KIZA, MUNGU, KIFO, VITA, NJAA NA MARADHI.
Mungu(light) na
Kiza(Darkness) ni ndugu. Hakuna aliyeumba, wametokea tu, lakini wa
kwanza kutokea KIZA kisha akafuatia NURU (Mungu).
Kiza ni
mwanamke, Mungu ni mwanaume, wakati Kiza ni mkubwa kwa umri na hata
nguvu kumzidi Mungu, Mungu yeye ni mwingi wa hila na ujanja, kwa hivyo
ni mwerevu kumzidi KIZA.
Mungu alifanya hila, na kwa hila yake
hiyo akaweza kuumba ulimwengu na malaika wakubwa wanne, ambao ni
Mikaeli, Lusifa, Rafaeli na Gabrieli.
KIZA akachukia na kwahivyo
pakazuka mapigano kati ya KIZA na Mungu. KIZA anaamini kuwa ulimwengu
ambao angeumba yeye ungekuwa bora kuliko huu alio uumba Mungu, na ya
kwamba Mungu alijua hilo na alimuonea wivu KIZA.
Inasemekana
KIFO(Death) kilizuka pamoja na MUNGU, au kilianza kabla ya Mungu, au
kilizuka muda mfupi sana baada ya kuumbwa malaika wanne. Ila mjue KIFO
ni moja kitu kikongwe kuwapo, na haijulikani kati ya KIFO na Mungu nani
mkubwa, wanaweza kuwa sawa kwa umri au KIFO akawa mkubwa au Mungu akawa
mkubwa. Yote ya yote, wakongwe wa wakongwe kabla hata ya ulimwengu
haujaumbwa ni KIZA, MUNGU na KIFO.
Kwakuwa Kiza kina nguvu kuliko
Mungu, ili mlazimu Mungu kusaidiana na malaika wakubwa kupambana na
Kiza, katika mapambano hayo Mungu na malaika wake hawakufanikiwa kumuua
Kiza, walichoweza kumfunga Kiza kwa kutumia chapa(mark) ambayo baadae
ilijulikana kama chapa ya Kaini(Mark of Cain)
Kitendo cha
mapigano hayo kati ya MUNGU na KIZA, kina maanisha kuwa "VITA" ni kitu
cha nne kikongwe kikiwa nyuma ya KIFO, MUNGU na KIZA.
Baada
Mungu kufanikiwa, KIZA chini ya kifungo chake akawa juu vilindi vya
maji, Mungu akaketi juu ya uso wa maji, na wakati huo asilimia kubwa ya
ulimwengu ulikuwa ushafanyika kasoro sayari dunia ilikuwa bado
haijakamilika. Hata hivyo, kimsingi hata sasa ulimwengu unaendelea
kutanuka na kukua na kila siku nyota zinapasuka na kila siku mifumo ya
nyota inazaliwa, yote yanafanyika chini ya pumzi ya Mungu(physical laws)
Chapa ikawa ndio kifungo na funguo kwa GEREZA alilofungiwa DARKNESS, na
funguo ambazo alikabidhiwa mtoto mpendwa, mtiifu na mnyenyekevu wa
Mungu, mtoto huyo ni Lucifer.
Chapa(funguo) ikageuka laana,
hajulikani kwanini iligeuka laana, ila inasemekana MFUNGWA(KIZA)
alifanya funguo kuwa LAANA kama mbinu ya kutoka kifungoni. LAANA
ikamfanya Lucifer kuwa na kibli, na kibli kilionekana pale Mungu
alipomuumba mwanadamu, Lucifer alichukia na alikataa kumsujudia Adamu.
Naam LAANA IKAWA UASI, na baadaye Lucifer akatimuliwa mbinguni na jeshi
la Mikaeli(Michael)
Wanyama wa kwanza kuumbwa walikuwa wanaitwa
leviathians, hawa wanyama walikuwa na njaa sana kiasi walane wenyewe kwa
wenyewe, na kwasababu hiyo basi tunagundua kuwa "NJAA" ni kitu cha tano
kikongwe nyuma ya VITA, ingawa kiumri Levithians alianza kisha ndio
akafuatia "NJAA"
Baada ya hapo Mungu akamilisha sayari dunia kwa
kumuumba mwanadamu, mwanadamu ambaye tuliona Lucifa aligoma kumsujudia.
