SERIKALI YA NIGERIA IMEMKAMATA KAMANDA WA BOKO HARAM.

SERIKALI YA NIGERIA IMEMKAMATA KAMANDA WA BOKO HARAM.

Serikali ya Nigeria imesema kuwa imekamata kamanda wa kundi la kigaidi la Boko Haram ambaye anashukiwa kuongoza shambulizi la bomu katika jengo la umoja wa mataifa (UN) mjini Abuja mnamo Agosti 26, 2011.

Kwa mujibu wa taarifa uliotolewa na msemaji wa wizara ya usalama wa ndani,Tony Opuiyo, mshukiwa huyo kwa jina Mohammed Usman au Khalid Al-Barnawi kwa jina lingine, alitiwa mbaroni mjini Lokoja katika jimbo la Kogi nchini humo. Opuiyo alisema kuwa kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua muhimu katika vita dhidi ya ugaidi.

Kulingana na Opuiyo, Al-Barnawi amekuwa akiongoza mashambulizi ya kigaidi nchini Nigeria na kupeleka vijana kwa mafunzo ya kigaidi mashariki ya kati na Afrika kaskazini.

AU YASEMA UCHAGUZI WA DJIBOUTI ULIKUWA HURU NA HAKI.

AU YASEMA UCHAGUZI WA DJIBOUTI ULIKUWA HURU NA HAKI.

Licha ya lalama kutoka vyama vya upinzani, lakini Umoja wa Afrika AU umesema uchaguzi mkuu wa Djibouti wa Ijumaa iliyopita ulikuwa huru na wa haki.
Mkuu wa timu ya waangalizi wa AU katika uchaguzi huo, Soumana Sako amesema licha ya uchaguzi huo kukabiliwa na kasoro za hapa na pale, lakini ulikuwa huru na wa haki. Amesema vyombo husika vilionyesha uwazi wa hali ya juu, jambo ambalo linaufanya uchaguzi huo kuhesabiwa kuwa huru.

Viongozi wa upinzani nchini Djibouti wametangaza kutotambua ushindi wa Rais Ismail Omar Guelleh katika uchaguzi mkuu uliofanyika Ijumaa iliyopita. Muhammed Tourtour, mmoja wa wagombea watano wa upinzani katika uchaguzi huo ametaja kama kichekesho na ndoto tangazo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kwamba Rais Guelleh alishinda kiti hicho kwa asilimia 86 na kusisitiza kuwa, uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu na kasoro nyingi.

Licha ya vyama vingi vya upinzani kususia uchaguzi huo, lakini Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi imesema kuwa asilimia 68 ya watu laki 1 na 87 elfu waliotimiza masharti ya kupiga kura walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo, madai ambayo upinzani unasema kuwa hayaingii akilini. Rais Guelleh mwenye umri wa miaka 68, amekuwa madarakani tokea mwaka 1999.

Djibouti ambayo ni nchi ndogo ya Pembe ya Afrika yenye idadi ya watu wasiofikia hata milioni moja, mwaka 2011 ilishuhudia wimbi la maandamano ya kupinga kuchaguliwa tena Rais Guelleh ambaye ilisemakana kuwa alipata asilimia 80 ya kura zilizopigwa.

Maandamano hayo yalijiri baada ya Rais Guelleh kuifanyia marekebisho katiba ya nchi, ili kumruhusu kugombea kiti hicho kwa mara ya tatu mfululizo.

DUBAI KUJENGA JENGO LINGINE REFU ZAIDI YA BURJ KHALIFA.

DUBAI KUJENGA JENGO LINGINE REFU ZAIDI YA BURJ KHALIFA.

Kampuni ya Dubai Emaar Properties inapanga kujenga jengo refu zaidi duniani ambalo litavunja rekodi ya sasa ya jengo la Burj Khalifa.

Wenzetu wanawekeza zaidi katika utalii wa majengo makubwa kama hayo. Sisi utalii wetu kwenye kutumbua majipu, Mchina anatoka China kuja kushangaa Magufuli na mikasi yake.

Hata hivyo mwanakisima una maoni gani juu ya ujengaji wa jengo hilo, hiv mnara wa Babeli ulikuwa na urefu gani?

WATOTO 700 WAKAA CHINI SHULE MOJA RORYA.

WATOTO 700 WAKAA CHINI SHULE MOJA RORYA.

