania waliowahi kuhudumu DRC.

Vitendo hivyo vyote vimeripotiwa katika kijiji cha Mavivi mashariki mwa DRC karibu na Beni. Umoja wa Mataifa unachunguza vitendo hivyo vya ubakaji na udhalilishaji kijinsia. Wakuu wa Tanzania wamefahamishwa kuhusu kashfa hiyo lakini hawajaeleza iwapo watatuma wachunguzi wao DRC au la. Askari wa Umoja wa Mataifa kote duniani wamekumbwa na kashfa za ubakaji na ngono, na mwaka 2015 kulikuwa na kesi 69 zilizoripotiwa.

KENYATA AZURU UFARANSA NA UJERUMANI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameanza leo ziara nchini Ufaransa na Ujerumani.
Agenda kuu kwenye ziara hiyo ni kuhusu usalama, biashara na uwekezaji.
Akiwa nchini Ufaransa atafanya mazungumzo na mwezake Francois Hollande.

Ufaransa ndio mwekezaji wa sita nchini Kenya ambayo pia inapokea misaada mikubwa zaidi ya kigeni kutoka Ufanransa.

Baada ya ziara ya Ufaransa Uhuru Kenyatta atafanya ziara ya siku mbili nchini Ujerumani ambako amealikwa na Chancellor Angela Merkel.

Kwa sasa Ujerumani ndio soko kuu la pili la watalii kwa Kenya baada ya Uingereza, na mauzo ya bidhaa za Kenya nchini humo yameongezeka hadi dola bilioni 11 mwaka 2014/

Kuna zaidi ya kampuni 90 za Ujerumani nchini Kenya ambazo zimewekeza dola milioni 120 na kutoa ajira kwa zaidi ya watu 4,200.

UN YAPINGA MAONESHO YA ISRAELI

Umoja wa Mataifa umepinga maonyesho ya picha za kipropaganda za utawala wa Kizayuni wa Israel katika makao makuu ya umoja huo mjini New York.

Imedokezwa kuwa maonyesho hayo ya Israel yalikuwa yafanyike leo Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo utawala wa Tel Aviv ulikuwa umepanga kuonyesha picha za kutetea sera zake za kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Balozi wa utawala haramu wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon amekasirishwa sana na hatua ya kupigwa marufuku maonyesho hayo na kusema jambo hilo linahatarisha uwepo wa Israel.

Utawala wa Kizayuni ulipanga kuonyesha picha ambazo zingearifisha mji wa Quds eti kuwa ni mji mkuu wa Israel. Wapalestina wanasisitiza kuwa Quds ni mji mkuu wa dola huru la Palestina.

Kwingineko Harakati ya Kimatiafa ya Kususia Israel BDS imeitaja kuwa ni ushindi mkubwa hatua ya kupigwa marufuku uonyeshaji wa filamu ya Kizayuni ya 'Mwili wa Tatu' katika maonyesho ya filamu za haki za binadmau huko Seoul Korea Kusini.

ASKARI WA UFARANSA WAONGOZA KWA JINAI YA KIJINSIA AFRIKA.

Iwapo tuhuma mpya za ukandamizaji wa kijinsia zilizotolewa dhidi ya askari wa Ufaransa barani Afrika zitathibitishwa, basi sura ya mkoloni huo mkongwe barani humo itazidi kuchafuka.

Katika radiamali yake juu ya tuhuma mpya zinazohusu ukatili na jinai za kijinsia za askari wa nchi hiyo, hivi karibuni Rais François Hollande wa Ufaransa alisema kuwa, ikiwa tuhuma hizo za utovu wa kimaadili zitathibitishwa dhidi ya askari wa nchi yake, basi suala hilo litachafua sura ya Ufaransa kimataifa.

Rais wa Ufaransa ameashiria pia mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na kusema kuwa anataraji pande mbili hizo zitashirikiana ili kubaini ukweli, kutekeleza uadilifu na kuadhibiwa askari wote watakaobainika kutenda jinai hizo ili uwe mfano kwa wengine, ikiwa tuhuma hizo zitathibitishwa. Aidha alisisitiza kuwa, ni jambo lisilokubalika kuachwa jambo hilo bila ya kuchukuliwa hatua kali wahusika wake.

Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imetangaza kuwa, punde tu baada ya kutolewa ripoti ya kamishna mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kashfa mpya za utovu wa maadili zinazowakabili askari wa Ufaransa barani Afrika, wizara hiyo iliwakabidhi askari hao kwa vyombo vyake vya sheria.

Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo karibu kila siku kumekuwa kukiripotiwa kashfa mpya za ukatili wa kijinsia katika jeshi hilo la Ufaransa nje ya nchi hiyo. Askari wa kulinda amani wa nchi hiyo wamekuwa wakiwabaka na kuwanyanyasa kijinsia watoto wadogo na wanawake waliokimbilia katika kambi za wakimbizi ili kuokoa maisha yao kwa kuwahadaa kwa biskuti au fedha kiduchu kabla ya kufanya ufuska wao.

Hata hivyo jambo la kusitikitisha zaidi ni kwamba, jinai hizo zimeendelea kufumbiwa macho huku wahusika wake wakiwa hawachukuliwi hatua zozote za maana za kiesheria. Siku chache zilizopita pia, askari mmoja wa Ufaransa alipatikana na hatia za kuwanajisi watoto wa wanne wa kike walio chini ya umri wa miaka 12 huko Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kuwahadaa kwa pesa kiduchu. Kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu, baada ya askari huyo kumaliza kufanya jinai hiyo, aliwalazimisha watoto hao kutembea kingono na mbwa wake kitendo ambacho kimepelekea binti mmoja kufariki dunia kutokana na maradhi aliyoambukizwa na mnyama huyo. Itafahamika kuwa, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wako katika nchi nyingi duniani hususan barani Afrika.

Lengo la kutumwa askari hao katika maeneo yenye migogoro na mapigano ya ndani au ya nje, ni kulinda raia na kurejesha usalama. Hata hivyo kuna kashfa za mara kwa mara zinaripotiwa zikifanywa na askari hao. Licha ya kuweko ripoti za jinai za kijinsia na nyenginezo kama hizo, lakini unyanyasaji huo bado unaendelea.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2013, askari 14 wa Ufaransa walikumbwa na kashfa ya ukatili wa kijinsia, na tangu wakati huo kesi za namna hiyo zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara. Hivi karibuni Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alinukuliwa akisema: "Tunao askari wa jamii ya kimataifa ambao wamepelekwa maeneo tofauti kwa ajili ya kuwalinda watu, hata hivyo na kwa bahati mbaya askari hao wanaamiliana na watu hao kwa ukatili, jinai ambazo kwa bahati mbaya zimekuwa zikinyamanziwa kimya."

Kwa upande wake Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mbali na kulaani jinai hizo, amekuwa akihimiza kuchukuliwa hatua kali dhidi ya wahusika wa jinai hizo ingawa hata hivi hadi leo hakuna hatua za maana zilizochukuliwa kutokana na uzembe unaoonekana ni wa makusudi wa kukwepa kutekeleza amri hiyo.