BUNDUKI ZAIDI YA 100 ZASALIMISHWA ARUSHA

Utekelezaji wa  zoezi la uhakiki wa Silaha  unaoendelea Mkoani Arusha  limewezesha kupatikana kwa Bunduki zaidi ya mia moja zikiwemo za kivita zilizokuwa zinamilikiwa na wananchi kinyume cha sheria katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama  ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw. Hashim Mgandila  amesema  Bunduki sita za kivita zilitelekezwa kwenye ofisi za vijiji. Na waliokuwa wanazimiki na kwamba zingine za kawaida licha ya wamiliki wake kuwa na vibali asilimia kubwa matumizi yake yanaonekana kuwa na utata.

Zoezi la kuhakiki silaha ni maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw.Daud Ntabenda linalolenga kudhibiti ongezeko la  matumizi mabaya ya silaha ambazo zimekuwa zikitumika kuua  wananchi wasio na hatia  tatizo ambalo ni kubwa zaidi katika wilaya ya Ngorongoro.

Mkoa wa Arusha unatajwa kuwa miongoni mwa Mikoa yenye watu wengi wanaomiliki silaha  ambazo asilimia kubwa licha ya wamiliki kuwa na vibali upatikanaji wake na matumiz yake yanadaiwa kuwa na utata.

UJUE UKWELI WA UCHAWI NA UNABII WA FIDEL CASTRO.

UJUE UKWELI WA UCHAWI NA UNABII WA FIDEL CASTRO.

"The US will come talk to us when it has a black president and the world has a Latin American Pope.”

Picha ya Fidel Castro ilo andikwa maneno hayo imekuwa ikisimbaa duniani kupitia mitandao ya kijamii, hasa hasa baada Katoliki kupata Papa wa Kilatin.

Pia nimeona rafiki zangu humu facebook wakiendelea kusambaza hiyo picha, leo hii nimeona nizame na kuchimbua ukweli wa utabiri huo, naam, nimelazimika kutafuta ukweli wa hiki kinaochoitwa unabii au uchawi wa Fidel Castro wa kuweza kuona mambo yajayo kabla hayajatukia.

Awali ya yote hakuna ukweli wowote juu ya kauli hii, huu ni uzushi kama uzushi mwingine wa mtandaoni na wa kwenye magazeti na majarida ambayo naweza kusema ya UDAKU. Ambayo siku zote hujitafutia umaarufu kwa kuwalisha maneno wasanii na wanasiasa maarufu.

Nukuu hiyo kumhusu Fidel Castro iliandikwa kwa mara ya kwanza na mwaandishi wa Kiagertina Bwa Pedro Jorge Silans katika jarida la "The Journal Of Carlos Paz" tarehe 10/03/2015.

Uzushi huu wa Bw Solans juu ya Fidel Castro ulimaanisha dhihaka ama istizai lakini katu hauwezi kuuita unabii sababu wakati unaandikwa kwa mara ya kwanza tayari Obama yuko ndani ya White House na Papa Fransis yuko Vatican akihudumu upapa. Nasema ni dhihaka na si unabii kutokana na sababu zifuatazo.

Mosi: Kwanini haya yajulikane baada ya miaka 40?

Tangu mwaka 1973 unaosemekana hayo maneno katamka Fidel Castro hayakujulikana au kuandikwa popote hadi  miaka 40 baadae tena ikiwa tayari Marekani ikiwa na rais mweusi na Katoliki kuwa na Papa wa kilatini? Kwanini mitandao au hilo jarida lilo andika kwa mara ya kwanza lilisubiri Whit house kuwa na rais mweusi na katoliki kuwa na papa wa kilatini?

Pili kwanini mwaka tu?

Solans anasema Mwaka ambao Fidel Castro amesema maneno hayo ni 1973, lakini hataji tarehe na mwezi. Maneno kama haya na tena utabiri mzito na hasahasa ukizingatia kupamba moto kwa vita baridi, iweje tarehe na mwezi wake usijulikane? Hiki ni kiashiria cha urongo na uzushi.

Tatu, Chanzo Cha Habari
Tarehe 10/03/2015 jarida la El Diario de Carlos Paz( The Journal Of Carlos Paz) liliandika makala yenye kichwa kisemacho " Cuba through changing times: The End Of the blockade?"

Mwandishi wa makala hiyo anaitwa Pedro Jorge Solans, pamoja na mambo mengine alo yaandika juu ya USA na CUBA, lakini pia alizungumzia huo utabiri wa Fidel Castro.