Binadamu anashikwa na maradhi na udhohofika kwa kuugua. Kwasababu hii
basi tunagundua "MARADHI" ni kitu cha sita nyuma ya "NJAA"
KIZA,
MUNGU, KIFO, VITA, NJAA na MARADHI hivi vyote viko na vilizuka tu na
hakuna aliyeviumba. Viumbe wa kwanza kuumbwa na mungu ni malaika, na
wanyama wa kwanza kuumbwa na mungu Levithans ambao pia wanatajwa katika
Isaya 27:1
Kwakuwa Mungu aliumba binadamu, na kwakuwa Levithans
walikuwa ni wanyama hatari sana kwa uhai wa binadamu hasa hasa kutokana
na kuathiriwa zaidi na njaa, Mungu akaumba Purgatory kisha akamuagiza
Malaika Mikaeli awafukuze levithians duniani na kuwafungia Purgatory.
Katika Purgatory Levithians wanaendelea kuishi huku wakiendelea kulana
wenyewe kwa wenyewe na huku wakizaana.
Unafikiri ile mijusi
mikubwa unayo iona katika filamu imepotea tu? Akina GodZilla wajua
wameenda wapi? Elewa hawakupotea bali wamefungiwa katika Purgatory! Ndio
Levithians wenyewe hao, na ili waweze kufungiwa "VITA" ilitamalaki na
Mikaeli akafanikiwa kuwafungia, waliokufa ndio mnaona masalia yao ya
mifupa katika majumba ya makumbusho.
Baadae dunia itaenda mwisho,
nakumbuka nilishawahi kuwaandikia juu ya mwisho wa dunia, kitakacho
fanya dunia iishe ni kuripuka kwa nyota jua, likitokea hilo uhai katika
dunia utatoweka kabisa, lakini huo sio mwisho wa ulimwengu.
Ulimwengu nao utaisha ama utafikia mwisho. Mkumbuke kuwa ulimwengu
unaendelea kutanuka na sababu ya kutanuka ni kuendelea kushikilia
misingi ya mlango uliotumika kumfungia KIZA. Hata hivyo, kutanuka huku
kutapelekea ulimwengu kupasuka na kusambaratika, hapa wana sayansi
wanasema kuwa ule mchakato wa BING BANG unaanza tena na kwa hivyo
ulimwengu na galaxy zake kuumbika tena.
Kwa upande wa wanasayansi
Bing Bang kutokea tena ni mchakato wa matirioni ya miaka, na mchakato
huo unahusisha physical law, matters, dark matters, energy, na dark
energy. Tukija upande wa kiroho huu ndio wakati ambapo "KIZA" kimetoka
kifungoni na kiko vitani na MUNGU.
Kama Mungu akishinda
ulimwengu utarudi tena na dunia kuwa Paradiso, na kama KIZA akishinda
basi ataumba ulimwengu wake na kwa vyovyote vile wakati huo MUNGU
atakuwa amefungwa au ameuliwa.
Mwisho wa dunia utakuwa na dalili nyingi lakini dalili kuu nne ni hizi zufuatazo.
1. NJAA atapata nguvu sana, na chakula kitakuwa hakitoshi ulimwenguni.
Hakitoshi haimaanishi chakula cha kutosha hakuna, hapana, bali watu na
wanyama watakula lakini hawatashiba.
2. MARADHI naye atapata
nguvu sana, si kwamba magonjwa yatakuwa mengi, bali magonjwa yaliyo kuwa
yanatibika yataanza kuwa sugu na kukataa dawa, lakini pia yatazuka
magonjwa mapya yaso na dawa wala chanjo.
3. VITA naye atapata
nguvu, itakuwa ni vita kati usasa na uzamani, ukristo na uislamu, weusi
na weupe, magharibi na mashariki, shia na suni, katoliki nautherani,
taifa na taifa, kabila kabila.
4. KIFO naye atapata nguvu, na
vitu hivyo vitatu vya juu vinaonesha uwepo wa KIFO, na uwepo wake
utadhihirishwa na mauji ya halaiki yatakayo sababishwa na NJAA, MARADHI
na VITA.
Hata hivyo na hasa kwa mujibu wa biblia kuwa "KIFO"
atauliwa na MUNGU, na hili linathibitishwa na nadharia ya biblia kuwa
YESU ameshinda MAUTI na ya kwamba atakayemuamini YESU na BABA aliyemtuma
HATAKUFA bali ataishi milele. Sasa ili kuwe na maisha ya milele ni
lazima "KIFO" afe, yaani asiwepo!
Yohana 5:24
Je Mungu
ataweza kumuua "KIFO"?? je kama Mungu anampango wa kumuua "KIFO" je
"KIFO" hatofanya hila kwa kumfungulia "KIZA" toka gerezani? Kwa maana
hakuna kitu ambacho Mungu anakihofia kama "KIZA" Je katika haya yote,
mitume na manabii wana nafasi gani? Je vitabu kama Quran na Biblia pia
vina nafasi gani? Kuna tafauti gani kati ya Hell na Purgatory?
Itaendelea
Njano5
0622845394