IKHWANUL YAENDELEZA MAPAMBANO YA AMANI HUKO MISRI.

Kaimu Kiongozi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri amesema kuwa harakati hiyo itaendelea kufanya maandamano na kuwasilisha malalamiko yake kwa njia ya amani.

Mahmoud Izzat ambaye amechukua nafasi ya Mohammed Badie kiongozi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin jana Jumapili alitoa taarifa na kubainisha kuwa Ikhwanul Muslimin itaendeleza mapambano yake na kuwasilisha malalamiko yake kwa njia ya amani hadi pale itakapofanikisha matakwa yake.

Mahmoud Izzat amesema kuwa Harakati ya Ikhwanul Muslimin itaendeleza mapambano hadi pale uhuru na izza vitakaporejea huko Misri humo, kwa kufuata misingi ya mwasisi wa kundi hilo Hassan al Bana.

Ni zaidi ya miaka miwili sasa ambapo Mohammed Badie Kiongozi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimi anashikiliwa korokoroni akituhumiwa kwa makosa mbalimbali na hadi kufiikia sasa amekatiwa hukumu mbili, moja ikiwa ni ya kunyongwa na nyingine ya kifungo cha maisha jela. Rais wa sasa wa Misri Abdel Fattah al Sisi amekuwa akitekeleza siasa za kuwakandamiza wapinzani nchini humo tangu aingie madarakani baada ya rais halali wa nchi hiyo aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Muhammad Morsi kupinduliwa na jeshi mwaka 2013. Maelfu ya wapinzani na wanachama wa ngazi za juu wa Ikhwanul Muslimi wametiwa mbaroni huko Misri na mamia ya wengine kuuliwa.

IRAN INA HIFADHI YA MAFUTA MAPIPA BIL 100 KATIKA GHUBA YA UAJEMI.

Hifadhi ya mafuta ghafi ya petroli ya Iran katika Ghuba ya Uajemi imefikia mapipa bilioni 100.

Hayo yamedokezwa na Saeid Hafezi Mkurugenzi wa Shirika la Kuchimba Mafuta Baharini la Iran (IOOC) ambaye amebainisha kuhusu utajiri mkubwa wa Iran wa gesi asilia na mafuta ya petroli katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

Hafezi amesema hivi sasa mafuta ambayo yanaweza kuchimbwa katika eneo hilo ni mapipa bilioni 16 na kuongeza kuwa, hivi sasa Iran inatafuta teknolojia mpya na ya kisasa zaidi ili iweze kuchimba mafuta hayo kutoka baharini.

Aidha amesema Iran ina hifadhi ya mita mraba bilioni 187 za gesi asilia katika Ghuba ya Uajemi. Amesema Iran hivi sasa ina uwezo wa kuchimba asilimia 75 ya gesi hiyo.

WAWILI WAFA KWA KUANGUKIWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO GEITA.

Watu wawili wameaga dunia baada ya kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo haramu ya dhahabu hapo juzi huko katika mkoa wa Geita.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya alasiri juzi Jumamosi, wakati watu watano walipokuwa ndani ya machimbo hayo yanayopatikana katika kijiji cha Busaka katika wilaya ya Chato. Kamanda Mwabulambo ameongeza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya kanda ya ziwa yamedhoofisha kuta za machimbo hayo ya madini na hivyo kusababisha kuporomoka.

Shaaban Ntarambe Mkuu wa wilaya ya Chato ametangaza kufungwa eneo la machimbo hayo. Itafahamika kuwa Geita ni kitovu cha uchimbaji wa madini ya dhahabu nchini Tanzania.

MTANZANIA ANYONGWA NA AL SHABABI.

Raia wa Tanzania aliyejiunga na kundi la al Shabaab la nchini Somalia amenyongwa na kundi hilo kwa tuhuma za ujasusi.

Mtandao wa habari wa Hiiraan Online umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, hukumu ya kifo dhidi ya Issa Jemes Mwesiga (27) raia wa Tanzania aliyejiunga na kundi la sh Shabaab mwaka 2013 ilitekelezwa na kundi hilo siku ya Jumamosi katika mji wa Jilib, katika mkoa wa Jubba Kati yapata kilomita 400 kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu baada ya mahakama ya kundi hilo kumpata na hatia ya kuifanyia ujasusi Marekani.