Solans amesema mwaka 1973 Kamanda Fidel Castro akiwa ndio kwanza akiwasili Havana akitokea Vietnam alizungumza na wanahabari wa kimataifa. Kipindi hicho vita baridi ilikuwa ndio imepamba moto, mwanahabari kiingereza aitwaye Bryan Davis akamuuliza Castro.

"Unafikiri ni lini hasa mahusiano kati ya Cuba na USA yatarejea tena?"

Fidel Castro akamkazia macho Davis kisha akamjibu.

"Marekani itakuja kukiri kwetu pindi wakiwa na rais Mweusi na Dunia ikwa na Papa wa kilatini" Hiyo nukuu iko kwa kiingereza ila nimeitafasiri hivyo.

Kwa mujibu wa Clarin gazeti maarufu la Argentina, wakati Solan akigundua kauli hiyo ya Caatro alikuwa Havana akifuatilia habari za mahusiano kati ya USA na Cuba.

Solan anasema alipokuwa Cuba alifanya mazungumzo na Dereva wa Tax Eduardo de la Torre aliyemhudumia , na katika mazungumzo hayo ndipo Solan akasikia kwa mara ya kwanza nukuu hiyo ya Castro kutoka kwa Eduardo. Eduard de la Torre ambaye kwa sasa ni Dereva Tax mwaka huo wa 1973 alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu.

Eduardo ni shabiki mkubwa wa Fidel Castro, yeye alimuona Castro kama nabii na alifananisha na Yesu Kristu pale alipomwambia Bw Solan

"Fidel Castro alifufuka mara nyingi kuliko hata Yesu Kristu, hivi unafikiri mara ngapi vyombo habari vya kimataifa viliripoti kuwa kamanda kafa lakini inatokea mzima?" Eduardo alisema kwa mtindo wa kutupia swali kwa Solans. Kwa ushabiki huu na utungaji huu wa hekaya Bwa Eduardo hafai kuwa chanzo cha habari cha kuaminiwa sana hususani habari hiyo ikimuhusu Castro.

Sasa ni ajabu sana maneno ya Dereva wa Tax katika mitaa  kubebwa na mwandishi huyu mazimamazima ikiwa jiji la Havana linasifika kwa nukuu za kuwalisha maneno watu maarufu. Bw Solan hakutakiwa kumtegemea Eduardo pekee kama chanzo sahihi cha habari yake ikiwa mwandishi anayeaminiwa kumuuliza swali hilo Castro yuko katika jijini London na sasa hiv mlevi mbwa, namaanisha angejiridhisha japo kwa kumuuliza Bryn Davis pia.

Nne: Kwanini vyombo vya habari vya Cuba na kimataifa havijaripoti?

Huenda nukuu hiyo ya Fidel Castro ni sahihi, lakini naingiwa na shaka kwasababu hakuna kumbukumbu rasmi ya kiserikali ikionesha kuwa Fidel Castro aliwahi kuzungumza na wanahabari kisha akatamka maneno hayo, lakini pia hakuna chombo chochote kilicho ripoti mkutano huo na maneno hayo hadi pale yalipokuja kuandikwa kwa mara ya Kwanza na Bw Solan.

Tumeona Whitehouse kuna rais mweusi na dunia ina papa wa kilatini, na hivi majuzi tu tumeona Obama akizulu Cuba, hivi kwanini vyombo vya kimataifa havijarejea maneno haya ya Castro wakati vikiripoti ziara ya Obama Cuba? Hiki ni kiashiria tosha kuwa Bw Solan aliamua tu kudanganya ulimwengu.

Hata hivyo, Bw Solans hakujishughulisha kuthibitisha maneno ya Eduardo kwa kutumia kumbukumbu za kihistoria au huenda alifanya hivyo lakini akawa amekosa kumbukumbu hizo, na kubwa zaidi hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha madai yake.

Rafael Rojas, author of A Brief of tha Cuban Revolution aliliambia gazeti la Mexico El Universal kuwa "Siamini hata kidogo kuwa Fidel Castro aliwahi kuzungumza maneno haya ya kinabii"

Rojas anasema iwe Castro au mtu yeyote lakini maneno hayo yamezushwa kama masihara mengine tu, kuonesha jambo fulani ni muhari kutokea, mathalani Cuba kuna msemo maarufu "it will happen when a frog grows hair"

Tano: Fidel Castro ni mbovu katika utabiri.