Wakizungumza shuleni hapo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Magesa Mulongo wanafunzi hao wamesema wanakaa chini kutokana na ukosefu wa madawati shuleni hapo jambo linalowakwamisha katika maendeleo ya kitaaluma.

Kwa upande wake mmoja wa walimu shuleni hapo mwalimu Marco Lucas amesema shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa miondombinu ikiwemo ukosefu wa nyumba ya walimu ambapo wao wanakaa mbali sana na shule jambo linalowapunguzia pia morali ya kazi.

Kutokana na upungufu huo wazazi wa wanafunzi hao wamesema hawatachangia maendeleo ya shule hiyo kwa kuwa michango waliyochanga awali ililiwa bila madawati kutengenezwa.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Mara Magesa Mulongo ameagiza wakurugenzi wa elimu kuhakikisha wanafanya ukaguzi katika shule na kubaini changamoto zilizopo ili ziweze kushughulikiwa kwa wakati huku Mkuu wa Wilaya ya Rorya Felix Lyaniva akisisitiza upatikanaji wa madawati kabla ya mwezi Juni kama alivyoagiza Rais Dkt. John Magufuli.

ABU SAYYAF WAUA WANAJESHI 18 UFILIPINO.

ABU SAYYAF WAUA WANAJESHI 18 UFILIPINO.

Jeshi la Ufilipino limekiri kuwa wanajeshi 18 wameuawa katika makabiliano makali na wapiganaji waasi wa Abu Sayyaf Kusini mwa taifa hilo.

Limeongeza kuwa wanajeshi wengine 50 walijeruhiwa wakati wa makabiliano katika kisiwa cha Basilan. Wapiganaji watano wa kundi hilo la Waislamu wenye itikadi kali waliuawa.

Inasemekana wanajeshi wa Ufilipino walikuwa wakimlenga kamanda wa Abu Sayyaf Isinilon Hapilon, ambaye ameapa uaminifu wake kwa kundi la Islamic State.

Kundi la Abu Sayyaf limetekeleza ulipuaji wa mabomu, utekaji nyara na kuwakata watu vichwa Kusini mwa Ufilipino.
Serikali ya Marekani imetangaza zawadi ya dola milioni 5 kwa habari zozote zitakazosaidia kumtia mbaroni Hapilon.

KUHOFIA MASHAMBULIZ YA DAESH, VISIMA VYA MAFUTA VYAFUNGWA LIBYA.

KUHOFIA MASHAMBULIZ YA DAESH, VISIMA VYA MAFUTA VYAFUNGWA LIBYA.

Maafisa usalama wa Libya wanaolinda visima vya mafuta nchini humo wamelazimika kufunga visima vitatu vya mafuta kutokana na wafanyakazi katika visima hivyo kugoma kwenda kazini kwa kuhofia mashambulio ya genge la kigaidi la Daesh.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kutoka mjini Benghazi kuwa, hivi sasa kumeenea wasiwasi nchini Libya kuwa, kundi la kigaidi la Daesh litadhibiti visima vya mafuta vya nchi hiyo na kusababisha hasara kubwa za mali na roho kwa wananchi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Hii ni katika hali ambayo katika miezi ya hivi karibuni, kundi la kigaidi la Daesh limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara katika visima vya mafuta vya nchi hiyo, ingawa limeshindwa hadi hivi sasa kudhibiti maeneo hayo.

Uzalishaji wa mafuta nchini Libya umepungua mno hivi sasa. Kiwango hicho ni cha chini ya khumusi moja ya kiwango kilichokuwa kikizalishwa nchini humo mwaka 2011, kabla ya kuanza kampeni ya kumg'oa madarakani Kanali Muammar Ghaddafi.

Hadi mwaka 2011, Libya ilikuwa inazalishaji mapipa milioni moja na laki sita kwa siku.

SAUDIA INA LENGO YA KUTOHESHIMU USITISHWAJI VITA YEMEN.

SAUDIA INA LENGO YA KUTOHESHIMU USITISHWAJI VITA YEMEN.

Licha ya kutiwa saini mapatano ya usitishaji vita nchini Yemen kati ya Saudia na Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo ya Answarullah, lakini bado mashambulizi ya Saudia na waitifaki wake yangali yanaendelea.