Kwa mujibu wa mtandao huo, jaji wa mahakama hiyo alisoma hukumu hiyo mbele ya kadamnasi ya watu kabla ya kutekelezwa adhabu hiyo ya kifo katika uwanja ulio wazi.

Jaji huyo alidai kwenye hukumu yake kwamba, mtuhumiwa amekiri makosa na hivyo amehukumiwa adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi.

Hadi tunapokea habari hii, serikali ya Tanzania haikuwa imesema chochote kuhusiana na habari hiyo.

MISS TANZANIA WA KWANZA 1967

Theresa Shayo Miss Tanzania wa kwanza, alitwaa taji hilo mwaka 1967 katika fainali zilizofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro. Alifariki mwaka 2007 nchini Ujerumani

XI JINPING:MAKUBALIANO YA KIMATAIFA YAHITAJI HAKI NA USAWA.

Rais Xi Jinping wa China amesema usawa na haki ni msingi wa makubaliano yoyote ya kimataifa.
Rais Xi amesema hayo alipohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi 6 kuhusu suala la nyuklia la Iran mjini Washington.
Rais Xi amesema, utatuzi wa suala la nyuklia la Iran umetoa funzo kubwa, kuwa makubaliano yoyote ya kimataifa yanatakiwa kufikiwa kwenye msingi wa haki na usawa, ambapo ufuatiliaji wa haki ya kila nchi unatakiwa kuzingatiwa.

Amesisitiza kuwa, mazungumzo ni njia yenye ufanisi zaidi ya kutatua masuala makubwa, ambapo nia ya kisiasa inahitajika huku ikisaidiwa na uratibu na ushirikiano kati ya nchi kubwa duniani.

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!

JINSI WANAFUNZI WA YESU WALIVYOKUFA.!

1. #Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga huko Uhabeshi (Ethiopia ya leo) baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya kanisa la Kristo. Alijeruhiwa kwa upanga na kidonda chake hakikupona hadi umauti ulipomfika.

2. #Marko
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwa na farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishowe akafariki.

3. #Luka
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana na msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya Kristo.

4. #Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, (Italia ya sasa). Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na  alitolewa akiwa mzima kabisa.

Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama Askofu huko Edessa (Uturuki ya sasa). Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. #Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisulubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusulubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba wenye nembo ya "X". Petro mwenyewe aliomba asulubiwa kwa namna hii kwani hakutaka kusulubiwa kama Yesu (Yohana 21:18).

6.#Yakobo
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga Kristo. Mnara huo ni ule ambao Shetani aliutumia kumjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe.  Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. #Yakobo (mwana wa Zebedayo)
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa Yakobo alichinjwa huko Jerusalemu kwa kukatwa kichwa kwa amri ya Herode (Matendo 12:2).

8. #Batholomayo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Armeni (Asia ya sasa). Alimshuhudia Yesu Kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa kwa kupigwa fimbo baada ya kugoma kuacha mafundisho yake dhidi ya Kristo.

9. #Andrea
Aliuawa kama Petro huko Ugiriki kwa kusulubiwa kwenye msalaba wenye umbo la "X" miguu juu kichwa chini sawa na Petro Petro. Ila baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua. Akiwa msalabani aliwaambia wafuasi wake "nilikua naisubiri saa kama hii"

10. #Tomaso
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko Chennai (India ya sasa) katika moja ya safari zake kama Mmisionari kwenda kuanzisha Kanisa huko.

11. #Yuda (Thadei)
Aliuawa kwa kupigwa na mshale ubavuni.

12. #Yuda (Iskariote)
Huyu alijiua kwa kujinyonga baada ya kumuuza Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

NOTE:
13. #Thadayo (au Mathia) ni Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda Iskariote (msaliti). Huyu alipigwa na mawe  hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

14. #Paulo
Hakuwa mmoja wa wale wanafunzi 12 wa Yesu. Lakini huhesabika kuwa mfuasi wa Kristo na mtetezi wa mwanzo wa Kanisa. Huyu aliteswa na baadaye akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka (A.D).