Wengine wanasema maneno hayo ya uzushi yanauhusishwa na mahojiano kati ya Fidel Castro na Barbara Walter yalofanyika mwaka 1977. Katika mahojiano hayo Feidel Castro alimwambia Barbara huenda USA na Cuba zitarudisha mahusiano  kati ya mwaka 1980 na 1984  kipindi ambacho Jimmy Carter akihudumu awamu yake pili Whitehouse.

Mahojiano ambayo yalibatilisha unabii wowote wa fidel Castro alio wahi kuutoa sababu mwaka 1980 Ronald Reagan alimuondoa Carter Whitehouse kwa ushindi wa kishindo. Kwa hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwa Castro kuwa sahihi na utabiri huu ikiwa utabiri kama huo alio uhusisha na Jimmy Carter ulifeli.

Bofya link hiyo kuona video ya mahojiano kati ya Castro na Barbara ya mwaka 1977.

http://abcnews.go.com/International/video/fidel-castros-prediction-normal-relations-us-27703096

Mwisho.

Ni aibu sana kwa mtu yeyote, kuokota kitu katika mtandao na kisha ukakisambaza bila kukifanyia utafiti, inakuwa aibu kubwa sana jambo hili likifanywa na masomi, lakini fedheha likifanywa na anayetegemewa na anayeigizwa.

Njano5
0622845394

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUUNDA JESHI LA PAMOJA

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUUNDA JESHI LA PAMOJA.

Jumuiya ya Afrika Mashariki ,EAC, inakaribia kuunda jeshi la pamoja kwa lengo la kulinda taasisi muhimu za kiuchumi za nchi wanachama.

Hayo yamebainika wakati wa mafunzo ya pamoja mjini Nairobi ya wanajeshi 300 kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda.

Kamanda wa Majeshi ya Kenya Jenerali Samson Mwathethe amesema kikosi hicho cha pamoja ni muhimu kwa kuzingatia matarajio makubwa ya ustawi wa kiuchumi Uganda na Kenya kutokana na uzalishaji mafuta na gesi asilia Tanzania.

Akizungumza Ijumaa wakati wa mazoezi hayo Jenerali Mwatheteh amesema, “Shirikisho limeanza kupata muundo wake hatua kwa hatua kama ilivyopangwa na nchi zote za EAC ikiwemo Sudan Kusini. Eneo hili lina ukubwa wa mita mraba milioni 2.4 na idadi ya watu milioni 170. Nchi zote wanachama zinafungamana na udumishwaji amani na usalama katika eneo.”

Mkuu wa Jeshi la Kenya amesema ugaidi ni tishio kubwa zaidi la usalama katika eneo na hivyo nchi zote zinapaswa kushirikiana. Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Ulinzi wa Kenya Raychelle Omamo amesema mafunzo hayo ya maafisa wa kijeshi ni katika fremu ya ushirikiano wa kiulinzi baina ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha amesema vikosi vya usalama vinapaswa kufahami mbinu za makundi ya kigaidi yanayolenga kuvuruga uchumi wa eneo hilo.

KWANINI NDEGE ZA ABIRIA HAZINA PARACHUTI?

NGOJA NIKUJUZE mwanaKISIMA.

Kwa nini ndege ya abiria haina parashuti?

Ndege ya kivita si kama tu ina parashuti, bali pia ina kiti chenye parashuti kinachomrusha rubani, kama dharura itatokea, kiti hicho kitanmrusha rubani, kisha parashuti itafunguka ili kuhakikisha rubani anashuka kwa usalama. Kiti hiki ni kizito kuliko mtu.

Kuweka viti hivi katika ndege inayoweza kubeba abiria zaidi ya 100 ni jambo lisilowezekana, kwa sababu viti zaidi ya 100 ni vizito kupita kiasi.

Aidha, rubani wa ndege ya kivita akirushwa nje, atapita kwenye kitu kama kifuniko kilicho juu yake, na jambo hili haliwezekani kufanyika kwenye ndege za abiria.