Kabla ya hapo ilikuwa imetangazwa kuwa, usitishaji vita nchini Yemen ungeanza kutekelezwa usiku wa manane wa kuamkia Jumapili, hata hivyo habari zinaripoti kuwa usitishaji vita huo umesogezwa mbele hadi usiku wa manane wa kuamkia Jumatatu.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, mazungumzo ya amani ya Yemen huko nchini Kuwait, yatakayosimamiwa na Ismail Ould Cheikh Ahmed, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya nchi hiyo, yatafanyika tarehe 18 ya mwezi huu wa Aprili.

Licha ya kukaribia muda wa usitishaji vita nchini Yemen, lakini bado mashambulizi ya kikatili ya Saudia yameendelea kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Ndege za kivita za Saudia zimefanya mashambulizi katika mji wa Taiz, kusini mwa nchi hiyo na mikoa ya Ma'rib na Al Jawf, ambapo watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa.

Uzoefu wa siasa za Saudia kuhusu Yemen unaonyesha kwamba, usitishaji vita ndio fursa ya kufikiwa malengo ambayo watawala wa Aal-Saud kwa kutumia majeshi wameshindwa kuyafikia hadi sasa nchini humo. Hii ni katika hali ambayo makubaliano ya usitishaji vita yaliyopita yalishindwa kutekelezwa kutokana na kupenda kujitanua kwa Saudia.

Pamoja na hayo chaguo la Riyadh la kutumia nguvu ya kijeshi kwa ajili ya kufikia malengo yake ya mwi

WANANCHI NA WANAJESHI WAONYESHANA UBAVU MASHARIKI YA DRC

WANANCHI NA WANAJESHI WAONYESHANA UBAVU MASHARIKI YA DRC

Habari kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinasema kuwa, kumezuka machafuko baina ya wananchi na wanajeshi wa serikali baada ya kuuawa kiongozi mmoja wa kieneo katika eneo hilo.

Machafuko hayo yameripotiwa kutokea katika eneo la Nyamilima katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Machafuko hayo yaliyoanza siku ya Jumamosi yameripotiwa kuendelea hadi leo (Jumatatu).

Machafuko hayo yamezuka baada ya kuuliwa kiongozi wa jamii ya Wahutu katika eneo la Binza, moja ya maeneo ya mji wa Nyamilima.

Ingawa hadi hivi sasa watu waliomuua kiongozi huyo wa Wahutu hajajulikana, lakini wananchi wa eneo hilo wanailaumu serikali kwa kushindwa kuwalinda.

Baadhi ya duru za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimedai kuwa, waasi wa Mai Mai ndio waliofanya mauaji hayo.

Wakazi wa eneo la Binza walimpiga vikali mwanajeshi mmoja wa serikali siku ya Jumamosi, mara baada ya mwanajeshi huyo kuingia eneo hilo. Mwanajeshi huyo aliyelazimika kujitetea mbele ya wakazi wenye hasira, alilazimika kuwafyatulia risasi watu hao na kuwajeruhi watu wawili wakati alipokuwa anakimbilia usalama wake.

Eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limezama kwenye machafuko na mapigano kwa muda wa miaka 20 sasa.

RAIS WA IRANI ASISITIZA MASHIRIKIANO KATIKA KUPAMBANA NA MAKUNDI YA KIGAIDI.

RAIS WA IRANI ASISITIZA MASHIRIKIANO KATIKA KUPAMBANA NA MAKUNDI YA KIGAIDI.

Rais Hassan Rouhani wa Iran kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za pamoja kukabiliana na makundi ya kigaidi.

Rais Rouhani amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina wasiwasi kutokana na machafuko yanayoenezwa na magaidi katika baadhi ya nchi barani Afrika na nchi kadhaa Mashariki ya Kati.

Akizungumza mjini Tehran katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Estonia Marina Kaljurand, Rais Rouhani amesema, jitihada za kurejesha utulivu na usalama katika nchi zinazolengwa na ugaidi ni jambo litakalochangia kuimarisha usalama kote duniani.

Kwingineko katika kikao hicho, Rais Rouhani amesema Iran inakaribisha kuimarisha uhusiano na Umoja wa Ulaya na kusema pande mbili zinaweza kushauriania kuhusu kudumisha utulivu na usalama duniani.

Kwa upande wake, Marina Kaljurand Waziri wa Mambo ya Nje wa Estonia amesema, Iran ina nafasi muhimu kieneo na kimataifa na kwamba nchi yake ina hamu kuimarisha uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu katika sekta mbali mbali.