Kabla ya kuchinjwa Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua (nyaraka) nyingi kwa makanisa mbalimbali. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

NB: Si muhimu kujua ni namna gani mitume walikufa, ila ni muhimu kujua kuwa mitume wote walikufa wakitetea imani yao. Walikua tayari kuchukiwa na kufa vifo vya mateso kwa ajili ya kumtetea na kumshuhudia Kristo.

Biblia imesema, "Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:23

Nakutakia pasaka njema.!

Malisa Godlisten GJ.!

WAJUE MAADUI WA NYOKA.

WAJUE MAADUI WA NYOKA.

Nyoka wenye sumu ni hatari sana, lakini wao pia wana maadui. Maadui zao ni pamoja na karani tamba, tai wanaokula nyoka (crested serpent eagle), vicheche na mamba. Baadhi ya nyoka wanakula nyoka, kwa mfano King Cobra anaweza kumla cobra. Hivyo nyoka wenye sumu wanahitaji kuchukua hatua mbalimbali Ili kujilinda katika mazingira yenye maadui wengi.

Hatua ya kwanza ni kujifanya aonekane kuwa mkubwa na hatari. Nyoka aina ya Death Adder wanaoishi huko Australia ni moja kati ya nyoka wenye sumu kali zaidi duniani, Lakini hawawezi kushinda tai wanaokula nyoka. Death Adder akikutana na tai, anatulia, kupanusha mwili wake ili ionekane kama tai hataweza kumeza. Kama tai hana maarifa ya kutosha, atamwacha na kuondoka.

Hatua ya Pili ni kujificha. Nyoka aina ya Western diamondback rattlesnake anaweza kujificha vizuri. Kutokana na madoa ya rangi ya kijivu kwenye ngozi yake, anaonekana kama changarawe. Kwa nyoka huyu anayetembea polepole, anaweza kupumzika bila ya kugunduliwa na maadui.

Hatua ya tatu ni kutoa onyo.
Nyoka aina ya rattlesnake anaweza kupiga kelele kwa kutikisika mkia wake ili kuwaonya wanyama wengine wasiingie eneo lake. Na nyoka aina ya Gaboon viper anatoa mlio wa ‘sss’ ili kutoa onyo.

SHIRIKA LA KIJASUSI LA ISRAELI HUMTUMIA MWANAMKE KAMA SILAHA.

SHIRIKA LA KIJASUSI LA ISRAELI HUMTUMIA MWANAMKE KAMA SILAHA.

Mtandao wa Intaneti wa "Sauti ya Israel" umefichua kuwa, silaha ya hatari zaidi inayotumiwa na shirika la kijasusi la utawala wa Kizayuni MOSSAD ni mwili wa mwanamke wa Kiyahudi.

Televisheni ya al Alam imeunukuu mtandao wa habari wa Alsumaria News ukiripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mwili wa mwanamke wa Kiisraeli unahesabiwa kuwa moja ya silaha muhimu sana za kufanikishia malengo ya MOSSAD kiasi kwamba watu wenye ushawishi ndani ya utawala wa Kizayuni wanawashawishi wanawake wa Kiyahudi kutofungwa na maadili yoyote yale na wapewe uhuru kamili wa kutumia wanavyotaka miili yao kwa ajili ya utawala wa Kizayuni.

Mtandao huo umemnukuu kuhani mmoja wa Kiyahudi akisema: Ingawa jamii yetu imeshikamana na dini, lakini tuna wajibu wa kuwashawishi wanawake wa Kiyahudi kujichanganya na watu wa jamii nyingine ili kuenea ukafiri na ufisadi na kudhoofisha misingi muhimu ya jamii hizo, ili iwe rahisi kuzidhibiti.

Mtandao huo umeongeza kuwa, mwanamke wa Kiisraeli anahesabiwa kuwa nguzo moja muhimu sana ya Shirika la Kijasusi la Israel, MOSSAD na wanahesabiwa kuwa ni silaha ya nne muhimu zaidi ya utawala wa Kizayuni baada ya jeshi la majini, jeshi la anga na jeshi la nchi kavu la Israel.

Mtandao huo wa Intaneti umeongeza kuwa, kila mwaka maelfu ya wanawake wa Kiyahudi wanajiunga na MOSSAD na moja ya kazi zao kubwa ni kuuza miili yao, kuua na maovu mengineyo kwa ajili ya kuulinda utawala wa Kizayuni wa Israel.