Baadhi ya wahandisi wanajaribu kusanifu ndege ya abiria ambayo paa lake linaweza kufunguliwa na parachuti kubwa itakayoweza kurusha chumba kizima cha abiria. Lakini mpango huo una utatanishi mkubwa. Idadi ya abiria itapunguzwa kwa kiasi kikubwa, na bado haijajulikana kama parachuti kubwa inaweza kufunguliwa na chumba kurushwa kwa mafanikio. Hivi sasa hakuna kiwanda chochote kinachopenda kutengeneza ndege za aina hiyo, na pia hakuna mashirika yoyote ya ndege yanayopenda kutumia ndege zinazobeba abiria wachache.

Kutokana na sababu hizi, parashuti hazitumiwi katika ndege za abiria, bali zinatumiwa katika ndege ndogo zinazobeba watu wachache tu.

KWANINI NDEGE HAFI ANAPOSIMAMA KWENYE UMEME?

Kwa nini ndege hauawi anaposimama kwenye waya wa umeme?

Umeme unaotumika majumbani kwetu una nyanya mbili, moja ina moto na nyingine haina moto. Umeme unaopita kwenye nyaya za Tanzania ni voti 230. Kama mtu akigusa nyaya mbili, au waya wenye moto na ardhi kwa wakati  mmoja, tofauti ya shinikizo la umeme kati ya pande mbili itasababisha mkondo wa umeme kupita mwili wake, na anaweza kuumia au hata kufa. Lakini ni kwanini ndege wanagusa nyaya hizo bila kuumia? Ni kwa sababu anasimama kwenye waya mmoja tu, mkondo wa umeme hautapita mwili wake.

Lakini kama ndege akisimama kwenye waya wenye shinikizo kubwa sana, tofauti ya shinikizo la umeme kati ya miguu  yake miwili itasababisha umeme kupita mwili wake na kumdhuru?

Tofauti ya shinikizo la umeme iko kati ya miguu yake, lakini ni dogo sana, hivyo ni umeme mdogo sana unaopita mwili wake, hivyo hautamdhuru hata kidogo.

PRINCE MURO YAKIVAA KITUO CHA BRT

Proncess Muro ilifanya yake kwa kuingia kituo cha BRT. kwa vyovyote vile itakuwa ilikuwa inashuka na ile road ya kati ya brt sasa kafika down nahis akapitiliza mpk ndan ya kibanda.

Hakuna aliyekufa, huenda ndio majaribio ya mradi wa mabasi yaendayo kasi!! Tutakufa wengi.

VIDEO: HIVI NDIVYO MKUU MKOA ALIYETEMWA NA ALIVYO JIDHALILISHA



UNAJIDHALILISHA KISA UKUU WA MKOA.Unaweza kuwaMtu mzima, yaani si kijanaMsomi, yaani unadegree zakolakini ukafanya mambo ambayo hata mtoto akakushangaa, na yule wa darasa la saba kama mimi pia nikakushangaa!Hivi nini hasa cha mno hata mtu ujidhalilishe? Sasa huyu msomi hapa anaongea pumba tu kama vile cheo cha ukuu wa mkoa kina hati miliki.Full kujipendekeza, sijui ataka apewe shavu lingine, "ati anaomba radhi" pumbavu, kama angekuwa baba yangu nyumbani angekutana na makofi.

Posted by Kisima cha Jangwani on Friday, March 25, 2016

AJALI YAUA WAWILI KENYA

Watu wawili wamefariki na wengine 16 kujeruhiwa baada ya Matatu kugongana ana kwa ana na basi kwenye barabara ya Kakamega-Mumias nchini Kenya. 

Waliofariki ni pamoja na dereva wa matatu hiyo na abiria aliyekuwa amekaa kwenye kiti ya mbele.
Ajali hiyo imetokea karibu na mji wa Joyland kilomita 3 kutoka mji wa Kakamega.

KOREA YA KASKAZINI YATIA JAMBAJAMBA BLUE HOUSE.











KOREA YA KASKAZINI YATIA JAMBAJAMBA BLUE HOUSE.

Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.
Zoezi hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong-un,kulingana na chombo cha habari cha KCNA ambaye alilitaka jeshi kujiandaaa kuivamia na kuiharibu serikali ya kusini.
Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za Pyongyang.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi lake kuwa katika hali ya tahadhari.
Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa Korea Kaskazini.

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.
Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani, kusini mwa mpaka wake.

Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake ,ripoti hiyo iliotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House hadi kuwa jivu.
Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini.

Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa,lakini ripoti hiyo ilionya mwisho mbaya wa rais Park.
Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.
Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park Chung-hee halikufanikiwa,raia saba wa Korea Kusini pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini waliuawa.